Mar 15, 2017
Mambo Sita (6) Ya Lazima Kuyajua Ili Kufikia Mafanikio, Kama Umeanza Na Kidogo Ulichonacho.
Yapo
mambo ya lazima kuyajua na kuyafatilia kwa ukaribu sana kama unaanza na kidogo
ulichonacho ili kuweza kufikia mafanikio. Bila kuzingatia mambo hayo uwezekano
wa kufanikiwa utakuwa ni mgumu.
Kwa
yeyote anayezingatia mambo haya haijalishi unaanza na kidogo kiasi gani, mafanikio
yataanza kuonekana mara moja kama utachukua hatua. Mambo haya yanazingatiwa
sana na kila anayeanza na kidogo hadi kufanikiwa.
Yafuatayo
Ni Mambo Sita (6) Ya Lazima Kuyajua Ili Kufikia Mafanikio, Kama Unaanza Na
Kidogo Ulichonacho.
1. Kuwa kwenye mwendo.
Siri
kubwa ya kuanza na kidogo ulichonacho hadi kufanikiwa ipo kwenye kukaa kwenye
mwendo au ‘momentum’. Namaanisha nini
ninaposema kukaa kwenye mwendo, yaani kuendelea kuchukua hatua kwa jambo ulilolichagua
hata kama ni kwa kidogo sana.
Ni
bora ukawa unafanya kitu kidogo kidogo, lakini mwisho wa siku utajikuta
unasogea kuliko kutulia. Ni bora kuanza biashara hata ndogo kuliko kusubiri ile
biashara iliyo kubwa ambayo hunayo. Anza na kidogo ulichonacho ili kikusaidie
kuweza kukaa kwenye mwendo.
Anza na kidogo, hadi ufikie mafanikio makubwa. |
Kaa
kwenye mwendo. Hata kanuni za kisayansi zinatuambia kila kitu kilichoko kwenye
mwendo kitazidi au kitaendelea kuwa kwenye mwendo, pengine itokee nguvu nje ya
kuzuia. Sasa kwa nini usichukue hatua na kuamua kukaa kwenye mwendo kuliko
kusubiri subiri.
Ili
kufanikiwa kukaa kwenye mwendo, chagua kitu unachokitaka, kisha kitu hicho
kifanye kila siku. Hiyo itakuwa ni njia nzuri sana ya kuweza kukuweka kwenye
mwendo wa mafanikio yako. ukifanya kitu hicho kila siku utake, usitake ni
lazima utasogea.
2. Maliza kila kitu unachokianza.
Ili
uweze kuwa kwenye mwendo vizuri wa kufikia mafanikio yako, jifunze kumaliza
kile ambacho unaanza nacho. Kama kila kitu ambacho unakianza hukimalizi, tambua
unatengeneza nguvu kubwa ya kukufanya ushindwe kwa baadae.
Kwa
vyovyote vile, kila siku jitahidi kumaliza kitu ambacho umejiwekea kufanya. Najua
sio rahisi kuweza kumaliza kila kitu ambacho unakianza, kwa sababu vipo
vinavyokwama pia bila kutarajia, lakini hiyo isiwe sababu, maliza kile
unachokianza.
Kama
kuna jambo umelianza, hata kwa macho ya kawaida kama linaonekana ni mlima
lianze jambo hilo na kuhakikisha unalimaliza. Weka jitihada zitakazokuwezesha
kulimaliza. Mafanikio yanajengwa na wewe jinsi unavyomaliza vitu na sio
kuachilia kati.
3. Jenga tabia za kukusaidia
kufanikiwa kila siku.
Kinachowangusha
wengi kwenye safari ya mafanikio ni tabia zao. Tunapozungumzia tabia ni yale
,mambo ambayo kuna wakati tunayafanya hata bila kufikiria, unafanya tu kwa
sababu ya mazoea ya kila siku. Hebu angalia ni mazoea gani yanakuzuia
kufanikiwa.
Kwa
mfano kuamka asubuhi na mapema ni tabia na pia kuchelewa kuamka ni tabia. Kulalamika
ni tabia na hata pia kuwajibika ni tabia. Hiyo haitoshi kutumia pesa hovyo ni
tabia na kuweka akiba nayo ni tabia. Ukichunguza zipo tabia nyingi ambazo
tunazo.
Unaona
mpaka hapo zipo tabia zinazokuangusha na zingine zinakusaidia kufikia mafanikio
yako. Hivyo hapa unatakiwa ujue kabisa kwamba kumbe tabia ni lazima kuzijua ili
kubadilisha maisha yako na kuwa ya mafanikio. Unapojenga tabia chanya zaidi
unajitengenezea mazingira ya kufanikiwa.
4. Tafakari maisha yako.
Badala
ya kuwa ‘busy’ muda wote katika kutwa
nzima, kuna wakati unatakiwa utenge muda wako kwa ajili ya kutafakari siku yako
imekwenda vipi. Ni muhimu kujua ni kitu gani umekifanya. Hapa ni lazima uwe na
siku inayokupa faida kila siku.
Ni
rahisi kujikuta kutwa nzima ukiwa uko ‘busy’
sana na shughuli hii mara ile nakushindwa kutambua kama kweli unaenda mbele au
unarudi nyuma. Lakini kama utajenga tabia ya kutafakari nini ulichokifanya
kutwa nzima na kimekusaidiaje itakusaidia kuelewa ni kipi uboreshe.
Unapotafakari
juu ya maisha yako itakusaidia kuweza kujua ni maeneo yapi ambayo unatakiwa
kuyaboresha zaidi na zaidi na mwisho wa siku utajikuta unazidi kuchanja mbuga
kuelekea kwenye mafanikio yako. Anza mara moja kutafakari juu ya maisha yako
bila kuchelewa.
5. Tengeneza utamaduni wa kufurahia
mafanikio yako.
Hatua
ndogo ndogo unazozipiga kila siku inabidi uziweke wazi kwa kuziona na kisha
baada ya hapo anza kusherekea hayo mafanikio ako. Jenga utamaduni wa kuweza
kusherekea mafanikio yako. haina maana umefanikiwa halafu unashindwa
kujipongeza hata wewe mwenyewe.
Unapokuwa
unafurahia na kusherekea mafanikio yako inakusaidia kukupa nguvu na hamasa tena
na tena ya kuweza kusonga mbele na kufanikiwa kwa hicho unachokifanya. Watu wenye mafanikio wanafurahia mafanikio
yao hata kama ni kidogo.
Tunakutakia siku njema na kila la kheri, endelea
kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza
na kuhamasika.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI
NGWANGWALU,
0713 04 80
35,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.