May 31, 2017
Zijue Faida Za Kumheshimu Kila Mtu Katika Kazi Yeyote Uitendayo.
Hapo
zamani za kale kulikuwako na mfalme mmoja ambaye alijulikana kwa jina la
mhavila. Mfalme huyu alikuwa na utu sana kwa watu wake. Japo kutokana na
majukumu yake ya hapa na pale ilikuwa ni ngumu sana kwake kuonana na watu
wake mara kwa mara.
Kila
mwakijiji wa jamii ile alitamani sana kukutana uso kwa uso na mfalme mhavila,
kwa kukuwa mfalme huyu alikuwa ni mtu mcheshi sana kwa watu wake. Siku moja
mfalme mhavila aliandaa mkutano mkubwa sana ambapo kila raia wa eneo lile
alihudhuria katika mkutano ule.
Watoto
kwa wakubwa, vijana kwa wazee wote walimiminika katika mkutano ule. Mfalme
mhavila aliwaeleza watu wake mambo mbalimbali ambayo kimsingi yalikuwa yana
manufaa sana katika kufanikisha masuala ya
maendeleo ya jamii na maendeleo ya watu hao kwa ujumla.
Mara
baada ya mkutano kuisha mfalme mhavila alikutana na mtu mmoja ambaye alikuwa ni
mjane, mjane huyo alionekana kwa macho ni maskini wa kutupwa, tunaweza kusema
hivyo hii ni kutokana na muonekano wake. Mjane yule alimtazama mfalme mhavila
kwa macho yenye kutia unyonge sana, baada ya dakika chache ndipo mjane yule
akafungua kinywa chache na kusema;
‘’samahani
mfalme mhavila kwa muda mrefu nimekuwa nikitafuta nafasi ya kuzungumza na wewe
ila kwa bahati mbaya nafsi hiyo sikuweza kuipata, ila kwa siku ya leo nina kila
sababu ya kumshukuru Mungu wangu kwa sababu tumeweza kukutana.
Kabla
ya mfalme hajainua kinywa chache mjane akandelea kusema ‘ nafahamu ya kwamba
upo bize na shughuli za hapa na pale, na unafanya hii yote kwa sababu ya
kusongesha kurudumu hili la maendeleo, kwa kufanya hivyo nikupongeze sana kwa
sababu kila mwenye macho na maskio anakiona na kukishuhudia kwa kile ambacho
anakifanya.
Mfalme
mhavila baada ya kusikia vile moyo wake ulikwenda kasi kidogo, hii yote ilikuwa
ni mshangao wa kile ambacho mjane alichokuwa amemueleza, mfalme mhavila aliwaza
kidogo, kisha akatafakari ndani ya nafsi yake. kisha mfalme mhavila akajibu
asante sana mama kwa kutambua mchango wangu kwa kile nikifacho, kwa kweli
nakushukuru sana.
Wakati
watu wengine wakishangaa na kujihoji mama mjane na mfalme walikuwa wanazungunza
nini, hakuna aliyepata majibu.
Hivyo
mara ya sekunde chache mama mjane akamwambia mfalme mhavila ‘’ samahani mfalme
mhavila nafahahamu ya kwamba una majukumu mengi sana, ila naomba jioni ya leo
uje tule kwa pamoja chakula cha jioni
nyumbani kwangu.
Mara
baada ya mama mjane kuzungumza hayo, mfalme mhavila akainua kinywa chake na
kusema “ nashukuru sana mama kwa maneno yako yenye kunitia nguvu za kiutendaji
wa kimaendeleo, kwani ulichokisema kimenipa fikra mpya za kuleta mbadiliko
mapya ya kimaendeleo, hivyo nakuahidi siku ya leo tutajumuika kwa pamoja katika
kupata hicho chakula cha jioni kwa pamoja.
Baada
ya mazungumzo hayo mfalme mhavila na mama mjane waliagana na kuahidiana kukutana
hiyo jioni kama ilivyopangwa. Mama mjane
alielekea nyumbani kwake kwa ajili ya kuandaa chakula hicho. Baada ya
dakika chache chakula hicho kilikuwa kipo tayari, hivyo mama mjane akaweka chakula
hicho mezani kwa ajili ya kuliwa. Mama mjane alimsubiri mfalme kwa muda wa saa
nzima, lakini cha ajabu ni kwamba mfalme mhavila hakufika .
Mama
mjane hakuchoka kumsubiri mfalme mhavila kwani alimini atakuja kama ambavyo
walivyokuwa wapenga, muda ilizidi kwenda laikini mfalme hakuonekana kufika.
Hivyo mama mjane akaamua kufunga mlango wake
kwa kuwa muda ulikuwa umeshakwenda.
Ilipita
nusu saaa tangu mama mjane afunge mlango wake lakini cha ajabu mfalme mhavila
hakutokea, wakati mama mjane anatafakari ni nini ambacho kitakuwa kimemsibu
mfalme mhavila ghafla akasikia mlango ukigongwa. Mama mjane aliinuka mahali alipokuwa
ameketi na kuelekea mlangoni kwa ajili ya kufungua.
Kabla
mama mjane haujaufungua mlango , mama mjane alifurahi sana kwani aliaamini
aliyekuwa amegonga mlango alikwa ni mfalme mhavila. Taratibu mama mjane
akashika kitasa cha mlango wake kwa ajili ya kuufungua mlango. Mara baada ya
kufungua alistajabu kumbe aliyekuuwa akigongo mlango hakuwa mfalme mhavila bali
alikuwa ni kijana ambaye alikuwa anatokwa na jasho sana. Hivyo yule kijana
hakupoteza muda, alimsabahi mama mjane kisha kueleza shinda yake moja kwa moja.
Kijana yule akasema samahani mama nimetoka mbali sana sehemu ambayo ni jangwani
, hivyo nimetembea muda mrefu bila kunywa maji, hivyo naomba unisaidie niweze
kupata maji ya kunywa.
Mama
mjane alipatwa na hasira kidogo kwa sababu alitegemea ambaye aligonga mlango
huenda alikuwa ni mfalme mhavila. Basi mama mjane alimtazama yule kijana kisha
akelekea ndani na kuchua maji ambayo alikuwa amemuandalia mfalme mhavila na
kumpa yule kijana.
Mara
baada ya yule kijana kunywa yale maji alimshukuru mama mjane, kisha kijana yule
akaondoka. Mama mjane alirudi ndani kwa ajili ya kumsubiri mfalme. Lakini cha
ajabu mfalme hukuweza kufika. Mama mjane alitafakari na kusema haiwezekani ni
kwanini mfalme hakuweza kutimiza ahadi?
Wakati
akitafakari hayo mara akasikia tena sauti ikitokea mlangoni, mama mjane
alifurahi sana kusikia sauti ile
ikibisha hodi kwani nafasi hii aliamini yule aliyekuwa akibisha hodi alikuwa ni
mfalme mhavila. Hivyo pasipo kupoteza muda mama mjane alielekea mlangoni kwa
ajili ya kumfungulia mfalme mhavila.
Mara
baada ya kufungua mlango ailikutana na mtoto mdogo ambaye mama mjane hakuweza
kumfahamu mtoto yule, mama mjane alijaribu kuvuta taswira ni wapi ambapo
aliwahi kumuona mtoto yule, mama mjane alikosa majibu kwani mtoto yule alikuwa
ni mgeni machoni pake.
Mtoto
alimsabahi mama mjane kisha akasema “ samahani mama yangu nimetoka nyumbani kwetu wazazi wangu
wameniacha tangu asubuhi, sijaweza kula chochote, hivyo naomba unisaidie
chakula niweze kula mama yangu, kwani naumwa na njaa sana mama.
Mama
alimtazama mtoto kwa macho yenye huruma sana, hivyo kwa kuwa muda ulikuwa
umeenda sana aliamini ya kwamba mfalme mhavila hawezi kufika kwake tena, hivyo
alichukua chakula ambacho alikuwa
amemuandalia mfalme mhavila na kumpa mtoto yule. Mtoto yule alikula na
kumshukuru mama mjane.
Mama
mjane alifunga mlango tena na kuamini ya kwamba mfalme mhavila asingeweza kuja
tena. Wakati akiwa ameketi ndani mwake mama mjane alisikia watu wakija uelekeo
wa nyumba yake wakiimba nyimbo nzuri na za kupendeza sana. Alitafakari kuna
nini? Wakati anazidi kutafakari sauti zile zilikuwa zinazidi kusogea katika
nyumba yake.
Mama
mjane alitoka nje ili kushuhudia kulikuwa kuna nini, ghafla alimuona mfalme
mhavila akiwa na umati mkubwa wa watu, mama mjane aliwaza atamueleza nini
mfalme mhavila kwani chakula alikuwa kakigawa chote. Mfalme mhavila alifika kwa
mama mjane na kusema asante sana kwa kunijali.
Mama
mjane aliwaza na kusema mfalme mhavila ananishukuru kwa lipi tena? Wakati sijamfanya
chochote?
Je mfalme Mhafavila alimshukuru mama mjane
kwa kipi hasa? Usikose itaendelea wiki ijayo siku kama ya leo,
Ndimi
afisa mipango Benson Chonya
0757909942
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.