Nov 9, 2018
Thamani Ya Mafanikio Kidogo Ya Leo, Ni Utajiri Tosha Kwako Kesho.
Ni
rahisi tu unaweza kupuuza mafanikio uliyoyapata leo kwa kuona mafanikio hayo ni
kidogo sana na hayakusaidii kwa chochote. Hali hiyo inatokea kwa wengi na
kutokana na hali hiyo watu hao hujikuta wakizidi kuporomoka sana kimafanikio.
Mathalani,
tuchukulie umefanya biashara ya aina fulani na ukapata faida kidogo tu,ambayo
kwa mtazamo wako, unaona faida hiyo ni kidogo, hivyo unaamua kuitumia yote kwa
kudharau kwamba faida hiyo ni kidogo sana na haina msaada.
Kama
ikatokea ukafanya hivyo katika mazingira yoyote yanayofanana na kama
nilivyoeleza hilo ni kosa kubwa kimafanikio. Iko hivyo kwa sababu mafanikio
yako yanategemea sana leo yako unafanya
nini cha faida hata kama ni kidogo kama nukta.
Umuhimu
wa mafanikio ya leo hauwezi kupuuzwa kwa sababu eti mafanikio hayo uliyo yapata
kidogo. Unatakiwa kuchukulia kila aina ya mafanikio hata kama ni madogo sana
kwa uzito ule ule mkubwa.
Hakuna
anayeamka asubuhi akiwa amefanikiwa. Mafanikio yote duniani yanajengwa kidogo
kidogo tena kwa muda mrefu. Hivyo unapofanikisha jambo fulani hata kama ni dogo
usilidharau, linathamini kwani litakupa mafanikio makubwa baadae.
Kitu
usichokijua pengine, thamani ya mafanikio yako ya leo hata kama ni kidogo, ni msingi
mkubwa wa utajiri wako wa kesho. Ili mafanikio hayo madogo yakusaidie na usiyapuuze,
anza kuyafanyia kazi hivi;-
Thamani mafanikio yako hata kama ni kidogo. |
Mosi,
weka malengo ya muda mrefu ya kimafanikio.
Katika
kuweka malengo ya muda mrefu ya kimafanikio usijali kitu chochote, hata kama
leo hii upo kwenye changamoto kubwa sana na unapata mafanikio kidogo, wewe
malengo hayo jiwekee na anza kuyafatilia siku hadi siku na ipo siku utashangaa
unayafanikisha.
Jiulize
malengo uliyonayo ni yapi? Je, una malengo ya kujenga ‘Logde’ au una malengo ya kujenga hoteli kubwa? Bila kujitilia
shaka yaandike malengo hayo na ikiwezekana chora picha ya hicho unachokitaka
ili ukumbuke vizuri.
Kwa
jinsi ambavyo malengo yako yatakuwa karibu na wewe yaani hapa namaanisha kwenye
picha na kwenye maandishi, ndivyo utajikuta unazidi kuchukua hatua za kufikia
malengo hayo hata kama ni kwa kidogo kidogo.
Sasa
ni nini kinachoshindikana, naamini hakuna, kama iko hivyo weka malengo yako.
Usiue ndoto zako eti kisa upo kwenye wakati mgumu wa kimafanikio au kile unachokipata
ni kidogo. Weka malengo yako unayotaka kuyafikia hata kama mfukoni mwako hauna
kitu.
Pili,
Tatua matatizo yako ya leo, kabla kesho haijafika.
Ukijifunza
kutatua changamoto zako mapema kila siku, hiyo itakusaidia sana kuweza kupiga
hatua na kuondoa kuahirisha ambako inaweza ikawa chanzo cha kukwamisha. Kitu
unachotakiwa kukitatua leo, kitatue bila shida.
Kwa nini
nakwambia hapa utatue changamoto zako mapema? ni kwa sababu changamoto
zinapokuwa ndogo zinakuwa hazihitaji gharama kubwa sana na hilo litakusaidia
kwa sababu ya kile kidogo unachokipata.
Ni
rahisi kujiingiza kwenye matatizo ya kila siku, ikiwa kila kitu hutakitatua kwa
wakati. Unatakiwa kutatua kila changamoto mapema sana ili uweze kuishikwa uhuru
na mafanikio kwa kile kidogo unachokipata.
Kwa hiyo
mpaka hapo unaona mafanikio yoyote unayopata hata kama ni madogo, yanaweza
kukusaidia kufanikiwa na ukafika mbali ikiwa utayafanyia kazi vizuri na kwa
umakini mkubwa. Chukua hatua.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kujifunza kila
siku.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.