Mar 20, 2017
Tumia Mbinu Hizi Kubuni Jina La Biashara Yako.
Roho kubwa katika biashara ni jina la biashara yako. Watu wengi wamekuwa wakikurupuka katika kuanza kufanya biashara ila wamekuwa wakisahau ya kwamba kitu ambacho kinaibeba biashara kwa asilimia kubwa ni jina la biashara.Wengi wao wamekuwa wakishirikiana jina la biashara kama ni sehemu ya kawaida sana. Lakini ninachotaka kukwambia haijalishi ni biashara ya aina gani ambayo unafanya hakikisha ya kwamba jina la biashara linachukua kipaumbele.
Hivyo ili kuonyesha ya kwamba unaipenda biashara yako hakikisha inaendana nami siku ya leo kwani nitakueleza kiundani kuhusu mbinu itakapotimia katika kubuni jina la biashara yako.
Bila kupoteza wakati zifuatazo ndizo mbinu za kupata jina la biashara yako.
1.Jina ni lazima liwe fupi.
Imeshauriwa ya kwamba katika kubuni jina la biashara ni lazima uhakikishe unapata jina ambalo ni fupi. Kwani kuwa na jina refu katika biashara yako huwafanya wateja wako waweze kulishau kwa urahisi.
Pia ni vyema jina hilo ambalo utalitumia liwe ni rahisi kutamkika. Na kwa kuongezea tu ni kwamba katika kubuni jina la biashara yako ni vyema ukahakikisha jina unalolitumia lisizidi maneno matano. Kwa mfano kuna mama mmoja yeye huwa anauza mkaa hivyo banda lake ameamua kuliita " mkaa plaza" hivyo hata wewe jaribu kuchagua jina ambalo ni fupi pia ni rahisi kutamkika.
2. Hakikisha ni jina linalo akisi kile unachokifanya.
Katika kitu ambacho unatakiwa kuweza kukifahamu kila wakati ni kuhakikisha unachagua jina ambalo linaendena na kile ambacho unakifanya. Kama unauza nguo basi hata jina liwe katika maahadhi ya biashara hiyo, hata pale mtu anapolisikia iwe rahisi kujua ni biashara gani ya biashara ambayo unaifanya.
Jina linalogusa hisia za watu
Moja kati ya njia bora ya kupata wateja katika biashara yako, ni kuipa biashara hiyo jina ambalo litagusa hisia za wateja wako. Kufanya hivyo kunamfanya mteja wako ajihisi ni sehemu ya biashara yako. Kwa mfano hivi hajawahi kuona mteja fulani akikosa kinywaji fulani ambacho amezoea kunywa hughairisha kabisa? Bila shaka umewahi kuona aina hii ya mteja. Hapa ndipo ninapozungumzia ya kwamba mfanye mteja kuwa sehemu ya biashara yako kwa kutoa huduma bora na kwa wakati sahihi ili kugusa hisia zake.
Jina la kipekee
Hupaswi kunakiri majina ya biashara nyingine.Chagua jina la kipekee ambalo litakutambulisha wewe na biashara yako.Kuipa biashara yako jina la biashara nyingine inaweza kuleta athari kwa biashara yako kwani unaweza kuwa unaitangaza biashara ya mtu mwingine bila kujifahamu hususani kama biashara ya mtu huyo imekuwa kubwa kuliko yako. Kwani hata huyu mwenye biashara yake Atasema wewe ni tawi lake. Hivyo epuka mfanano wa majina.
Lakini nimalize kwa Kusema ya kwamba biashara bora huenda sambamba upatikanaji wa huduma bora na kwa wakati sahihi na uwepo jina lililo thabiti la kibiashara.
Ndimi afisa Mipango Benson Chonya
bensonchonya23@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.