Nov 20, 2018
Sababu Tano (5) Kwa Nini Unaogopa Sana Kushindwa.
Kati ya kitu ambacho watu wengi sana wanakiogopa ni kule kushindwa. Ukiwauliza watu hao kwa nini wanaogopa sana kushindwa kwenye kile kitu wanachataka kufanya, sana sana watakwambia sababu moja tu kwamba wanaogopa kupata hasara.
Watu
hawa wanakuwa hawana sababu zingine makini za kwa nini wao wanaogopa kushindwa,
na hali ambayo inawasababishia wao hata washindwe kuchukua hatua. Suala la
kuogopa kushindwa lipo kwa watu wengi sana, na unaweza ukawa miongoni mwao.
Hebu
tuulizane mimi na wewe, au nikuulize je, unajua hasa kwa nini watu wanaogopa
sana kushindwa, iwe kuogopa kushindwa kwenye mradi, kwenye masomo, au kwenye usaili,
lakini woga huo upo tena kwa sehemu kubwa tu, naamini unalijua hilo.
Sina
shaka unafikiri na kujiuliza aisee ni kweli watu tunaogopa kushindwa na una
hamu ya kutaka kujua sababu zake ni zipi hasa zinazofanya watu waogope sana
kushindwa. Tulia hapo hapo, nikupe sababu yakinifu za kwa nini watu wengi wanaogopa kushindwa.
1. Ufinyu
wa mawazo.
Watu
wanaogopa kushindwa kwa sababu ya ufinyu wa mawazo au akili zao zinakuwa kama vile zimefikia ukomo. Kivipi? Mtu anakuwa
anaogopa kushindwa kwa kuamini kwamba akishindwa ndio hana nafasi tena ya kujaribu, kwa hiyo hawezi kufanikiwa
hata iweje.
Ukiwa
una mawazo haya yanayoamini nafasi pekee ya hicho ukifanyacho ni moja tu na
haitajirudia kwako tena, basi utaogopa sana kushindwa. Hutaweza kufanya
biashara kwa usahihi au chochote kwa sababu utaogopa kama ukishindwa ndio
umepoteza na kupotea.
Maisha
hayana nafasi moja kama unavyofikiri. Ukishindwa leo, kuna nafasi ya kujaribu
tena na tena mpaka utafanikiwa. Ukiondoa ufinyu wa mawazo au ‘limited mind’ ya kuamini kwamba
ukishindwa ndio basi, hutaogopa kushindwa tena, upo?
2. Kutaka
kuonekana sahihi wakati wote.
Leo kila
mtu akifikiria kufanya jambo anataka kuwa sahihi sana mbele ya watu. Anataka kufanya
jambo lake huku akiwa amekamilika kwa asilimia mia moja. Mtu huyu anasahau
kabisa kwamba hata wale anaowaona wamekamilika walianza wakiwa hawajakamilika.
Kwa mawazo
hayo ni lazima, piga ua garagaza, mtu huyu ataogopa kushindwa. Kila wakati
akitaka kufanya jambo anakuwa anajiuliza je, nikishindwa itakuwaje, si nitachekwa
na watu na nitaonekana sifai.
Kwa hiyo
hapa na kwa kifupi, kinachowapoteza watu wengi na kuogopa kushindwa ni kwa sababu
ya kutaka kuanza kwa ukamili, ukiwa sawa kila kitu. Kwa sababu hiyo kuogopa
kushindwa huwezi kukwepa hata iweje, umeidaka hiyo?
3.
Athari mbaya tulizofundishwa shuleni.
Tokea
tukiwa shule au tukiwa wadogo tumefundishwa na kukaririshwa na kwa bahati mbaya
na sisi tukameza kama kasuku na kujua kwamba kushindwa ni kitu kibaya. Hakuna ambaye
kafundishwa kushindwa ni kitu kizuri.
Ili kukuhakikishia
kushindwa ni kitu kibaya, tena tukawekewa na viboko, ukizingua tu kwa kushindwa unacharazwa bakora zako ili
kesho usishindwe. Kwa hiyo kila wakati ulikuwa ukiwaza mmh nikishindwa tu,
kimenuka.
Sasa
nikuulize, je, uliyepitia mazingira kama haya utakwepa kuogopa kushindwa? Hapa ni
lazima utaogopa kushindwa tu na utakuwa unaona kushindwa ni kosa kubwa sana. Hivyo
utafanya kila linawezekana usishindwe, kumbe ndio umepotea, umeiona hiyo?
4.
Kuhofia kuchekwa.
Eti unaogopa
kushindwa kwa sababu ya kuogopa kuchekwa, unasema daah, hivi nikishindwa watu
watasema nini, si watanicheka sana na itakuwaje. Kwa sababu hii tu, aloo,
lazima uogope kushindwa na hutaweza kuchukua hatua.
Unajua
kila mtu anataka kuonekana simba, anataka kuonekana anafanikiwa kwenye jamii,
sasa kwa mawazo hayo mtu anataka mambo yake yaonekane yamewaka hakuna kushindwa,
hapo ndipo hofu inapoanza kuzalishwa sasa.
Kwa mtu
mwenye mawazo kama hayo ya kuogopa kuchekwa, wee, utamwambia nini, badala ya
kuweka nguvu zake kwenye kuchukua hatua, yeye anakomaa na kuogopa kushindwa kwa
kile anachotaka kukifanya, hatari hiyo umeisoma eeh?
5.
Kutokujiamini.
Sababu
nyingine ya kiufundi ya kuogopa kwetu
kushindwa ni kwa sababu hatujiamini. Hauamini kwamba eti unaweza ukatoka kwenye
kushindwa hadi kufanikiwa. Haumini kama ndani yako unao uwezo mkubwa wa
kukusaidia kufanikiwa.
Kama
hujiamini kuogopa kushindwa kunakuhusu sana tu na tena sana. Kama huamini uwezo
wako, basi hiyo kwako itakuwa ni sababu ya msingi sana itakayokufanya uogope sana
kushindwa kwa chochote kile, unachotaka kukifanya.
Kwa kujifunza
sababu hizi zinakufanya uogope kushindwa naamini zimekuondolea hofu kwa kiasi,
lakini elewa hivi, huwezi kufanikiwa pasipo kushindwa, kwani kushindwa ni sehemu ya
mafanikio. Hivyo usiogope sana kushindwa, bali kushindwa huko kufanye kuwa
ngazi ya mafanikio yako. Na piga marufuku kuogopa kushindwa maishani mwako
kabisa.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa
vifaranga wa kuku aina ya KUROILER,
SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao
kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na
wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.