Mar 14, 2017
Ongeza Maarifa Na Badili Maisha Yako,..Kupitia Hamasa Hizi Muhimu Kwako.
Kati ya nguzo mojawapo kubwa ya mafanikio ni
hamasa. Huwezi kufanikiwa bila kuwa na hamasa hata kama una rasilimali nyingi vipi
za kukusaidia kufanikiwa, itafika mahali utashindwa.
Kwa kuwa hamasa ni muhimu katika mafanikio yoyote
yale, hebu leo hii kupitia makala haya tujifunze pamoja baadhi ya hamasa ambazo
zitakusaidia kuweza kupiga hatua ya kimafanikio.
Hamasa ya 1.
Katika dunia ya sasa, taarifa nyingi za ni nini ufanye au kipi usifanye ili uweze
kufanikiwa, tayari zipo. Kazi kubwa uliyonayo, ni kutumia taarifa hizo ili
ziweze kukusaidia kufanikiwa.
Watu wengi wanashindwa kwenye maisha si kwa sababu
hawana taarifa sahihi za mafanikio, bali ni kwa sababu hata zile taarifa kidogo
walizonazo hawazitumii kuweza kuwasaidia kufanikiwa.
Acha kulalamika kila wakati kwamba eti huzioni
fursa, kama ni fursa, zipo nyingi na za kutosha. Tatizo kubwa ulilonalo ni kule
kwa wewe kushindwa kuchukua hatua ya kuzitumia fursa hizo kwa uhakika ili
zikupatie mafanikio.
Kuchukua hatua na kuweka juhudi hiyo peke yake
haitoshi ili kufikia mafanikio makubwa. Unatakiwa kuongeza kitu cha ziada
ambacho ni MTAZAMO SAHIHI. Hiki
ndicho kitu unachotakiwa kukiongeza wakati unachukua hatua na kuweka juhudi.
Unapokuwa na mtazamo sahihi, huku ukichukua hatua
na kuweka juhudi zote kwa kile unachokifanya, lazima utafanikiwa. Watu wote
wenye mafanikio wana mitazamo mingi sahihi inayowapa nguvu ya kufanya tena na
tena hadi kufanikiwa.
Hamasa ya 3.
Maisha ya mafanikio yanaundwa na vitu vidogo vidogo
sana. Zile hatua ndogo kabisa ambazo unaziona haziwezi kukusaidia kufanikiwa,
hizo ndizo zinaweza kukupa mafanikio kama utafanya kwa muda mrefu.
Hebu kama kuna kitu unataka kukifanya, anza
kukifanya bila kujiuliza uliza. Acha kabisa kuahirisha mambo yako, utakuja
kujuta sana baadae utakuwa umepoteza pesa nyingi na mafanikio kwa ujumla kwa
sababu ya kuahirisha.
Ipo gharama kubwa sana ya kusubiri subiri na
kuahirisha mambo kuliko unavyofikiri. Utapoteza mambo mengi sana ambayo moyo
wako utakuuma sana na kujiuliza kwa nini ulisubiri na hujufanya mapema. Fanya na
acha tena kusubiria kitu au kuahirisha.
Hamasa ya 4.
Tofauti kubwa kati ya watu wenye mafanikio na wasio
na mafanikio, haipo kwenye kurithi, kipaji au uwezo mkubwa sana. Tofauti kubwa
inajitokeza kwenye kufanya yale mambo ambayo yanaonekana ni rahisi.
Hili ndio kosa ambalo watu wenye mafanikio
hawafanyi. Yale mambo ambayo yanaonekana ni madogo na ya kudharaulika kabisa
wao wanayafanya bila shida yoyote na ndio yanayowapa mafanikio makubwa.
Hata ukiangalia watu wenye mafanikio na watu wasio
na mafanikio wanafanya mambo yale yale ambayo yanafanana kwa siku kwa mfano
kula, kusoma kitabu cha aina moja na kuhudhuria semina.
Tofauti inaanza kujitokeza hasa pale kwenye umakini
wa kutumia hasa mambo yale wanayojifunza karibu kila siku. Umakini hapa sasa,
ndio unawatenga waliofanikiwa na ambao hawajafanikiwa.
Hamasa ya 5.
Kuna vitu vitatu ambavyo unatakiwa uwe navyo ili
uweze kupata kile unachokihitaji katika maisha yako. Vitu hivi ni lengo
maalumu kwa kile unachokitaka, maarifa ya hicho unachokitaka na hamasa ya
kupata kitu hicho. Hayo ni
mambo ya lazima sana ili uweze kupata kitu unachokitaka kwene maisha yako.
Najua kuna kitu muhimu umejifunza hapa cha kuweza
kukusadia kubadili maisha yako. Endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspt.com
kujifunza kila siku.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI
NGWANGWALU,
0713 04 80 35,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.