Mar 23, 2017
Hatua Nne Za Kufikia Malengo Yako Kwa Uhakika Mkubwa.
Kila
mtu katika maisha yake ana malengo maalumu ambayo anakuwa amejiwekea na anakuwa
ana waza kwamba kwa namna yoyote ni lazima baada ya muda fulani malengo yake
yatatimia.
Pia
sina shaka na wewe, naamini umejifunza kwa sehemu namna au mbinu ambazo mtu
anaweza akazitumia kuweza kufikia malengo yake. Lakini leo hii, si vibaya kama
nitakung’ata sikio kukumbushia tena jinsi unavyoweza kufikia malengo yako kwa
uhakika mkubwa.
Najua
kila mtu ana njia zake na mbinu ambazo anazitumia kuweza kufikia malengo yoyote
katika maisha. Leo hii, naomba nikuonyeshe mbinu ambazo zinatumiwa karibu na
watu wote wenye mafanikio makubwa kufikia malengo yao kila wakati.
Andika malengo yako chini.
Yaweke
malengo yako kwenye karatasii ili yawe rahisi kuyaona. Yawe ni malengo mahsusi
ambayo utekelezaji wake unafikika na uwe tayari umejiwekea tarehe maalumu ya kuyafikia.
Hio ndiyo sifa ya malengo unayotakiwa kuwa nayo.
Anza kuweka mipango.
Umesha
andika malengo yako tayari. Hatua inayofuata ni kwa wewe sasa, kuweka mipango
ya kufanya. Kumbuka unapofanya jambo unapata nguvu zaidi ya kuweza
kulifanikisha kuliko ukitulia. Hivyo ni lazima mipango yako iwe hai na ya kiutekelezaji.
Lipa gharama.
Kubali
kulipia kila gharama inayohitajika ili kufikia malengo yako. Gharama hizo
zinaweza zikawa ni muda au nidhamu binafsi. Lakini gharama yoyote fanya kila
ufanyalo hakikisha unailipa. Kama utakwepa kulipa gharama yoyote ile naomba
nikwambie sahau mafanikio.
Yapitie malengo yako kila siku.
Hakuna
namna ya nyingine ya kuwa mshindi zaidi ya wewe kukomaa kupitia malengo yako
kila siku. Unapopitia malengo yako kila siku yanakupa nguvu na hamasa kubwa ya
kuona ni jinsi gani yanawezekana na unaweza kuyafikia.
Hivyo
ndivyo, unaweza kutimiza malengo kwa kufuata hizo hatua rahisi kabisa.
Nikutakie
siku njema na kila kheri,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
IMANI
NGWANGWALU,
0713 04 80 35,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.