Aug 9, 2017
Mbinu Mpya Za Kumfanya Mteja Kuwa Mfalme.
Moja kati ya
changamoto kubwa ya ufanyaji wa biashara ni kule kufanya kazi kwa mazoea,
nasema hivi kwa sababu wafanyabiashara wengi husikika wakisema ya kwamba mteja
ni mfalme, lakini katika hili kumekuwa na ukakasi ni wateja wachache sana ambao
huuona ufalme huo.
Hii ni kwa
sababu wafanyabiashara wachache sana ambao wamekuwa wakijua ni nini maaana ya
mteja. Wafanyabiashara wengi wamekuwa wakimchukulia mteja pale anapokuja kwenye
biashara ambayo anafanya tu. Kufanya hivi hufanya kuoina ramani ya biashara
haina busara kwani biashara utazidi kuiona ni ngumu siku zote.
Hivyo ili
uweze kumfanya mteja wako awe ni mfalme unatakiwa kufanya mambo yafuatayo;
1. Acha mara
moja kumsubiri mteja wako aje kukufuata mfanyabiashara mahali ulipo, bali anza
utaratibu wa kumfuta mteja wako mahali alipo, kufanya hivyo kutamfanya mteja
wako ajisikie huru na pia ajihisi kuwa yeye ni mfalme kweli, na pia kufanya
hivi kutamjengea utaratibu mpya na pia kujiona yeye si mteja tu kwako bali ni
sehemu ya biashara yako.
2. Tengeneza
utaratibu mpya wa kuwa na mawasiliano ya karibu na mteja wako, si umekuwa
ukisema ya kwamba mteja ni mfalme, kama ndivyo hivyo basi hakikisha ya kwamba
unakuwa na mawasiliano na wateja, mawasiliano haya chochonde naomba yawe ni kwa
ajili ya biashara tu, kwani pindi ukiyatumia mawasiliano hayo kivingine basi
jiandae kuwafukuza wateja wote ulionao. Mawasiliano haya yawe ni yale ya
kuwajuza wateja kuhusu ujio wa bidhaa mpya.
3. Jifunze
mbinu mpya ya kuweza kufanya mazungumzo na wateja. Hivi hujawahi kenda katika
biashara ya mtu mwingine mpaka ukajuta ni kwanini ulienda mahali hapo, bila
shaka kama hali hii imewahi kukutokea basi ni vyema katika biashara yako uweze
kujenga utaratibu mpya ambao utakufanya wateja wako wajisiie huru kila wakija
wako.
4. Uchawi
mkubwa ambao unafanyika katika biashara ni kutoa ofa kwa wateja wako. Hii ni
siri ambayo nakuibia wewe siku ya leo, haijalishi ni biashara gani ambayo
unaifanya ila ili uweze kukua katika biashara hiyo ni vyema ukajiwekea
utaratibu wa kutoa ofa katika biashara yako, jitahidi kutoa ofa kama yafanyavyo
makampuni ya simu kufanya hivi kutawafanya wateja wengi waje kwako.
Asante sana
kwa kusoma makala haya, mpaka kufikia hapo sina na ziada nikutakie siku njema na
kazi njema.
Niliandika
makala haya ni yuleyule wa siku zote, afisa mipango Benson Chonya.
0757909942,
bensonchony23@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.