Mar 9, 2017
Umuhimu Wa Kutumia Mbegu Na Zana Bora Kwa Mkulima.
Ili kufanikiwa katika
kilimo, kuna umuhimu mkubwa kwa mkulima kutumia mbegu na zana bora za kilimo
ili kuleta tija kwa mkulima yeyote anayetaka kupata mafanikio hayo makubwa.
Kwa mfano mkulima
inatakiwa kujiuliza kwa nini mbegu ya kawaida ya nyanya kama Mwanga,Tanya mbegu
hizo zote kiasi cha 100g ambayo ndiyo ya kutosha ekari moja unaweza ukaipata
kwa shilingi za kitanzania elfu 16-20 Lakini mbegu kama Faida F1 ambayo 60g inatosha
ekari moja unaweza kupata kwa 150,000/=?
Utofauti wa hizo mbegu ni
ustihimilivu katika magonjwa, kustahimili hali ya hewa, utofauti mkubwa wa
mapato au mavuno shambani,yaani Faida F1 mavuno yake ni mara tatu zaidi ya
mavuno ya mbegu ya kawaida, na unavuna kwa muda mrefu miezi 5-7 endapo
utaendelea na matunzo.
Pia unakuta mkulima
anayetaka mafanikio anaenda dukani anaulizia au anataka bomba/pampu/sprayer ya
bei ndogo kabisa elfu 30-45 lakini akitumia kupulizia dawa hata ekari moja tuu
utakuta anarudi dukani kutafuta spares, na wakati angeweza kupata sprayer yenye
ubora kwa laki moja na bila kununua spares mara kwa mara.
Hivyo ili mkulima yeyote
anayetaka mafanikio inatakiwa atumie mbegu na pembejeo za kilimo zilizo bora
zaidi ili kufikia mafanikio makubwa zaidi. Kunielewa vizuri katika hili, leo
ngoja nikuelezee kidogo kuhusu kilimo cha tikiti na uone umuhimu wa kutumia
mbegu na zana bora za kisasa.
Katika
kukuelezea kuhusu kilimo bora cha matikiti, naomba tutatumia
mfano wa mbegu bora PATO F1.
MAHITAJI
Shamba ekari moja (4000 mita
za mraba) liwe lako au la kukodi.
Ukipata shamba la tifutifu
lililo changanyikana na mchanga itakuwa vema zaidi.
Angalizo: Usilime matikiti
kwenye udongo unaotuamisha maji yaani mfinyanzi kwani kama unavyoona udongo
unavyo pasuka hivyo hata matikiti yakifikia hatu ya kukomaa yatapasuka pia.
Kiasi
cha mbegu 250g yenye mbegu 5000 inatosha kupanda ekari moja.
HATUA ZA ULIMAJI.
Andaa
shamba
kwa kulima iwe kwa mkono au trekta lakini utifue kwenda chini angalau sentimita
15 kwenda chini.
Baada
ya kulima liache shamba lipumzike baada ya hapo tumia kiua gugu non selective (Grypro
ambayo itaangamiza nyasi zote ambazo zilikuwa zinaota, baada ya
kupiga dawa liache kwa muda wa wiki moja hadi mbili ndiyo uende kupanda.
Kabla
ya kuanza kupanda hakikisha unaanda mbolea ya kupandia yenye virutubisho vingi
vya Phosphorus (P) kwa mfano DAP, Agrigrow starter NPK 14:28:18 kwa ajiri ya
kupandia.
Panda
mbegu
kwa kuzingatia nafasi zifuatazo,mstari hadi mstari mita 2 na mche hadi mche
sentimita 45.
Kwa
siku 0-15 days (Planting) inatakiwa uwe na dawa ya wadudu Avirmec 1.8EC ambayo
utatumia mls 7 kwa lita 20,na mbolea ya majani Agrigrow starter ,kwa sababu matikiti
hupendwa sana na wadudu hiyo mbolea ya majani yenye virutubisho vingi vya
Phosphorus ili kuufanya mmea uwe na mizizi imara na kuwezesha mmea kufyonza
virutubisho vizuri kutoka kwenye udongo.
Siku
16-25(Vegetative /Trailing) tumia mbolea ya majani Agrigrow
vegetative NPK 30:10:10. Hii mbolea itafanya miche ikue haraka haraka na
kufanya uwe na matawi mengi au unaweza tumia Allwin top, na uwe na dawa ya
wadudu Prosper 720EC (Profenofos 600g/L +Cypermethrin 120g/L),na mbolea za
chini zenye virutubisho vya Nitrogen kwa wingi,dawa ya ukungu Agrilax 72WP.
Siku
25-40days(Flowering) hii ni hatua muhimu sana kwa mmea ambayo hata upigaji wa
dawa hautakiwi upige wadudu wa muhimu wakiwa shambani,kwa mfano ukamkatisha
nyuki akiwa anafanya kazi yake tunda litalotokea linakuwa halina umbo
zuri(irregular shape)
Kwa
kipindi hicho unatakiwa uwe na dawa za ya ukungu Agrilax 72WP,dawa ya wadudu
Prosper 720EC na hakikisha unapiga dawa asubuhi sana au jioni sana,mbolea ya
majani unaweza utumie Agrigrow flowering and fruiting ambayo
itazuia kupukutika kwa maua,
Uwe
na mbolea ya chini ambayo ina virutubisho vya Potassium kwa wingi
Siku
40-60-90days(fruiting) Uwe na dawa ya wadudu Avirmec 1.8EC (Abamectin),dawa ya
ukungu Agrilax,mbolea ya majani Agrigrow flowering and fruiting au Allwin top
ambayo itaboresha tunda na ubora wake.
Pia
wakati huo uwe na mbolea ya chini yenye virutibisho vingi vya Potassium.
MAVUNO.
Baada ya hapo tuangalie
idadi ya miche abayo utatarajia kuwa nayo na idadi ya matunda ambayo utatakiwa
uyavune kwa ekari moja.
Idadi ya miche inapatikana
kwa formula/Kanuni maalumu ambayo ni;-
Plant population (PP)
=Area(1acre,4000m square) divided by Spacing times number of seeds per hole
Au
Miche =Eneo(ekari moja)
÷nafasi ya upandaji zidisha na mbegu utazokuwa unaweka kwa kila shimo.
Area/Eneo ni 1acre/ekari
moja ambayo ina ukubwa wa 4000mita za mraba.
Nafasi kati ya mstari hadi
mstari ni mita 2(2m) ,mche hadi mche ni sentimita 45(45cm) or 0.45m,na inatakiwa
upande mbegu moja moja tu.
Kwa hiyo
PP=Area/Spacing ×number of seeds per hole
PP=((4000/(2×0.45))×1
PP=4,444plants/acre
PP=4,444plants.
Kwa hiyo kutakuwa na miche
4,444 kwa ekari moja.
Na kwa kawaida tikiti la
hybrid (PATO F1) huzaa matunda kuanzia 5-7 na muda mwingine yanaweza kufikia
hata 10 ,ila tunamshauri mkulima apunguze matunda na kuyaacha matunda matatu
tuu kwa kila mche.
Tunamshauri mkulima
kupunguza matunda ili kupata matunda matatu tu, kwa mche mmoja ambayo yatakuwa
na ubora,na kuyauza kwa bei nzuri.
Kwa hyo basi kama mche
mmoja utakuwa na matunda matatu yaliyo bora.
Je
utakuwa na matunda mangapi kwa ekari,hebu tuangalie hesabu hii chini;-
1plant= 3ftuits
4,444plants= x?
Therefore=4,444×3
=13,332fruits/acre
Kwa hyo utagundua kuwa
unatakiwa uwe na matunda 13,332 kwa ekari moja.
Kama sehemu uliyopo
wananunua tikiti hata kwa bei ya chini sh 500,utakuwa na jumla ya pesa
500×13,332=sh 6,666,000/=
Kama wananua kwa sh 1000
basi utakuwa na sh 1000×13,332=sh 13,332,000/=
Kama wananua kwa sh 1500
utakuwa na jumla ya pesa 1500×13,332=sh 19,998,000/=
Kama utaweza kupata soko
zuri zaidi kwa bei ya sh 2000 basi utakuwa na jumla ya sh
2000×13,332=26,664,000/=
Na kwa wale wanaouza kwa
kilo kwa mfano bhakresa hununua tikiti kwa kilo,hili tikiti la PATO F 1 baada
ya kulivuna linakuwa na lilo 8-15.
Makala
hii imeandikwa na Boniface L Pwele mtaalamu wa kilimo. Kwa ushauri wa kilimo
cha kisasa, ununuzi na utambuzi wa mbegu bora, wasiliana nae kwa blugahno95@gmail.com au mpigie kwa+255 762 56 76 28.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.