Aug 11, 2017
Jinsi Ya Kutengeneza Tambi Za Dengu.
Karibu sana mpenzi msomaji
wa blog hii ya dira ya mafanikio, lengo letu ni kuhakikisha kila mmoja
anatimiza kusidio lake hapa duniani. Kama utakuwa ni mdau wetu mzuri tayari
tumekwisha fundisha namna ya kutengeneza tomato souce, chill souce, karanga za mayai,
tambi za mayai. Hivyo kwa kuwa tunajali uwepo wako kila wakati siku ya leo tutajifunza namna ya kutengeneza tambi za dengu.
Mahitaji:
1. Unga
wa dengu ½ kilo
2. Binzari
nyembamba ½ kijiko cha mezani
3. Unga
wa pilipili manga kijiko 1 cha chai
4. Unga
wa mchele ¼ kilo
5. Chumvi
kiasi
6. Mafuta
ya alizeti ½ lita
7. Baking
powder
Namna
ya kutengeneza
Changanya unga wa mchele
pamoja na ule wa dengu. Kisha chukua nyunyuzia baking powder na baadaye chumvi.
Weka unga wa binzari nyembamba na pilipili manga. Changaya vizuri na kisha weka
maji kidogo kidogo huku ukukanda hadi liwe donge gumu kama unavyofanya kwenye
maandazi. Baada ya hapo weka donge lako pembeni na funika. Acha likae kwa muda
wa nusu saa hadi saa moja.
Baada ya hapo chukua karai
la mafuta weka jikoni acha hadi mafuta yapate moto kabisa. Kisha chukua mashine
ya kupikia tambi na weka donge lako. Kandamiza taratibu huku ukiruhusu
minyororo ya tambi kuingia kwenye mafuta yaliyo jikoni.
Weka kiasi kiasi huku
ukikaanga. Acha mpaka zitakapokuwa zimeiva na kukauka vizuri. Ipua na weka
pembeni. Weka kwenye sahani safi na kavu. Tambi zako zitakuwa tayari kwa
kuliwa.
Tafuta fingushio vizuri
funga kisha peleka sokoni, wengine wataniuliza afisa mipango mashine hizi za
dengu nazipata wapi? Wala usijali mashine hizi zipo nenda kwenye maduka ambayo
yanauza vyombo mbalimbali vya mapishi kisha ulizia ya kwamba unataka mashine za
kutengeneze tambi watakupa.
Mpaka kufikia hapo hatuna la
ziada tukutane siku nyingine, kama unahitaji masomo mengine kama haya ya
ujasiriamali usisite kuwasilaina nasi.
Ndimi
Afisa Mipango Benson chonya,
0757909942,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.