Feb 2, 2017
Mafanikio Makubwa Yanajengwa Sana Na Mambo Haya.
Watu wengi wenye mafanikio makubwa kiuchumi huwa ni watu wa kufanya mambo fulani ambayo yanawasaidia sana kujenga mafanikio yao kila siku. Kwa kufanya
mambo hayo huweza kuwaongoza moja kwa moja kufikia mafanikio makubwa katika
maisha yao.
Na mara nyingi watu hawa wenye mafanikio makubwa,
kwao inakuwa ni vigumu kuweza kuacha kufanya mambo hayo. Huwa ni watu wa kufanya
mambo hayo karibu kila siku na kila mara.
Katika makala haya tutaangalia mambo muhimu
yanayojenga mafanikio. kama nilivyosema haya ni mambo ambayo yanatumiwa karibu na watu wote
wenye mafanikio makubwa. Hata wewe unaweza ukajifunza mambo haya leo na kujenga
mafanikio makubwa.
Fuatana nasi katika makala hii kuyajua mambo hayo
zaidi:-
1.
Kujifunza.
Hili ndilo jambo la kwanza linajenga mafanikio yoyote
yale. Maisha ya watu wote wenye mafanikio makubwa kwa sehemu kubwa yametawaliwa
na kujifunza sana.
Leo hii kama umeamua kujenga mafanikio yako makubwa
ni lazima ujifunze tena sana na kila siku. Hii ni tabia ambayo itakupelekea kukufikisha
kwenye mafanikio makubwa sana.
2. Kuweka
vipaumbele.
Siri nyingine ya kujenga mafanikio makubwa ipo
kwenye kuweka vipaumbele. Ili kufanikiwa ni lazima uwe mwekaji mzuri wa mipango
yako kwa kuzingatia vipaumbele zaidi. Tambua bila kuweka vipaumbele itakuwa ngumu
sana kwako kuweza kufanikiwa.
3. Kujitoa
mhanga.
Mafanikio yote mara nyingi yanategemea pia kujengwa
na tabia ya kujitoa mhanga ambayo unatakiwa kuwa nayo. Unapojitioa mhanga
inakusaidia kufanya maamuzi magumu ambayo kwa mtu wa kawaida ni lazima
ataogopa.
4. Nidhamu
binafsi.
Hauwezi kufanikiwa kama kwenye maisha yako huna
nidhamu binafsi. Mafanikio makubwa yanajengwa sana na nidhamu ambayo inatakiwa
ikuongeze kila siku hadi kufikia kilele cha mafanikio yako.
5. Kufanya
kazi kwa bidii sana.
Hakuna mbadala wa hili kama una lengo la kutoka
kwenye umaskini. Ili ufanikiwe unatakiwa kufanya kazi haswa tena sio kazi ya
kitoto. Unapojituma kila siku mafanikio yatake yasitake ni lazima yatakuja
upande wako.
6. Ung’ang’anizi.
Kwenye maisha zipo changamoto nyingi sana. Sasa ili
uweze kujenga mafanikio yako kwa uhakika ni lazima unatakiwa kuwa mbishi wa
mafanikio yako. usikubali kushindwa kirahisi, hiyo itakuwa ni hasara kubwa sana
na utashindwa kufanikiwa.
7. Kuuliza.
Kujenga mafanikio makubwa ni lazima kila wakati
ujiulize maswali yatakayokusaidia kukutoa hapo walipo na kwenda ngazi nyingine
kimafanikio. Usiwe msikilizaji au mpokeaji wa moja kwa moja bila kupata muda wa
kudadisi na kuuliza. Uliza upate msaada na kujenga mafanikio yako.
8. Maliza
kile unachokianza.
Watu wenye mafanikio si waanzaji tu wa mambo mapya
mengi, bali pia ni watu wa kumaliza kile walichokianza. Wanapopanga mipango yao
ni lazima mwisho wa kumaliza wauone na ndicho kitu ambacho kinakuwa
kinafanyiika mpaka kufikia ndoto zao.
Endelea
kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama
makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja
tena kwa ukaribu. Kujiunga tuma neno THE
UNIVERSITY OF WINNER’S, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA
KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni
wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.