Mar 1, 2017
Ukifahamu Vyema Mambo Haya, Utajiri Ni Wako.
Zipo sheria au mambo ambayo watu wengi wenye
mafanikio wanayafahamu na kuyatumia kama ngazi ya kuufikia utajiri wao.
Haijalishi mambo hayo au sheria hizo umezitumia kwa kukusudia au kwa bahati mbaya
ila ukizitumia tu unafanikiwa.
Leo kupitia makala haya nataka nikushirikishe mambo
muhimu ambayo ni muhimu sana kwako, lakini ambayo ukiyatumia yatakusaidia moja kwa
moja kuweza kufikia mafanikio makubwa hadi utajiri wako.
Twende pamoja kujifunza kupitia mambo
hayo;-.
1. Fanya
mambo yako kwa utofauti.
Hakuna uchawi katika mafanikio mkubwa kama huu,
kama unafanya vitu vyako kwa utofauti, ni lazima utapata mafanikio makubwa.
Watu wote wanaofanya mambo kwa utofauti wanafanikiwa bila pingamizi lolote.
Haijalishi una pesa au huna. Haijalishi una mtaji
au huna. Haijalishi una kipaji au huna, lakini wewe fanya mambo yako kwa utofauti
utapata mafanikio makubwa sana ambayo hata hukutegemea.
2. Waza
chanya wakati wote.
Kufikiri na kutenda kwa utofauti mara nyingi
kunatokana na jinsi unavyowaza. Je, unawaza nini kichwani mwako? Kichwa chako
kina kitu gani hiyo ndiyo itakayokufanya ufanikiwe.
Waza umefanikiwa hata kama ndani yako huoni kitu.
Waza unaona una afya tele hata wakati ambao unaona wazi kabisa bado hujapona.
Mawazo yako yana nguvu kubwa sana ya kukufanya ufanikiwe. Yatumie vizuri
yakusaidie kufanikiwa.
3. Jenga picha kamili ya kile unachokitaka.
Mafanikio makubwa sio
uchawi ni sayansi. Unataka kufanikiwa itumie sayansi hii kwa kujiwekea picha
sahihi ya kile unachokitaka kichwani mwako. Kijue vizuri kile unachokitaka bila
kubababisha hata kidogo.
Kijue kile unachokitaka
kama vile unavyojua gari lako, nyumba yako au sehemu yoyote ile unayoifahamu.
Kama kitu hicho unakijua kwa namna hiyo ni rahisi kuweza kukivuta na kuwa
upande wako.
4. Kuwa mtu shukrani.
Kwa watu wengi hiki
kinaweza kuonekana ni kitu cha kawaida kabisa lakini shukrani yoyote ina nguvu
kubwa sana na muunganiko na mafanikio yako. Unapokuwa ni mtu wa shukrani
unakuwa unavuta mafanikio mengine zaidi bila ya wewe kujielewa.
Kama unaishi maisha ya
kutokuwa na shukrani unakuwa unavunja uhusiano moja kwa moja na Mungu wa
mafanikio. Hebu jifunze kuwa na shukrani, hata biblia imeandika sana kuhusu
hili jambo la kuwa na shukrani.
5. Acha kuongelea umaskini kabisa.
Umaskini hauwezi kutoka
kwako eti kwa sababu unajifunza juu ya umaskini na sababu zake. Hauwezi kupata
kitu kwa kujifunza kinyume chake. Unataka kuwa tajiri jifunze juu ya utajiri na
yale yote wanayofanya matajiri na sio ujifunze umaskini.
Hivyo kwa vyovyote vile
acha kuwaza au kuongelea umaskini. Wewe na umaskini sio watu marafiki. Jifunze
juu ya utajiri na mambo yanayopelekea hadi mtu mwingine akawa tajiri kwenye
maisha.
6. Chukua hatua mara moja.
Weka akili na mawazo yako
yote kwenye kuchukua hatua moja kwa moja. Acha biashara ya kuahirisha na kusema
nitafanya hiki kesho au kesho kutwa hebu fanya sasa hilo unalotaka kulifanya
leo.
Kama kuna sehemu ulikuwa
umekosea jana hiyo ilikuwa ni jana. Lakini lilokubwa kwako ni kuchukua hatua
mara moja za utendaji bila kuangalia mazingira uliyopo. Kama unasubiri
mazingira yakae sawa, yatakaa sawa wakati huku ukiendelea kutenda.
Hakuna atakayeshindwa
kufikia mafanikio ikiwa unatumia mambo hayo vizuri ya mafanikio kwa ufasaha. CHUKUA
HATUA.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI
NGWANGWALU,
0713
04 80 35,
dirayamafanikio.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.