Feb 27, 2017
Malezi; Watoto Wasitumike Kama ‘Risasi’ Za Kushambuliana Sisi Wenyewe.
Mfumo
dume umekuwa na mwelekeo wa kuchochoea utoaji wa talaka kwa wana ndoa kirahisi
sana. Utakuta wanaume huamua kuwapa talaka wake zao hata kwa makosa madogo
madogo tu.
Na
wanapofanya hivyo huhakikisha kuwa akina mama hao hawaondoki na kila kitu. Mara nyingi
wamekuwa wakiondoka bila chochote, msaada wowote na hata bila watoto wao.
Wengi
wetu tumekuwa hatushituki, tunapowaona wanandoa ambao walikuwa wakipendana
wakipeana talaka. Na vile vile tukiwawekea utaratibu wa kuwasaidia wanandoa
wanao achana, ili waweze kupona kihisia na kiakili.
Lakini,
jambo la kukumbuka ni kwamba, unapompa talaka mwenzako, maana yake unamkana na
kuondoa msamaha wako, upendo wako, na uaminifu wako kutoka kwake.
Pia,
kuishi maisha ya useja ni jambo lililogumu hata zaidi. Iwapo wewe bado ni
kijana na damu yako inachemka, kuishi maisha ya peke yako kunakufanya ukose
usalama, uwe na hofu ya kukufanya upate maradhi yatokanayo na hisia. Lakini,
pia upweke na kadhia zingine nyingine huwezi kuvikwepa.
Ni
kweli kuwa, ndoa ni jambo jema na linalokubalika na jamii. Lakini iwapo ndoa
itakuwa na matatizo au migogoro, wanandoa watapaswa wafanye nini? Ukweli ni
kwamba, ni lazima pawepo na mlango wa nyuma wa kutokea. Tunapaswa tukumbuke
kwamba, tunapoona kuna kitu kinachoitwa talaka, tujue tunapoelekea si pazuri.
Kuufahamu
ukweli huu kutakusaidia tuepukana na matatizo, sisi na watoto wetu. Ingawa
lengo si kutalakiana, lakini dunia yetu hii ni kubwa, na lolote lile linaweza
kutokea.
Vilevile
ukweli ni kwamba, wanandoa wanapotalikiana huendelea kubaki na maumivu au
mateso kwa miaka mingine ipatayo kumi. Hali huwa mbaya zaidi kwa watoto.
Kwa
mujibu wa kitabu kiitwacho Second chances
kilichotungwa na kuandikwa na Sandra
Blakeslee na Judith Wallerstein,
ambao walifanya utafiti wa muda mrefu unaohusu madhara yanaotokana na talaka.
Katika
utafiti wao wanasema kwamba, hata kama talaka itatolewa katika njia halali na ya
haki, bado huo ni udanganyifu wa kihisia tu, kwani madhara yake huendelea
kuwepo.
Pia
wanasema kwamba, talaka ndiyo sehemu pekee katika maisha ambayo watoto hutumika
kama risasi za kushambuliana sisi wenyewe, yaani mke na mume. Talaka ina
maumivu makali kushinda matatizo ambayo
inajaribu kuyatatua.
Hata
hivyo, jambo la kukumbuka ni kuwa, ndoa siyo kamilifu kwa sababu inaundwa na
binadamu wasiokuwa wakamilifu. Licha ya ukweli huo, bado uwezekano upo
kuboresha zetu. Na tutaweza kufanya hivyo, iwapo tutakuwa na uelewa wa kutosha
unaohusu ndoa.
Ni
Baraka ya aina yake ikiwa utaamua kusali na kujiandaa kwa ajili ya ndoa yako. Bila
shaka kuna matatizo mbalimbali kwenye ndoa. Lakini iwapo kila mwanandoa
atakubali kuwajibika kikamilifu, ndoa inaweza kuboreka kila mwaka, na kisha
kuleta furaha, kuongeza na kukuza urafiki wa wanandoa.
Endelea
kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Tunakutakia
kila la kheri,
Imani Ngwangwalu,
0713
04 80 35,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.