Nov 15, 2018
Mafanikio Yako Yanatengenezwa Na Muda Huu Tu.
Kati ya kitu ambacho huwezi kucheza nacho na ikitokea umekipoteza ndio imetoka hiyo, ni muda ulionao. Unaweza ukacheza na vyote kwenye maisha yako na ukavipoteza na ukaanza upya hadi kufanikiwa, lakini si muda wako, ukipoteza muda haurudi tena.
Upo uwezekano pesa
ukaiweka ya akiba kama umeipata pesa nyingi na ya ziada. Hata hivyo inapotokea
pesa imepotea, upo uwezekano pia wa kuweza kutafuta pesa zingine kwa baadae na
ukawa tena na pesa kama kawaida utafikiri hukupoteza kitu.
Lakini uwezekano
huo ambao upo kwenye pesa hauwezi kutokea hata kidogo kwenye muda wako. Muda
ulionao ni kitu kingine ambapo thamani yake haipimiki kwa chochote. Unapochagua
kupoteza muda wako ndio unapoteza maisha yako kabisa.
Unayo nafasi moja
tu ya kufanya maisha yako ya kesho yawe bora ikiwa utaitumia leo kwa uhakika.
Unayo nafasi moja ya kutumia fursa uliyonayo kwa uhakika hadi kufanikiwa kwa
muda ulinao. Ikiwa utajichanganya na kutumia fursa hovyo huwezi kufanikiwa.
Muda ulionao leo
unaweza kufanya maisha yako ya kesho yakawa mazuri sana au yakawa hovyo kabisa,
kikubwa tu inategemea muda wako unautumiaje? Kama unautumia muda wako hovyo
andika maumivu.
Ndio maana
unatakiwa utambue leo yako ikipita, hiyo ndio imepita haiwezi kurudi tena. Kwa
hiyo kama kuna jambo umeliahirisha na kuamua kulifanya kesho, basi ujue kabisa
umesogeza mafanikio yako kesho.
Unachotakiwa kujua
kitu kingine kinachowaangusha watu wengi kwenye maisha si kwa sababu hawana
uwezo huo, bali kinachowaangusha ni kwamba wamekuwa ni watu wa kutumia muda wao
hovyo sana kila siku.
Kama unajiona huna
cha kufanya kwenye maisha yako, hebu tumia muda wako kidogo ulionao kuweza hata
kujifunza juu ya maisha kupitia vitabu au semina ili uweze kubadilisha maisha
yako. Usikubali kupoteza muda wako hovyo hiyo ni hatari kubwa sana kwako.
Juhudi zako lazima
ziendane na kutambua umuhimu wa kutunza muda wako ili kufikia mafanikio
makubwa. Ikiwa utakuwa unaishi tu kiholela na kuona muda kwako ni kitu ambacho
hakina thamani kabisa utapotea.
Kumbuka kila wakati
muda unaotengeneza maisha yako ni muda huo huo mdogo ambao unaouna hauna
thamani huo ndio unaofana maisha yako yawe bora au hovyo kabisa. Unatakiwa kuwa
makini na muda wako ili kujenga maisha uyatakayo.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki
katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.