Aug 4, 2017
Tabia Mbaya Za Fedha Zinazowaacha Wengi Kwenye Umaskini.
Idadi
kubwa ya watu linapokuja suala la pesa, wapo makini sana na tabia kama kupanga mipango mizuri, kutumia
pesa kwa busara na hata ikiwezekana kubana matumizi ili kuhakikisha usalama wa
pesa unakuwepo.
Lakini,
hata hivyo pamoja na wengi kijitahidi kufanya hivyo, bado zipo tabia ambazo
watu wanazo zinawaacha au zinasababisha wengi kuendelea kubaki kwenye umaskini
ingawa ukiangalia pia watu hao wana uwezo wa kupata pesa kila wakati.
Kwa hiyo
hapa unaona tatizo la watu wengi sio kupata pesa, kama ni pesa kweli wanazipata,
ila shida inakuja kwa kukumbatia tabia hizo ambazo zinawarudisha nyuma sana na
matokeo yake kuwaacha katika dimbwi la umaskini.
Leo hapa
katika makala haya, tunakuletea tabia mbaya ambazo kwa mtu yeyote akiwa nazo ni
lazima mtu huyo ataendelea kubaki kwenye umaskini. Hakuna ujanja katika hili,
kama una tabia hizi, nimesema utaendelea kubaki kuwa maskini.
Weka kumbukumbu ya pesa zako. |
1. Kushindwa kuweka kumbukumbu ya matumizi
yako.
Haijalishi
unakipato kikubwa au una kipato kidogo, kuandika matumizi yako ni jambo la lazima
ili uweze kufanikiwa. Kitendo cha kuwa na kumbukumbu na matumizi yako si suala
la kumwachia Bill Gates peke yake hata wewe linakuhusu.
Huhitaji
kutumia pesa zako tu hovyo kwa sababu eti unazo, unachotakiwa kujua ni wapi
kila pesa yako inakwenda. Zoezi hili litakusadia sana kuwa makini na pesa zako
na kukuokolea pesa nyingi ambazo zingepotea bila sababu.
Hili
jambo liko wazi, hutaki kuweka kumbukumbu zako vizuri, utake usitake huwezi
kutoka kwenye umaskini hata ufanyeje. Kama unabisha wafatilie watu wenye pesa
nyingi sana, utaona hili wanalifanya sana maishani mwao.
2. Mhemko wa matumizi.
Tunaposema
mhemko wa matumizi ni kufanya matumizi ya pesa kwa kutawaliwa na hisia zako.
Hapa unakuwa unafanya matumizi kwa kuongozwa sana na hisia na unakuja kushituka
kile kipindi ambacho pesa zako zimekwisha.
Kwa mfano,
kwa sababu una pesa kila kitu kinachopita machoni mwako unataka unanunue, zizikipita
nguo unataka kununua, kikipita kitu hiki au kile unataka kununua pia, huu ndio
mhemko wa matumizi tunaouzungumzia hapa na ni tabia mbaya ya kipesa..
Watu
matajiri wapo makini sana na matumizi yao, na hiki kitu hata wewe unatakiwa kuwa
nacho ili kutengeneza utajiri wako. Pia kama hutaki kuwa makini na matumizi
yako na kutawaliwa na mhemko, elewa utaendelea kubaki maskini.
3. Kung’ang’ania njia moja ya kipato.
Kati
ya hatari kubwa sana ambazo watu wengi wanacheza nazo na inawaacha kwenye
umaskini ni kung’ang’ania kuendelea kuwa na njia moja ya kuengeneza kipato. Utakuta
mtu anapata pesa nyingi kweli lakini njia ya kipato kimoja inamuangusha.
Najua
unawajua watu ambao walikuwa wakifanya kazi kubwa na zenye mishahara mikubwa,
lakini mara baada ya kuacha kazi unashangaa maisha yao yako hovyo sana. Yote
hiyo inasababishwa na kuwa na chanzo kimoja cha kipato.
Labda
tuseme hivi, utake usitake kama una njia moja ya kipato kuendelea kubaki
maskini kunakuhusu kwa asilimia mia moja. Pigana na hali yako kwa kila namna
uweze kutengeneza njia nyingne ya kutengeneza kipato, ndio utatoka..
4. Kukosa uvumilivu.
Sikuzote
ili kupata pesa hakuji mara moja tu, ni zoezi ambalo linahitaji sana uvumilivu
na kuchapa kazi kwa juhudi zote. Wengi wanashindwa kujua hili na kushindwa
kuwekeza kwenye vitega uchumi ambavyo vingewapa pesa nyingi kwa baadae.
Kama
unatabia za kutaka kupata pesa nyingi kwa chapu chapu na kushindwa kuwa mvimilivu
sahau jambo hili. Unatajiri una kawaida ya kujengwa hatua kwa hatua hadi
kufikia kilele kikubwa cha mafanikio.
Hizo
ndizo tabia nne ambazo zinawaacha wengi kwenye umaskini, ingawa ule uwezo wa
kupata pesa wanakuwa nao. Fanyia kazi hayo uliyojifunza, chukua hatua kila siku
kuelekea kwenye mafanikio yako na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Blog; dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.