Mar 10, 2017
Badili Jinsi Unavyofikiri, Utengeneze Maisha Ya Mafanikio Makubwa.
Ukweli ni kwamba,
hatuhitaji pesa kubadili jinsi tunavyofikiri. Kwa maisha yetu yalivyo, sisi
sote tuna uwezo wa kubadili jinsi tunavyofikiri bila kutumia gharama yoyote.
Habari mbaya ni
kwamba, wakati mwingine ni
vigumu kubadili kiini cha imani tuliyokuwanayo juu ya pesa, kwasababu imani hii
tumerithi kutoka vizazi na vizazi na wakati mwingine yawezekana tulijifunza
kutoka kwa ndugu na jamaa, marafiki zetu wa kazini na shuleni/vyuoni.
Lakini,
pamoja na kukulia katika mazingira haya, habari njema ni kwamba bado
inawezekana kubadilika.
Unaweza kubadili jinsi unavyofikiri juu ya matatizo yaliyopo, kwa kuanza kuimarisha fikra zako ili ziwe za tofauti na siku zote. Hatua ya pili ni kuchukua hatua, hii ikiwa ni pamoja na kutenda au kuyafanyia kazi mawazo yako.

Hatua ya tatu ni
matokeo ya hatua ya kwanza na ya pili, nikimaanisha kwamba ukichukua hatua kwa
maana ya kuyafanyia kazi yale yote mazuri uliyoyafikiria kwa usahihi mwanzoni,
matokeo yake ni kwamba utapata suluhisho ya matatizo yaliyokuwepo.
Ukipata suluhisho
watu wengine watakuletea pesa hali hii itakuwezesha kupata pesa na hasa uhuru
wa kipato. Katika hali ya kawaida ili tupate pesa inatubidi kufuata mzunguko wa
vitu vitatu “Fikiri—Chukua hatua—Pata pesa”.
Ili kuweza kubadili kile unachofikiri ni lazima kuacha kutumia akili ya hisia. Akili ya hisia ni pale unapoijiwa na vitu kichwani lakini huna uhakika kama vipo, unaishia kudhani basi! Sehemu kubwa ya kuwa binadamu ni kuwa binadamu. Na kuwa binadamu maana yake ni kuwa na hisia. Watu wote huwa tunahisi woga, uzuni, hasira, upendo, chuki, maudhi, furaha n.k. Kinachotufanya kuwa watu binafsi ni namna ambavyo tunashughulikia hisia zetu.
Katika uhalisia wa maisha, hakuna binadamu anayeweza kumzuia binadamu mwenzake na hisia. Kwakuwa tunao uhuru wa kuwa na hisia, kinachotakiwa ni kutokimbilia kutenda au kuchukua hatua kwa kufuata nguvu ya hisia tulizonazo.
Pindi unapopata
hisia fulani, ni kazi yako kwenda hatua ya kutafuta ukweli juu ya hisia zako na
baada ya hapo unaweza sasa kufanya maamuzi ya kuchukua hatua kwa vitendo.
Linapokuja suala la kuwekeza pesa wote huwa tunapata woga na woga mara nyingi huwa ni hisia zaidi kuliko ukweli halisi. Hata matajiri nao wanapata woga linapofika suala la kuwekeza pesa zao. Tofauti ni jinsi tunavyodhibiti woga tulionao au hisia tulizonazo.

Kwa watu walio
wengi, hisia za woga ndizo uwatengenezea fikra: mfano kutokana na woga wa
kupoteza pesa, mtu anapata fikra ya kwamba "itunze pesa yako mahala ambapo
zitakuwa salama” au “Ukikopa utafirisika na kufa maskini” n.k.
Kwa watu ambao ni matajiri hofu na woga wa kupoteza pesa huwafanya wafikiri na kupata fikra ya kwamba: “iwekeze pesa yako kwa umakini”; “Jifunze kushughulikia hasara na hatari za biashara”; “kuwa na mkakati wa kisheria kulinda utajiri wako n.k.
Tunachojifunza hapa kati ya tajiri na maskini ni kwamba watu wote tunakuwa na hisia sawa juu ya pesa yetu, lakini fikra tofauti; tabia tofauti; matendo tofauti na mwisho wa siku tunapata matokeo (utajiri) tofauti.
Jambo la pili tunaloweza kujifunza kutoka kwa matajiri ni kwamba, mafanikio yetu yanahitaji zaidi ya elimu rasimi. Kuwa na elimu rasimi peke yake, bila kubadilisha hisia zetu za ndani, imani, tabia na mtazamo n.k. hatutaweza kufika popote zaidi tutaishia kupata maumivu makali kutokana na muda mwingi tulioutumia shuleni kutafuta elimu rasimi ambayo tulidhani itatutoa kwenye umaskini.

Elimu rasimi
angalau imekwisha tujengea mazingira ya kujua kusoma na kuandika, kutafakari,
kuchambua baya na zuri n.k. kwahiyo kazi ya kuboresha fikra haiwezi
kushindikana kwakuwa tayari uwezo tunao. Kumbuka kuwa maisha ya mafanikio ni
mambo makuu matatu: FIKIRI—TENDA—PATA MATOKEO (PESA).
Kitu rahisi ambacho ufanywa na matajiri ni kwamba wao ile hatua ya “FIKIRI” ni tofauti na tofauti hii inakutwa kwenye fikra, na zaidi sauti zao za ndani.
Kitu rahisi ambacho ufanywa na matajiri ni kwamba wao ile hatua ya “FIKIRI” ni tofauti na tofauti hii inakutwa kwenye fikra, na zaidi sauti zao za ndani.
Watu ambao ni
matajiri wakubwa duniani wanashauri na wakati mwingine kutukataza tusipende
kusema maneno kama haya: Siwezi kumudu, siwezi kufanya hivyo; tunza sana
pesa yako; usipoteze pesa; ukishindwa na usipate kabisa itakuwaje…n.k.
Hapa wanakuwa
wanajaribu kutusaidia kuwa na “FIKIRI” tofauti. Watu wote
tunatenda sawa lakini kwasababu tunafanyia kazi “FIKIRI” ile
ile siku zote ndiyo maana tunapata matokeo yale yale ambayo hatuyapendi.
Mpendwa msomaji wa mtandao wa DIRA YA MAFANIKIO utakubaliana na mimi kuwa suala hapa siyo kufanya kazi (kutenda) bali ni kuboresha kwanza akiLi na mawazo, ili hatimaye uwe na FIKRA sahihi juu ya kile unachopanga kukifanya.

Njia mojawapo ni
kujaza kichwani mwako taarifa zilizochambuliwa kwa kina na siyo kutumia taarifa
za majukwaani, vijiweni, barabarani na sehemu nyinginezo hasi.
Kwa mafunzo ya
kuboresha fikra zako endelea kuwa karibu nasi kwa kutembelea mara kwa mara
mtandao huu:http://dirayamanikio.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.