Jul 1, 2017
KITABU; ANY THING YOU WANT(Kitu Chochote Unachokitaka).
Uchambuzi wa kitabu katika aya moja.
Watu
wengi katika maisha wanafanya mambo ambayo yanawapotezea furaha sana. Unapofanya
biashara kumbuka kutengeneza sheria nzuri zitakazokusaidia kuongeza wateja
wako. Pia Katika biashara usisahau jambo moja la msingi kwamba upo kwa ajili
ya wateja wako.
Any Thing You Want (Kitu chochote unachokitaka).
Hata
hivyo mwandishi wa kitabu hiki Derek Sivers, yapo mambo mengi ambayo ameyaongelea
katika katika kitabu chake na yana manufaa kwako pia. Twende kwa pamoja
tujifunze mambo mengine ya msingi yaliyoyachambuliwa, kwa kuangalia uchambuzi wa
kitabu kizima.
1. Ipo
tofauti kubwa kati ya kujiajiri kwenye biashara yako na kuwa mmiliki wa
biashara yako. Unapokuwa umejiajiri katika biashara na ikatokea umetoka kidogo,
kila kitu kitashindwa, lakini unapokuwa mmiliki wa biashara hata uiache
biashara yako mwaka mzima, biashara hiyo itaendelea kuwepo.
2.
Usifanye kitu chochote sababu kubwa ikawa ni pesa, fanya mambo yako kwa ajili ya kutoa
thamani, pesa itakuja yenyewe.
3. Hauwezi
kujua sana vizuri kile kitu unachataka kukifanya, mpaka kitu hicho uanze
kukifanya ndio utakijua kwa asilimia karibu zote.
4.
Mafanikio yanakuja kwa kuendelea kuweka juhudi na kuboresha kila hali katika
maisha yako. Endelea kuweka juhudi hata wakati mambo yanapokuwa hovyo.
5.
Njia bora ya kukua kibiashara ni kwa wewe kuangalia kwanza wateja wako wa
kwanza, kisha na kuendelea kutafuta
wateja wengine.
6. Ni
muhimu kujua njia za kumlinda mteja wako kila wakati, ukiweza kufanya hivyo
utajikuta upo vizuri kibiashara.
7.
Jifunze mambo mwenyewe, kwa kujifunza mambo hayo itakusaidia sana kukua wewe na
kukujengea mafanikio makubwa.
8. Kila
wakati jenga tabia ya kuamini wengine unapokuwa kwenye biashara, lakini kuwa
makini sana unapotaka kugawa majukumu yako.
9.
Chochote unachokifanya, ujue huo ndio ubunifu wako. Fanya unachokifanya kwa
ubora ili ndoto zako zitimie.
10. Unaweza
ukawa na furaha sana hata kama una kiasi kidogo cha pesa, sio lazima una pesa
nyingi sana ndio utengeneze furaha kubwa.
11.
Kila wakati usisahau kwamba unaweza ukaweka sheria au kanuni za kukusaidia
kupata chochote unachotaka na hilo linawezekana.
12.
Weka mipango mingi ambayo unaona inaweza ikakusaidia kukufanikiwa. Hakuna njia
moja ya mafanikio ambayo inasema hii ndio sahihi.
Chukua
hatua na fanyia kazi mambo hayo muhimu uliyojifunza kutoka kwenye kitabu hiki na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama
unamtaji mdogo, mtaji wa kati au mtaji mkubwa na unahitaji wazo bora la
biashara litakalokutoa kimaisha, tafadhari usisite kuwasiliana nasi kwa 0713 048 035 au tutumie e-mail kwenda dirayamafanikio@gmail.com,
kwa msaada zaidi.
Kila
la kheri katika kufikia mafanikio makubwa,
Ni wako rafiki
katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.