Nov 23, 2018
Mbinu Za Kujitofautisha Kibiashara Hatimaye kupata Faida.
Babu yangu aliwahi kunisihi ya kwamba kufanya biashara na hatimaye kufanikiwa katika biashara hiyo kunahitaji juhudi za maksudi kutoka kwa mfanyabishara husika. Hii ni kwa sababu kufanya biashara ni kumsubiri mteja ambaye huna imani ya kwamba atakuja ama la.
Pia ulimwengu wa sasa kila kitu kinachonekana kwa macho
kimekuwa ni biashara na biashara hizi asilimia 99.9 ni biashara ambazo
zinafanana, hivyo ili uweze kuona unafanikiwa katika biashara hiyo ni lazima
uwaze juu ya kujitofautisha kibiashara hatimaye upate faida.
Swali linaweza kuja ni je najitofautishaje kibiashara? Wala
usipate tabu nipo hapa kwa ajili ya kukata kiu ya maswali yako kama ifutavyo:-
Ili uweze kuwa ni mtu wa tofauti katika biashara unayoifanya
unatakiwa kuhakikisha unajikita zaidi katika kuhakikisha unatangaza biashara
yako kwa kiwango cha hali ya juu na ya kipekee, kwani ukweli ulio bayana na
usiopingwa ni kwamba biashara nzuri na yenye kuleta faida kubwa chanzo chake ni
matangazo.
Jambo jingine linakalokusaidia kuwa ni mtu wa kitofauti katika
biashara yako ni kuhakikisha ya kwamba unaboresha zaidi katika kitengo cha
huduma kwa wateja. Mfanye mteja wako asikuchoke yaani kuanzia anapokuja mpaka
anapoondoka, awe ni mtu ambaye anajisikia furaha na amani muda wote na hii yote
itatokana na vile ambavyo utakavyompokea na kumuhudumia.
Pia jifunze kuweka mazingira ya ofisi yako katika muonekana
nadhifu na wenye kuvutia kila mteja anayepita au anayekuja, hii ni kuanzia
mapambo yako, upangaji wa vitu vyako vya kuuza na vile visivyo vya kuuza pia.
Mwisho kabisa kila wakati unatakiwa kukumbuka hakuna mteja
anayependa kucheleweshewa kupata huduma, hivyo jifunze kutoa huduma yako kwa
haraka na kwa wakati muafaka.
Mpaka kufikia hapo sina la ziada, kazi ibaki kuwa kwako katika
utekelezaji wa hayo niliyoyaeleza. Nikutakie siku njema na mafanikio ,ema, na
Mwenyezi Mungu akawe pamoja nawe katika utekelezaji wa majukumu Yako.
Ndimi Afisa Mipango
Benson Chonya.
0757-909942
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.