Nov 12, 2018
Kama Utashindwa Kutumia Mambo Haya Matatu Vizuri, Huwezi Kufanikiwa.
Ukiwaangalia watu wengi
kwa mtindo ambao wanaendesha maisha yao, ni rahisi sana kusema watu hao hata
wafanyaje hawataweza kufanikiwa kwenye maisha. Unaweza ukajiuliza swali hapa
nimejuaje kama hawawezi kufanikiwa?
Sikiliza
nikwambie. maisha ya mafanikio ni kama sayansi kama zilivyo sayansi
zingine, hata kama hujui lakini ndivyo ilivyo. Hakuna swala linaitwa
kubahatisha, ni matokeo ya kufanya vitu vya aina fulani ndiko kuna kupa
mafanikio yako uyatakayo.
Kwa hiyo hili swala
sio la uwe mtabiri au upige ramli ndio ujue kwamba utafanikiwa au
hautafanikiwa. Mwendo wako au ‘life style’ yako inaweza
ikawa tochi kwako na kwa wengine kujua ni kweli utafanikiwa au utaishia kwenye
ndoto tu.
Najua umenielewa lakini naomba nikwambie kwa msisitizo kwamba, yapo maisha ambayo ukiyaishi huwezi kufanikiwa. Utahangaika sana kutafuta mafanikio na utayumba huku na huko lakini wapi utabaki pale pale ulipo.
Kwa kuwa wewe ni rafiki yangu, nataka nikupe siri, kwamba ipo namna ambayo unatakiwa uishi ili weze kufanikiwa. Yapo mambo ambayo unatakiwa uyatumie na mengine usiyatumie ili ufanikiwe maishani mwako.
Najua umenielewa lakini naomba nikwambie kwa msisitizo kwamba, yapo maisha ambayo ukiyaishi huwezi kufanikiwa. Utahangaika sana kutafuta mafanikio na utayumba huku na huko lakini wapi utabaki pale pale ulipo.
Kwa kuwa wewe ni rafiki yangu, nataka nikupe siri, kwamba ipo namna ambayo unatakiwa uishi ili weze kufanikiwa. Yapo mambo ambayo unatakiwa uyatumie na mengine usiyatumie ili ufanikiwe maishani mwako.
Leo hii kupitia somo
hili nataka nikuonyeshe mambo matatu tu, ambayo mambo hayo usipoyatumia vizuri
huwezi fanikiwa. Nimesema ni mambo matatu, sio mengi, lakini mambo haya
yanawaangusha wengi. Mambo haya ni kama haya yafuatayo:-
Muda.
Idadi kubwa ya watu ni wabovu sana katika matumizi ya muda wao. Wengi wanatumia muda wao katika vitu ambavyo badala viwape faida wanatumia muda katika vitu ambavyo viwanangusha moja kwa moja.
Idadi kubwa ya watu ni wabovu sana katika matumizi ya muda wao. Wengi wanatumia muda wao katika vitu ambavyo badala viwape faida wanatumia muda katika vitu ambavyo viwanangusha moja kwa moja.
Nitakupa mfano hapa,
moja ya matumizi mabovu kwa sasa ya muda yapo kwenye mitandao ya kijamii,
matumizi mengine ya muda mabaya yapo kwenye kufatilia habari za umbea au kuiga
hadithi zisizo na msingi wowote zinazofanana na hizi.
Unaposhindwa kuwa na
matumizi yoyote ya muda mzuri, andika umeshindwa. Historia ya dunia inaonyesha
wote wanaoutumia muda hovyo maisha yao ni ya kushindwa. Hakuna ambaye
alifanikiwa kwa kuwa na matumizi ya hovyo ya muda wake.
Ni wajibu wako kuanzia
sasa kama unataka kufanikiwa, kujijengea utaratibu wa kutumia muda wako vizuri.
Kinyume cha hapo utakuwa unatafuta balaa lako la kushindwa. kama huna cha
kufanya soma, jifunze shule ya maisha na vipo vitu vingi vya kujifunza, lakini
usipoteze muda.
Nguvu.
Mbali na matumizi ya
muda ambapo watu wengi wanatumia muda wao vibaya sana kama ambavyo tayari
tumeshasema, lakini pia wapo watu wanatumia nguvu zao vibaya. Si maanishi nguvu
nyingine, namaanisha nguvu hizi za mwili.
Wapo watu badala ya
kufanya kazi, wanatumia nguvu zao kubishana na watu hovyo au wanatumia nguvu
zao kufanya kazi zisizo za msingi ambazo zinawapotezea nguvu zao bure
ambazo zingewasaidia kuzalisha zaidi.
Unapopoteza nguvu
ambazo kiuhalisia zingekusaidia wewe kuweza kufanikiwa, unakuwa ni mtu ambaye
unajitafutia balaa lingine la kuweza kushindwa kwenye maisha yako. Unatakiwa
kuwa makini sana na nguvu zako.
Kila wakati ujue nguvu
zako zinahitajika kuweza kuzalisha kitu fulani cha manufaa. Hilo unatakiwa
uliweke akilini mwako na ujue moja kwa moja kwamba nguvu zako hazitakiwi
kupotea potea hovyo, zinahitajika kutumika kwa faida.
Uzingativu.
Pia watu wengi
wanapotezwa kwenye ramani ya mafanikio kwa sababu wanakuwa ni watu ambao hawana
uzingativu wa kutosha. Akili zinakuwa hazitulii sehemu moja, akili zao zinakuwa
zipo sehemu nyingi sana.
Utakuta mtu yupo
ofisini akili zake zote zipo nyumbani, na akiwa nyumbani tena akili zake
zinarudi ofisini. Unapokuwa unakosa au kupoteza uzingativu ujue kabisa unakuwa
unajiingiza katika hali ya kushindwa.
Unapaswa kujua kama ni
kazi unayoifanya, unatakia kuweka akili zako zote hapo. Usiyumbe na wala
kupepesa macho kwingine kwa kufanya hivyo, tambua kabisa utaweza kujenga
uwezo mkubwa wa kufanikiwa na kufikia mafanikio makubwa.
Kwa kumalizia niseme
hivi, kama kuna kitu unakifanya na unaona kabisa kinakupotezea muda, nguvu na
uzingativu, ujue kabisa kitu hicho hakiwezi kukupa mafanikio achana nacho,
kwani usipotumia mambo hayo matatu vizuri, utakwama tu.
MAKALA HII IMEANDIKWA NA IMANI
NGWANGWALU AMBAYE NI MWANDISHI WA MAKALA ZA MAFANIKIO KATIKA DIRA YA MAFANIKIO.
MAWASILIANO; +255 713 04 80 35
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.