Mar 13, 2017
Jenga Tabia Ya Kujiuliza Maswali Uishi Maisha Unayotaka.
Ili kubadilisha maisha yako na kuwa bora, unahitaji
kujenga tabia ya kujiuliza maswali yatakayokusaidia kubadili maisha yako. Kila
wakati jiulize ni njia au kwa namna gani ambavyo utaweza kuboresha maisha yako
na kuwa ya mafanikio.
Acha kujiuliza kwa nini ‘mimi sina hiki au kile,’ badala yake jiulize nitawezeje kupata kile
ninachokihitaji. Ukiwa unajiuliza hivi kila siku unapata msukumo wa kukusaidia
kupata kile unachokihitaji maishani mwako.
Jiulize kila wakati, je, usipobadilisha hali ya
maisha yako sasa na ikaendelea hivyo, maisha yako yatakawaje baada ya miaka
mitano au kumi. Na pia jiulize maisha yako kifamilia, kiuchumi na kimahusianao
yatakuwaje baada ya miaka mitano.
Njia rahisi ya uhakika na yenye nguvu kubwa ya
kubadilisha maisha yako ni kujiuliza maswali. Unaweza ukawa upo kwenye hali
ngumu sana ya kimaisha lakini kama unajiuliza maswali ya nitatoka vipi hapa
nilipo, ni lazima utafanikiwa.
Kwa kawaida unapojiuliza maswali juu ya jinsi ya
kubadilisha maisha yako na kuyafanya bora, vipo vitu viwili ambavyo
vitakutokea;-
1. Utabadili mtazamo wako na kile kitu unachokitaka.
Kwa mfano, kama unajiuliza kila wakati, nitafanyaje
ili nifanikiwe katika jambo hili? Hapo ni lazima mawazo yote na akili zote
zitakuwa kwenye kutafuta njia itakayokusaidia kupata jibu hilo.
Hoji na ujiulize kila kitu kwenye maisha yako. |
2. Itakuwa rahisi kwako kupata rasilimali za
kukusaidia kufanikiwa.
Kwa jinsi unavyoendelea kujiuliza jinsi ya
kuboresha maisha yako, utashangaa ukipata watu wa kukusaidia kutimiza ndoto
zako. Watu wengi wanashindwa kujiuliza maswali kwa sababu ya kuona haiwezekani
tena.
Kujiuliza maswali ni utaratibu mzuri sana ambao
utakufanya ufikiri tofauti na kubadili maisha yako kwa sehemu kubwa.
Unapoinza
siku yako kila siku anza kujiuliza maswali kama hivi;-
a) Kitu gani
ambacho nimejitoa kukifanya kwa moyo wote katika maisha yangu yote, bila kujali
nalipwa au si lipwi na mtu. Sababu ipi inayonifanya nikifanye kitu hicho?
b) Kitu gani
ninachojivunia katika maisha yangu mpaka sasa? Kama kipo vizuri, kama hakipo
nachukua hatua gani na mimi kuwa na vitu vichache vya kujivunia?
c) Kitu gani
ninachokifurahia sana, katika maisha yangu? Kwa nini nakifurahia kitu hicho?
Unapoimaliza
siku yako yaani jioni, jiulize pia hivi:-
a)
Kitu gani
ambacho nimekitoa katika siku ya leo, ambacho kimekuwa msaada kwa wengine. Kipi
nilichokitoa ili kuboresha maisha ya wengine?
b)
Kitu gani
ambacho nilichojifunza leo na kinamsaada mkubwa sana kwa maisha yangu yote?
c)
Na kwa jinsi
gani siku ya leo imeongeza thamani ya maisha yangu? Je, imekuwa ni siku ya
faida kubwa kwako na kubadili kwa sehemu, maisha yako?
Endelea kujiuliza maswali mengi tena na tena kwa
kadri unavyoweza tena na tena, utashangaa maisha yakibadilika. Mafanikio sio
ajali, ni kujifunza mbinu mbalimbali za mafanikio kama hivi.
Tunakutakia kila la kheri katika kufikia mafanikio
makubwa,
Endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA NAWE MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI
NGWANGWALU,
0713 04 80 35,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.