Aug 5, 2017
Kama Huna Mtaji Na Unahitaji Kuwekeza, Fanya Hivi Kwanza…
Unapokuwa
na kiasi fulani cha pesa, na unataka pesa hizo ziongozeke, sina shaka kitu
pekee ambacho unachotakiwa kufanya ni kuwekeza pesa hizo ili zikuletee matokeo
unayoyataka. Kwa kuwekeza pesa hizo itakusaidia kujenga uchumi imara wa kipesa.
Halikadhalika,
unapokuwa hauna pesa, kitu gani unachotakiwa kufanya? Pia hapa, unatakiwa
kuwekeza vizuri katika rasilimali ulizonazo kama muda wako, kipaji chako, maarifa, uzoefu wako na hata nguvu ulizonazo.
Kama
wenye pesa wanavyowekeza, pia kama huna kitu unatakiwa kuwekeza katika
rasilimali hizo za msingi ili kujenga msingi mkubwa wa mafanikio yako kesho. Hutakiwi
kulia eti huna pesa, wekeza katika vile ulivyonavyo ndani mwako kwanza.
Pia
unaweza ukajiuliza nitawekeza vipi wakati sina pesa, sikiliza kuwekeza katika
maisha yako haimaanishi kila wakati lazima ukawa unapesa, anza kuwekeza na yale
mambo ambayo yatakupa faida kesho. Kivipi hili linawekana? Sikiliza.
Wekeza muda wako vizuri ukusaidie kufanikiwa. |
Anza
kuwekeza kwenye muda wako, kwa kuwa sasa hivi pengine hauna kitu cha kufanya,
muda wako wekeza kwa kujifunza katika mambo mbalimbali. Wekeza muda wako
kujifunza juu ya mafanikio au chochote ukitakacho.
Kwa kadri
unavyojifunza hapo unakuwa unatengeneza thamani kubwa sana kwako itakayokuingizia
kipato. Hakuna maarifa ambayo yanatumiwa vizuri yanamwangusha mtu, tumia muda
wako kujifunza utaona matokeo bora sana kwako.
Anza
kuwekeza kwenye nguvu zako, hakuna mtu ambaye amezaliwa hana nguvu. Kila mtu
ana nguvu fuani, kwa kuwa huna mtaji na huna kiato cha uhakika hebu zitumie
nguvu zako zikusaidie kukuingizia pesa zitakazokusaidaia kukutoa hapo ulipo.
Tumia
nguvu zako kwenye kilimo, tumia nguvu zako kwenye kubeba mizigo, tumia nguvu
zako kwenye chochote kile unachoweza ili ziwe na manufaa kwako. Hujapewa hizo
nguvu zako bure, zifanyie kazi.
Anza
kuwekeza kwenye vipaji vyako, kaa chini ujiulize una kitu gani cha thamani
ambacho ukikitumia kinaweza kukusaidia kufanikiwa? Kama ni kuchora, chora
kweli, kama ni kuimba, imba kweli, kipaji chochote ulichonacho kitumie.
Wengi
wanaojua kutumia vipaji vile walivyonavyo wanafanikiwa sana, nawe pia unaweza
kuwa miongoni mwao. Kitu kikubwa unachotakiwa kujua, usijidharau, jiamini na
kisha tafuta kipaji chako na kitumie mara moja.
Anza
kuwekeza kwenye uzoefu na maarifa ulionayo, tumia uzoefu wako na maarifa hata
kama ni kidogo kutafuta fursa za kibiashara. Unaweza kuwashirikisha watu
wengine wazo ulinalo na ikakusaidia kupata mtaji na hatimaye kufanikiwa.
Hapa
kwa kifupi namaanisha unaweza kuwa mtu wa kati, yaani kutafuta fursa na
kumshirikisha yule mwenye pesa au uhitaji na yeye akakulipa. Huhitaji kuona haya kwenye maisha, vinginevyo
utaumbuka.
Kwa hiyo
mpaka hapo unaona ili kufanikiwa kila mtu anahitaji kuwekeza. Mwenye pesa
anahitaji kuwekeza pesa zake sana na hata pia na wewe ambaye hauna pesa
unahitaji kuwekeza vile vitu vya msingi ulivyonavyo.
Usijidanganye
kuanza kuangalia ‘season movies’ usiku na mchana kwa kuwa eti bado hujaaliwa na
serikali au huna kitu cha kufanya. Nikupe uhakika kama unafanya hivyo basi
umeamua kupoteza maisha yako mwenyewe tena kwa hiari yako.
Kumbuka
hitaji la kuwekeza kila siku kila mtu analo bika kujali mtu huyo ni maskini au
tajiri. Fanyia kazi haya uliyojifunz aleo na endelea kutembelea
dirayamafanikio.blogspot.com kujifunza kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.