Mar 2, 2017
Elimu Mahususi Katika Kukua Kwa Biashara Yako.
Tumekuwa
mashuhuda wazuri ambao tumekuwa tukishuhudia baadhi ya biashara nyingi zikifa
hii ni kutokana na wahusika hao wamekuwa wakifanya biashara hizo kimazoea.
Lakini
kumbuka acha mara moja kufanya biashara kimazoea kwani ukiendelea na tabia hiyo
mafanikio yatakuwa yanajitenga nawe kila wakati.
Hivyo
ili kuepuka kufanya biashara komazoea unahitaji aina hizi za elimu ambazo
zitakusaidia kukua kwa kibiashara yako.
a)
Elimu ya mawasiliano.
Hii
ni elimu muhimu sana ambayo ni lazima mfanyabiashara yeyote yule anatakiwa kuwa
nayo katika biashara yake. Aina hii ya
elimu huusisha dhima nzima ya jinsi ambavyo utawasilisha na wateja wako.
Zipo
biashara zimekuwa zikiendelea kufa kila kukicha hii ni kwa sababu wamiliki wa
biashara hizo wamekuwa hawana aina hii ya elimu ya mawasiliano.
Pata elimu sahihi ya biashara, ukuze biashara yako. |
Wengi
wao wamekuwa wamesahau ya kwamba mteja huwa anavutiwa hasa pale ambapo unamjali
hasa pale anapokuja katika biashara yako.
Ili uweze kukua kibiashara hakikisha ya kwamba unakuwa na mawasiliano
mazuri kwa mteja wako.
Mawasiliano
haya hutegemea hasa katika kauli zako. Kauli njema ni kuvutio kikubwa katika
biashara. Jifunze kuwa na lugha nzuri za
kibiashara kama unataka kufanikiwa katika biashara yako.
Lakini
vilevile kama hiyo haitoshi aina hii ya elimu ina ukaribu mbashara juu ya
mmiliki wa biashara fulani kuweza kushirikiana na wafanyabishara wengine ambao
wanaokuzunguka.
Kufanya
biashara bila kuwa na ukaribu na wafanyakazi wengine ni sawa na bure. Hivyo nakusihi tu ya kwamba jitahidi kuwa na
mawasiliano bora na wafanyabiashara wengine.
b)
Elimu ya teknolojia.
Kwa
kuwa sasa tupo ulimwengu wa utandawazi na vitu mbalimbali vimekuwa
vikitengenezwa kila kukicha hivyo hakikisha unaendana na kasi hiyo. Biashara yako ili ikuwe katika mstari wake, unatakiwa kuifanya katika hali ya kisasa
zaidi.
Tumia
vifaa mbalimbali vya kietroniki katika kujua mbinu za kuwa mbunifu kibiashara,
na pia kujua namna ya kuongeza wateja hatimaye kuongeza mauzo.
Kwa
mfano, unaweza kutumia simu yako kuwataarifu wateja wako kuhusu ujio wa bidhaa
mpya. Au unaweza kusoma mambo mbalimbali
ambayo yanapatikana katika mitandao mbalimbali itakayokufanya uongeze wateja. Pia
kumbuka maarifa hayana ukomo.
Itaendelea
wiki ijayo siku kama ya leo.......
Ndimi Afisa Mipango : Benson Chonya,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.