Aug 3, 2017
Misingi Ya Kuzingatia Katika Utunzaji Wa Vifaranga.
Ufugaji wa kuku imekuwa ni kazi muhimu na inayokubalika
katika jamii nyingi. Ni kazi isiyohitaji gharama kubwa sana, ambayo imekuwa na
mafanikio kwa kiasi kikubwa kwa wanaiofanya kibiashara.
Tatizo ambalo limekuwa sugu na kusababisha hasara kwa wafugaji walio wengi, ni kutofahamu namna bora ya kuwatunza vifaranga kuanzia siku ya kwanza wanapoanguliwa hadi kuwa kuku wakubwa. Hali hii imekuwa ikiwasababishia wafugaji hasara na kuwakatisha tamaa.
Hii inatokana na wafugaji kuzingatia kuwa na banda na chakula tu, bila kuzingatia aina nyingine ya matunzo muhimu yanayohitajika kwa ajili ya kuwafanya vifaranga waishi na kukua wakiwa na afya.
Leo katika makala haya ya kilimo na ufugaji
tunakuletea baadhi ya mambo muhimu ya kuzingatia kuanzia siku ya kwanza ili
vifaranga wako wasipate madhara na hatimaye kufa;-
Mara baada ya kuanguliwa, vifaranga wawekwe
sehemu yenye joto kwa wastani unaohitajika.
Hakikisha sehemu ya banda ulipowaweka
vifaranga ni kavu, na isiyokuwa na vimelea.
Hakikisha vifaranga wote wanapata chanjo ya
mahepe (mareks) siku ya kwanza.
Siku ya saba, vifaranga wachanjwe dhidi ya ugonjwa wa kideri.
Inapofika siku ya 14, vifaranga wachanjwe
dhidi ya ugonjwa wa gumboro.
Rudia chanjo ya kideri katika siku ya
ishirini na moja.
Siku ya ishirini na nane, rudia tena chanjo
ya gumboro
Baada ya wiki nane, hakikisha kuwa vifaranga
wako wanapata chanjo ya ndui.
Kwa kuzingatia mtiririko huo, utakuwa na
uhakika kuwa kuku wako ni salama. Watakuwa bila tatizo, jambo ambalo litakupa
uhakika wa kuwa na mazao bora, na hatimaye kupata faida.
Pamoja na hayo, hakikisha kuwa unazingatia
lishe bora. Hii itasaidia kuwapa kuku afya njema na kuzalisha kwa kiwango
kinachotakiwa.
Kwa mahitaji ya vifaranga bora waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika;-
1. Hawa ni wauzaji wa vifaranga bora wa kuku wa kienyeji asilia, kuroiler na sasso.
2. Faida za
kununua vifaranga kutoka kwetu ni kuku wanakuwa na maumbo makubwa, wanahimili
magonjwa, wanawahi kutaga na unapewa ushauri wa kitaalamu juu ya ufugaji.
3. Bei zetu ni
Tsh. 2000/= kwa kila kifaranga.
Karibuni sana, kwa mawasiliano tumia namba za simu 0686 141 0 97/ 0767 048 035.Tunapatikana
Tanga – Tanzania.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.