Feb 16, 2017
Sababu 15 Zinazopelekea Kushindwa Katika Maisha Yako Wakati Wote.
Kama
wewe ni msomaji mzuri wa vitabu sina shaka na wewe, naamini umeshawahi kusoma kitabu cha ‘Think and Grow rich’ kilichoandikwa na
Napoleon Hill miaka mingi ya nyuma.
Katika
kitabu hiki mwandishi ameandika mbinu mbalimbali ambazo zinaweza kukusaidia na kukutoa kutoa kwenye umaskini hadi kuweza kufikia
ngazi ya utajiri.
Hiyo
haitoshi, Napoleon hill pia kupitia
kitabu hiki, ameweza kuandika kwa ufasaha sababu 30 ambazo zinapelekea watu
wengi kushindwa katika maisha wakati wote.
Kupitia
makala yetu haya ya leo nataka nikushirikishe kwa ufupi baadhi ya sababu hizo
muhimu ambazo hufanya maisha ya watu wengi kushindwa kufanikiwa na kuishi kwenye
umaskini.
Zifuatazo
Ndizo Sababu 15 Zinazopelekea Kushidwa Katika Maisha Wote.
1. Kukosa malengo maalumu.
Kama
unaishi bila ya kuwa na malengo maalumu, hujui unapokwenda kwenye maisha ni
sababu tosha itakayokufanya ushindwe katika maisha yako. Ishi kwa malengo
ujenge mafanikio yako.
2. Kukosa nidhamu.
Hakuna
mafanikio ambayo unaweza ukayapata bila ya kuwa na nidhamu. Inatakiwa uwe una
nidhamu karibu katika kila eneo la maisha yako. Wengi wanaoshindwa katika
maisha kiukweli hawana nidhamu.
3. Kuahirisha mambo.
Pia
kuahirisha mambo inatajwa kama sababu ya kukufanya ushindwe katika maisha. Kama
kuna jambo unataka kulifanya,hebu lifanye wakati huo huo. Acha kusubiri kesho
utapotea.
4. Kukosa nguvu ya kushikiria.
Wengi
nao wanashindwa kwa sababu hawawezi kunga’ng’ania. Ikiwa unataka kufanikiwa
lakini huna maamuzi ya kuwa mbishi sahau mafanikio. Hii ni dunia inayotaka uwe
mbishi kweli mpaka ufanikiwe kimafanikio.
5. Mtazamo hasi.
Hiki
pia ni kikwazo kikubwa cha mafanikio kwa watu wengi. Kama wewe una mtazamo
hasi, hauwezi kufanikiwa. Mafanikio yanajengwa kwa mtazamo chanya.
6. Kukosa maamuzi sahihi.
Ikiwa
kila wakati huna maamuzi sahihi, kwa mfano, maamuzi ya kukusaidia kufanikiwa,
tambua upo pia kwenye eneo la kushindwa kila wakati. Maamuzi bora ni nguzo au
njia sahihi ya kukufanya ukafanikiwa wakati wote.
7. Woga.
Pia
mwandishi ameeleza kwamba maisha ya wengi yamejawa na hofu sana. Sasa hiki nacho
ni kikwazo kikubwa cha kuweza kufika mafanikio makubwa. Ni lazima kuishinda hofu
ili kufikia mafanikio yoyote katika maisha yako.
8. Kujiwekea tahadhari sana.
Kuna
watu ambao wao hawataki kukosea kabisa. Ni watu wanaotaka kuwa wako kamili kila
wakati. Ili ufanikiwe ni muhimu ukajua kukosea pia ni ngazi ya kukusaidia kuweza
kufanikiwa. Kosea, jifunze na songa mbele.
9. Kukosa nguvu ya uzingativu.
Inatakiwa
mawazo yako yawe kwenye kile unachokifanya mpaka ufanikiwe. Kama mawazo
yako unayapeleka sehemu tofauti huwezi kufanikiwa. Kwa kila unachokifanya,
zingatia hapo kwanza.
10. Kukosa uvumilivu.
Maisha
yanaenda sambamba na kuwa mvumilivu. Kuna wakati unaweza kukutana na magumu
sana, lakini ukishindwa kuvumilia ndio basi tena huwezi kufanikiwa.
11. Kukosa ushirikianao na wengine.
Huwezi
kufanikiwa kama huna ushirikinao mzuri na watu wengine. Mafanikio ni
kutegemeana, hasa katika suala la kushirikiana. Ni muhimu sana kushirikiana na
wengine ili kuweza kufanikiwa.
12. Kukosa mtaji.
Watu
wengine pia wanashindwa kufanikiwa kwa sababu ya kukosa mtaji. Ingawa katika
hili sio sababu kubwa sana kwa sababu unaweza ukajipanga na kisha ukapata mtaji baada ya muda fulani.
13. Kuishi kwa kuhisi sana.
Pia
kuna wengine wanashindwa kufanikiwa kwa sababu ya kuishi kwa hisia. Utakuta badala
ya kufanya jambo fulani kwa uhakika, mtu anawaza tu kwamba nitafanya kesho au
hata nisipofanya hakuna shida.
14. Kuingia katika biashara isiyo
sahihi.
Kama
upo kwenye biashara ambayo haipo sahihi, pia ni rahisi kuweza kushindwa katika
hilo jambo unalolifanya. Inatakiwa kuwa makini na kichagua biashara ambayo ni
sahihi kwako na ambayo itakupa mafanikio.
15. Kuingia katika mahusianao mabovu.
Hakuna
kitu kibaya kama kuingia katika mahusiano mabovu. Unapojiingiza katika
mahusianao mabovu ni chanzo kingine kinachoweza kukufanya ukashindwa katika
maisha yako.
Ukichunguza
na kuangalia hizo ndizo sababu zinaweza kukufanya ukashindwa wakati wote,
haijalishi unafanya nini kama una sababu hizo nyingi ni lazima utashindwa.
Endelea
kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama
makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja
tena kwa ukaribu. Kujiunga tuma neno THE
UNIVERSITY OF WINNER’S, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA
KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni
wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.