Aug 17, 2017
Kinachosababisha Mahusiano Mengi ya Kimapenzi kufa Ni Hiki.
Habari
za muda huu mpenzi msomaji wa mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO ni matumaini yetu u mzima na unaendelea na
majukumu yako ya kila siku, Nikuarike kwa moyo mkunjufu siku ya leo ili tuangalie kwa pamoja chanzo cha mahusiano
mengi ya kimapenzi kufa.
Tumekuwa
ni mashuhuda wazuri tukishuhudia mahusiano ya kimapenzi yanapoanza, huwa
yaanaanza kwa mbwembwe nyingi sana, lakini yanapokuja kufa huwa ni kimya kimya,
wale wale ambao tuliwashuhudia wakitembea kwa pamoja mara baada ya mahusiano
hayo kufa, tumekuwa tukiona kila mtu yupo kivyake.
Licha
ya kuendelea kushuhudia hivyo, ukichukunguza kwa umakini sababu ya kufa kwa
mahusiano hayo utakuja kugundua kitu kimoja kikubwa ambacho kimesababisha kufa
kwa mahusiano hayo ni; uwongo unapobadilika kuwa ukweli.
Hii
ni sababu kubwa sana ambayo husababisha mahusiano mengi kufa, na sababu hii
ndiyo husababisha mtafaruko mkubwa katika mahusiano yaliyo mengi. Hii ni
kwa sababu watu wengi ambao wanaingia katika
mahusiano hutumia njia ya kudanganya ili aweze kumpata fulani, kwa sababu
katika sayari ya leo bila uongo mapenzi hayaendi.
Kuwa mkweli kwenye mapenzi. |
Hii
ipo wazi, ya kwamba mapenzi ni uongo ambao hufanana na ukweli. Wakati mwingine
kabla hujaanza mahusiano na mpezi wako, huwa kunakuwapo na ahadi nyingi sana
ambazo zipo baadhi huwa ni za ukweli na zipo nyinginezo ambazo huwa ni za
uongo.
Na
hizo nyinginezo za uongo pale ambapo inakuja kugundulika ya kwamba zilikuwa za
uongo ndipo unakuwa mwanzo wa mahusiano hayo kufa, unakuta mtu wakati wa
kumtongoza msichana fulani anamuahidi vitu vingi vya uongo msichana huyo, na
msichana huyo pasipo kujua anajikuta anakubali huku akitegemea kwamba ahadi zote alizoahidiwa na mpenzi wake
zitakuja kuwa ukweli, mwisho wa siku ahadi hizo zinabaki kuwa stori mwisho wa
siku msichana huyo anaamua kuachana na mwanaume huyo.
Kwa
mfano unakuta mtu anamwambia mtu ukiwa na mimi nitakupa nyumba, gari, fedha lakini
baada ya muda kadhaa kupita vitu hivyo vinaishia kwenye maneno tu.
Na sababu
nyingine ambayo husababibisha mahusiono mengi kufa ni kitu ambacho kinaitwa
matarajio. Na matarajio hayo huwa katika ahadi ambazo zilikuwepo wakati awali.
Unakuta mtu kabla hajaingia katika mahusiano na mtu fulani anakuwa anatarajia kupata kitu fulani kutoka kwa mtu huyo, mwisho wa
siku kitu hicho ambacho alikuwa anatarajia anakuta hakipo.
Hivyo
akikuta hakipo mwisho wa siku anaamua kuachana na mtu huyo na kwenda kwa mtu
mwingine. Hivyo mambo makubwa ambayo hubomoa mahusaiano ya kimapenzi ni hayo
ambayo nimeyaeleza.
Ndimi afisa mipango Benson chonya,
bensonchonya23@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.