Nov 14, 2018
Katika Maisha Acha kubweteka na Jambo Hili.
Hapo zamani za kale wakati nasoma shule ya msingi nilikuwa ni mvivu sana wa kujisomea hasa pale ninapokuwa nyumbani, baba yangu aliigundua tabia yangu hivyo alipanga kudhibiti tabia hiyo mara moja.
Aliamua kuanzisha utaratibu wa kunipa maswali ya
hesabu taribani 30 kwa kila siku , hii yote ulikuwa ni utaratibu wake ambao
aliona utanisadia kuongeza uwezo wangu wa kufanya katika somo la hesabu lakini pia ili niweze kuongeza
uwezo wangu wa kujisomea hasa pale ninapokuwa nyumbani.
Miongoni mwa vitu ambavyo huwa sivisahau mpaka leo hii
kutoka kwa baba yangu ni pamoja na adhabu alizokuwa ananipa hususani pale nilipokuwa
nakosa hesabu zile alizokuwakuwa ananipa,
hata niwe nimepata asilimia 95 nilikuwa nachapwa vibako kama mtu
aliyepata sifuri.
Yeye alikuwa hangalii hesabu nilizopata, bali yeye
alikuwa anangalia zile nilizokosa zaidi, na mara baada ya adhabu ya viboko,
baba alikuwa ananiuliza ni kwanini nimekosa zile hesabu?, mwanzoni niliona baba
ananionea kwa kunipa adhabu za viboko kwa kukosa asilimia tano pekee.
Ila kadri siku zilivyozidi kwenda nilikuja kumuuliza
baba ni kwanini alikuwa ananifanyia vile?
Baba alinimbia nilifanya vile ili kukufundisha somo
muhimu sana katika maisha ambalo halina uhusiano na hesabau zile, na somo hilo
ni la muhimu sana katika maisha yetu na somo hilo linaitwa kubweteka. Unajua katika maisha watu hufurahia zaidi
yale waliyokamilisha pekee huku wakiyasahau kabisa yale ambayo hawajayafanya au
kuyakamilisha.
Pia kitendo cha kuyafurahia yale ambayo umeyafanya na
kujiona wewe ni bora zaidi hukufanya uzidi kubweteka na kuachana na yale
unayoyakosea katika maisha, hivyo mwanangu katika maisha haya unatakiwa
kukumbuka ya kwamba yale uliyoyapanga na kuyakamilisha ni jambo jema sana, ila
kama unataka kuwa bora zaidi ya hapo ulipo sasa unatakiwa kushughulika na yale
machache yalikuwa ni vikwazo ambayo yamekufanya ushindwe kufanya vizuri zaidi.
Mara baada ya kuongea hayo nilimshukuru sana baba
yangu kwa kunipa mwangaza mpya ambao utanisadia mimi kwa namna moja ama
nyingine kuweza kupiga hatua za kimafanikio.
Hivyo ni amani yangu kubwa hata wewe ambaye unasoma
makala haya utaacha kushughulika na yale mazuri pekee unayofanya bali utaanza
kushughukika na yale ambayo ni kikwazo kwako yanayokufanya ushindwe kuwa bora
zaidi.
Mpaka kufika hapo sina la ziada naomba nikutakie siku
njema na mafanikio mema.
NDIMI: Afisa
Mipango Benson Chonya.
0757909942.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.