Aug 15, 2017
Unajenga na Kubomoa Maisha Yako Hivi…
Ni rahisi
kwenye maisha yako kuwajibika, kama kweli umeamua kuwajibika na kufanya mambo
yanayo kuwajibisha.
Ni rahisi
kwenye maisha yako kuendelea na hali ya utoto, kama bado unaendekeza utoto huo
na huna dalili hata ya kubadilika.
Ni rahisi
kwenye maisha yako kuendelea kuwa mkomavu wa kifikra na maisha kwa ujumla, kama
kweli mambo ya ukomavu ndio unayoyafanyia kazi.
Ni rahisi
kujiamini kwenye maisha yako, kama unafanya mambo yanayopelekea kujiamini kwenye maisha yako pia.
Ni rahisi
kuwa na mtu wa sababu na kushindwa kuchukua hatua kama hizo sababu ndizo unaona
kwako zinakusaidia sana.
Jenga maisha yako kwa kuchukua hatua sahihi. |
Ni rahisi
kuendelea kuwa mvivu, kama unaendeleza uvivu usio na maana kwenye maisha yako na
kila wakati.
Ni rahisi
kuendelea kubaki kwenye umaskini, ukiwa hujaamua kujitoa hasa kupigania kutoka
kwenye umaskini.
Ni rahisi
kuendelea kuwa mbunifu, kama ubunifu ndio unaotafuta kwenye maisha yako na
kuamua kujishughulisha ili kupata ubunifu huo.
Ni rahisi
kubaki katika hali yoyote ile, uwe unataka au hutaki ili mradi tu hali hiyo
unaifanyia kazi kila mara.
Jiulize,
kitu gani unachokifanya sasa kwenye maisha yako? kitu hicho unachokifanya na
unakizingatia sana itakuwa ni sehemu ya maisha yako.
Hakuna
muujiza, hakuna matokeo ya kushangaza, kile unachokifanya, kile unachokizingatia
utakuwa kama kitu hicho.
Matendo
yako yanaonyesha wewe utakuwa ni mtu wa aina gani. Vile ulivyo na utakavyokuwa
kunaenda sawa na matendo yako.
Washindi
wanachukua hatua zinazowafanya wazidi kuwa washindi, wanaoshindwa pia huchukua
hatua zinazowapelekea kushindwa.
Usipoteze
muda wako kufanya mambo ambayo yatakutoa kwenye ramani ya mafanikio yako, fanya
mambo ya kukujenga kimafanikio.
Chochote
unachokitaka kwenye maisha yako, usipoteze muda kukisubiri, badala yake chukua
hatua za kufanya.
Fanya
vitu ambavyo vitakusogeza karibu kabisa na ndoto zako. Fanya vitu ambavyo vitafanya
malengo yako yaweze kutimia.
Unaweza
kuwa chochote, unaweza kuwa mtu wa mafanikio, unaweza kuwa mtu wa kukubalika,
uamuzi wa yote hayo upo mkononi mwako.
Hakuna
kinachoshindikana kwako, kumbuka kama nilivyosema, jinsi unavyofanya mambo kwa
namna fulani ndivyo unavyojenga au kubomoa maisha yako.
Kwa kifupi
unajenga na kubomoa maisha yako kutokana na hatua unazoamua kuchukua ziwe ndogo
au kubwa.
Nikutakie
kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa na endelea kutembelea
dirayamafanikio.blogspot.com kujifunza kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.