Aug 13, 2017
Jifunze Namna Ya Kutumia Mitandao Ya Kijamii Kwa Faida.
Watu wengi
tumejikita katika kutumia mitandao ya kijamii pasipo kupata faida yeyote. Wengi
wetu tunatumia kama kiburudisho cha nafsi. Wengi tunapenda sana kitu ambacho
kinaitwa ‘likes, followers’ na habari
mbalimbali ambazo hazina msaada wowote katika maisha yetu.
Pia taarifa
ambazo tumekiwa tunazipata katika mitandao hiyo, ni taarifa za aina moja, na ndio
maana taarifa moja ambayo itakuwa ni kuyashangaza kila mtu atatamani sana na
yeye aweze kuipost katika akaunti zake za mitandao ya kijamii. Tabia hii napenda
kuita ni ulevi wa mitandao.
Ulevi huu wa
mitandao umetufanya wengi wetu kuwa na fani ya uandishi pasipo kusomea. Unakuta
mtu kapata taarifa fulani katika mitandao ya kijamii naye pasipo kujua chanzo
cha habari hiyo, na yeye anapost katika mitandao ambayo anamiliki.
Lakini ukweli
ni kwamba kama upo makini na maisha yako, ni vyema pia ukawa makini na mitandao
ya kijamii pia. Unaweza ukawa bado unajiuliza leo Afisa mipango anazungumzia
nini? Wala usikwame mahala popote nipo kwa ajili ya kukueleza ukweli japo
ukweli huu hautaupenda, hata usipoupenda nataka lengo langu ubadilike.
Tumia mitandao ya kijamii kwa faida. |
Mitandao ya
kijamii imekuwa ikieleza bayana, jinsi watu na tabia zao jinsi zilivyo. Siku
hizi ukitaka kujua tabia ya mtu jaribu kuingia katika mitandao yake ya jamii
halafu chunguza kwa umakini kilichomo ndani ya mitandao hiyo ya jamii utajua
tabia ya mtu huyo pasina kumuuliza mtu yeyote. "Mitandao ya kijamii ni kioo
cha tabia" kwani kinatupa picha kamili ya jinsi mtu alivyo.
Upo usemi
usemao mtu akinyanyua kinywa chake kuzungumza, anaeleza yeye ni mtu wa aina
gani, kwa usemi huo huo nami naongezea mitandao ya kijamii ndiyo sehemu ambayo
inatoa picha kamili kwa watu ya kwamba wewe ni mtu wa aina gani?
Hivyo kila
wakati nakusihi kama kweli unajiheshimu na unapenda kuongeza mtandao mkubwa wa
marafiki ili kupata mafanikio makubwa, unatakiwa kuanza kuitumia kitandao ya
kijamii kwa faida kama ifuatavyo;-
1. Hakikisha
marafiki ulionao katika mitandao yako ya kijamii ni marafiki wa faida kwako.
Kwani wengi wetu katika mitandao ya kijamii tuna marafiki wengi ila marafiki wa
faida ni wachache. Mwingine ataniuliza sasa nitajuje kama huyu niliyenaye ni
rafiki wa faida? Jibu lipo wazi fuatilia vitu ambavyo anafanya na kupost
utapata majibu kwamba ni rafiki wa faida au laaah!
2. Hakikisha
unaposti vitu ambavyo vinakuelezea wewe kwa ujumla kwa watu wengine. kama ni
biashara basi tangaza mara kwa mara huduma au bidhaa ambazo unauza. Lengo la
kufanya hivi si kupata wataja pekee, bali kutakufanya uweze kuongeza mtandao wa
watu mbalimbali ambao watakuwa wanafanya mambo ambayo na wewe unayafanya, hivyo
itakuwa mwanzo mpya wa kubadilishana mawazo.
3. Hakikisha
unasoma kila siku vitu vipya katika eneo ambalo litakujenga. Ondoka mara moja
katika lile kundi la watu ambao wanapata taarifa za aina moja. Hivyo jijengee utaratibu
mpya wa kupata taarifa ambazo ni za kipekee (unique information). Kama wewe ni
mwimbaji wa muziki, hakikisha unapata taarifa ambazo zitakujenga katika eneo
hilo zaidi.
Kama niilivyosema
hapo awali ya kwamba mitandao ya kijamii huwapa watu taarifa ya kwamba wewe ni
mtu wa aina gani, hivyo jijengee utaratibu ambao utawafanya watu wapate picha
kamaili kuhusu wewe, pia kuhusu mambo mbalimbali ambayo unayafanya.
Mwisho
nimalize kwa kusema ya kwamba, jifunze kutumia mitandao ya kijamii kwa faida, kwani
ndio msingi mkubwa wa mafanikio yako.
Ndimi Afisa
Mipango : Benson Chonya
0757909942.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.