Mar 16, 2017
Biashara Nzuri Ambayo Unaweza Ukaifanya Na Kupata Faida Kubwa Ni Hii Hapa.
Habari za leo, mpenzi msomaji wa safu hii ya
biashara? Nikukaribishe kwa moyo mkunjufu ili tuweze kujifunza na elimu
hii ya biashara. Andaa ubogo wako ili uweze kupokea mambo muhimu ya kukusaidi kufanikiwa.
Moja ya maswali ambayo nimekuwa
nikiulizwa sana na wasomaji wetu ni kwamba je, afisa mipango Ben, nifanye
biashara gani ambayo itakuwa ina faida kubwa kwangu?
Kama ambavyo nimekuwa nikiulizwa mara
kadha wa kadha na swali hilo tena limekuwa likijirudia. Hivyo kwa kutumia
dakika chache naomba niweze kujibu swali hilo.
Jambo la msingi sana ambalo unatakiwa kulizingatia ni
kwamba kila biashara ambayo unaiona machoni mwako ina faida na hasara
zake, Nimeanza kwa kusema hivyo kwani watu wengi wamekuwa wakiaangalia
upande mmoja tu wa kupata faida tu.
Lakini ukweli ambao unatakiwa kuujua
mapema ni kwamba kabla ya kuingia katika biashara tambua ya kwamba katika
biashara hiyo kuna faida na hasara, hivyo uwe tayari kubeba mambo hayo mawili
pindi yatakapojitokeza.
Biashara yenye faida huanza na wazo, wazo ambalo
limekuwa likitokana na mfanyabiashara kabla ya kuanza kufanya biashara husika.
Wazo hilo hujengwa na misingi ya kina ya kufanya uchunguzi yakinifu juu ya
biashara hiyo.
Usipofanya uchunguzi wa kutosha juu ya biashara unayotaka
kuifanya ipo siku utalalamika. Ila tunashauriwa ya kwamba katika kufanya
uchunguzi wa kutosha ni lazima ujikite katika kuangalia eneo ambalo utaiendesha
biashara hiyo.
Wakati unangalia eneo kwa ajili ya kufanyia biashara,
angalia eneo ambalo:-
Eneo linalofikika kwa urahisi.
Angalia eneo ambalo lina uwingi wa mkusanyiko mwingi wa
watu tofauti tofauti.
Tafuta eneo ambalo kuna upatikaji wa huduma za kijamii,
kama vile ukaribu wa benki, umeme, maji na mengineyo mengi yatakoyokusiadia
kukua kibiashara.
Angalia eneo ambalo lipo karibu na wafanyabiashara
wengine. Kwa mfano, kama unafanya biashara ya mashati basi chagua eneo
ambalo kuna mfanyabiashara anauza tai. Kufanya hivi kuna msaidia mteja kutopata
tabu ya kuhangaika kupata bidhaa fulani.
Lakini kubwa kuliko yote ni kwamba katika kufanya
uchunguzi wa eneo la kufanyia biashara ni vyema unafanya uchunguzi kwa
kuangalia hasa ni yapi mahitaji ya watu. Kisha wewe uweze kuyasogeza
mahitaji hayo karibu.
Mwisho naomba ujiulize hivi, ni wapi ambapo imepanga kufanya biashara
h? Na watu wana changamoto zipi nawe umekuja suluhisho lipi? Ukipata majibu hayo huo ndio utakuwa
mwanzo wa kujua biashara gani italipa eneo hilo na hatimaye kupata faida.
Hivyo niseme hivi, biashara inayolipa
na kutoa faida kubwa ni ile biashara ambayo umeshaifanyia uchunguzi wa kutosha
na kujua soko lake liko wapi na lina ukubwa gani. Hiyo ndiyo biashara
inayolipa.
Endelea kujifunza maisha, mafanikio
na biashara kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku, usikose kumshirikisha
na mwingine ili aweze kupata maarifa haya muhimu.
Afisa mipango Benson Chonya,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.