Aug 14, 2017
Mambo Manne Yatakayokusaidia Kuokoa Muda Wako Wakati Wote.
Kati
ya kitu ambacho ni changamoto kwa wengi sana ni swala la muda. Kwa watu wengi
kutunza muda na kuutumia kwa manufaa imekuwa ni changamoto kubwa na kwa bahati
mbaya wengi wanaopoteza muda sana wanaona ni kitu cha kawaida.
Madhara
ya kupoteza muda yamekuwa hayaonekanai moja kwa moja, lakini nikwambie tu hivi
kupoteza muda na kuamua kuutumia hovyo, hiyo ni zaidi ya kupoteza pesa au kwa
lugha nyingine ndio unapoteza maisha yako.
Unaweza
ukajiuliza kwa nini ninasema hivyo? Hiyo iko hivyo kwa sababu ukipoteza muda
wako sasa hata kama ni dakika moja, hauwezi kurudi mpaka unaiacha hii dunia.
Kwa msingi huo, unatakiwa kutunza sana muda wako kuliko kitu chochote.
Na
swala la kutunza muda haliji kwa bahati mbaya, yapo mambo ya msingi sana ambayo
kama umedhamiria kweli kuutunza muda wako unatakiwa uyafatilie kwa makini ili
yakusaidie kutunza muda wako kwa usahihi.
Tunza muda wako vizuri ukupe mafanikio. |
Jambo
la kwanza, hamasa.
Hapa
ni lazima kweli uwe na hamu au nia ya kutunza muda wako. Kitu cha kwanza ambacho
kitakuwa kinachemka ndani yako kwako ni kwa wewe kutaka kuona lile kusudi kutunza
muda linatimia tena kwa uhakika.
Ukiwa
una nia au shauku ya kweli ya kutunza muda wako, hii ni hatua ya kwanza kabisa
ambayo utakuwa unaanza nayo na ambayo itakuwa kama msingi wa kukusaidia kuweza
kutunza muda wako kwa uhakika.
Jambo
la pili, tafuta mwelekeo sahihi.
Huwezi
wewe ukawa mtunza muda mzuri, halafu ukawa hujui au huna mwelekeo sahihi.
Unatakiwa ujue mwelekeo sahihi wa kazi zako kwa siku, kwamba zitakwendaje, utafanya nini wapi na wakati gani.
Ili
kufanikiwa katika hili hutakiwi kuanza siku yako bila kujua siku inayofuata
utafanya nini wapi na kwa wakati gani. Weka ratiba yote ya mambo yako ambayo
unatakiwa kuyatekeleza kwa siku husika na uyafatile, hapo utaokoa muda wako.
Jambo
la tatu, maamuzi sahihi.
Tunaona
hapa kuwa na mwelekeo sahihi na hamasa ya kutunza muda peke yake hiyo haitoshi, unatakiwa kuongeza
kitu cha ziada ambacho ni kuwa na maamuzi sahihi. Lazima maamuzi yako yawe
sawa. Ukiwa na maamuzi ya kutanga tanga, utapoteza muda wako sana.
Ni
muhimu hapa kujua unatakiwa kufanya kitu gani wapi na wakati gani. Unapojijengea maamuzi sahihi, utajikuta
unaokoa muda wako mwingi ambao pengine ungeweza kupotea bila sababu ya msingi
kwako.
Jambo
la nne, nidhamu binafsi.
Itakuwa
ni kazi bure kufanya mambo yote tuliyotangulia kuyaongea kama huna nidhamu
binafsi. Unatakiwa uwe na nidhamu binafsi katika kutekeleza majukumu yako kama
ulivyoyaweka kulingana na siku hiyo.
Kwa
kuzingatia mambo hayo, itakuwa ni silaha tosha kwako wewe ya kuweza kukusaidia
kutunza muda wako vizuri na kwa uhakika mkubwa. Ikitokea kama hautafanya hivyo sahau kutunza muda na utaendelea
kuupoteza.
Chukua
hatua, kila la kheri katika kufikia mafanikio yako na endelea kutembelea
dirayamafanikio.blogspot.com kujifunza kila wakati.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.