Mar 29, 2017
Hawa Ndio Wanawake Waliofanikiwa Sana Kwenye Ujasiriamali.
Siku zote tunasema na tutaendelea kusema kwamba mafanikio hayana rangi, kabila, umri
wala jinsia, ukiamua kufanikiwa kwa vyovyote vile ulivyo hata uwe katika kona
gani ya dunia utafanikiwa tu, kwa sababu umeamua iwe hivyo kwako na itakuwa.
Nasema hivyo kwa sababu, mara nyingi watu wengi linapokuja suala
la mafanikio huwa kuna bagua bagua nyingi sana kwa upande wao. Kwa mfano, mtu
anakwambia kabisa huwezi kufanikiwa kwa sababu wewe umri wako ni mdogo au
huwezi kufanikiwa sana kwa sababu wewe ni mwanamke.
Ukiangalia ukweli wa mambo ulivyo kwenye mafanikio hauko hivyo,
kwa vyovyote vile ulivyo unaweza ukafanikiwa na kutengeneza mafanikio makubwa
bila kujali unaishi nchi gani au bila kujali wewe ni mtu wa jinsia gani yaani
mwanaume au mwanamke.
Kutilia mkazo katika hilo na ili unielewe vizuri ninachosema
hapa, leo kupitia makala haya tuangalie baadhi ya wanawake ambao wamepata
mafanikio makubwa sana duniani kupitia ujasiriamali, ingawa kuna wakati pengine
walibezwa na kukejeliwa sana kwamba hawawezi kufika popote.
1. Oprah Winfrey
Pamoja na kwamba Oprah kwa sasa ameshaacha mambo ya utangazaji
kwenye televisheni lakini ni moja ya wanawake ambao wamefanikiwa sana na kuwa
na pesa nyingi kutokana na kujituma na kuwekeza kadri alivyoweza hadi kufikia
mafanikio aliyonayo sasa.
Yeye kama yeye kupitia kituo chake cha ‘Oprah Winfrey leadership
academy’amefanikiwa kuwasaidia watoto wengi wa kike, pia ni jambo
ambalo limekuwa llikimuungizia pesa za kutosha. Ameidhirihishia dunia kwamba
mafanikio hayana jinsia ni kujituma tu.
2. Folorunsho Alakija
Alakija ni moja
pia ya wanawake wenye pesa na tajiri sana nchini Nigeria. Biashara zake zilizompa
utajiri ni biashara ya mapambo na mafuta. Kwa sasa Alikija anakadiriwa
kufikia utajiri wa dola za kimarekani billion 1. 6.
Mpaka hapo unaona
ni kwa jinsi gani ambavyo naye amejitahidi kuweka juhudi nyingi za kufikia
mafanikio yake aliyonayo katika kile anachokifanya. Hiyo yote inaonyesha juhudi
ikiwekwa popote hakuna kinachoshindikana.
3. Wang Laichun
Laichun pia inasemekana
ni moja ya mabillionea wa kichina ambapo utajiri wake alionao ambao kwa sasa unafikia
dola za kimarekai bilini 1.67, umetokana na juhudi zake binafsi na sio kurithi.
Biashara
iliyompaisha hadi kufika huko aliko sasa ni biashara ya vifaa vya umeme ambavyo
anavisambaza na amekuwa mojawapo ya wanawake matajiri sana duniani.
4. Debbie Fields
Pia katika
wanawake wajasiriamali na wenye pesa huwezi kumsahau mwanadada huyu Debbie
fields katika ulimwengu wa mafanikio. Ni moja ya wanawake kweli waliofanikiwa
haswaa.
Utajiri wake hasa
ni wa nini? Huu ni mwandada anayejihusisha na kutengeneza vyakula vya aina tofauti
tofauti vyenye mfumo kama wa keki. Ambapo kwa sasa anasambaza vyakula vyake
zaidi ya nchi kumi duniani.
Mafanikio katika
maisha yako yanawezekana. Huna haja ya kuwa na sababu kwamba mimi sina hiki au
kile au mimi kwa sababu ni jinsia hii siwezi kufanikiwa, weka juhudi, matokeo
utayaona.
Endelea kujifunza
kupitia dirayamafanikio.blogspt.com kila siku.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI
NGWANGWALU,
0713 04 80 35,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.