Nov 24, 2018
Kwa Nini Hutakiwi Kuonyesha Udhaifu Wako Kwa Wengine?
Kila mmoja wetu ana udhaifu wa aina fulani. Kwa mfano, kuna wengine wana hasira, kuna wengine wana huruma, na kuna wengine hawawezi kuficha siri. Kila mmoja ukiangalia ana udhaifu wa aina fulani, hata wewe upo udhaifu ambao unao.
Pamoja
na kila mtu ana udhaiafu wake, lakini kitaalamu unashauriwa usijaribu kuuweka
udhaifu wako huo kwa watu wengine kwa sababu, ipo siku watu hao watakaojua udhaifu
wako watautumia udhaifu huo huo kuumiza wewe.
Hata
ikitokea mtu huyu ni wa karibu sana, usimwambie udhaifu wako wewe kaa nao. Ndio
maana hata kwenye biashara wengine wanashinda na kufanikiwa kwa sababu ya kujua
udhaifu wa upande wa pili uko wapi na kuufanyia kazi.
Si kwenye
biashara tu, hata kwenye vita, au kwenye mpira, wale wanaojua udhaifu wa
wengine vizuri hao ndio wanaoshinda. Kwa hiyo kuweka udhaifu wako nje ni sawa
na kuanza kujitangazia kwamba ni lazima utashindwa katika eneo fulani la maisha
yako.
Mfano mzuri wa kuweka udhaifu wako nje, tunauona kwenye maandiko matakatifu kwenye hadithi ya Samsoni na Delila. Unaona Samsoni aliweza kukamatwa na kuteswa na adui zake mara baada ya kusema udhaifu wake kwa mkewe.
Mfano mzuri wa kuweka udhaifu wako nje, tunauona kwenye maandiko matakatifu kwenye hadithi ya Samsoni na Delila. Unaona Samsoni aliweza kukamatwa na kuteswa na adui zake mara baada ya kusema udhaifu wake kwa mkewe.
Katika mfano huo, ingawa wengi tunajua lakini unaonyesha Samsoni siri ya nguvu zake nyingi ambazo alitumia kuulia Simba na kupiga maadui zake zilikuwa kwenye nywele. Alikuwa hatakiwi kukata nywele kwa namna yoyote ile na hiyo ilikuwa ni siri kwake ambayo hakutakiwa kusema kwa mtu.
Lakini
alipoulizwa na kubembelezwa sana ataje siri ya nguvu zake na mkewe, mwisho
akajikuta akiisema, aliamua kuweka udhaifu wake nje, na matokeo yake wakati
amelala aliweza kukatwa nywele na kukosa nguvu hizo alizokuwa nazo na matokeo
mabaya yalimkuta kwa sababu ya kuonyesha udhaifu wake nje.
Unatakiwa
kujua ni kitu kibaya na hatari kwako ni kujaribu kuuweka udhaifu wako nje na
kila mtu auone. Huko ni kujitakia hatari kubwa sana ambayo inaweza kukupoteza
wewe. Kama una udhaifu wa aina fulani kaa kimya, sio lazima useme.
Kikubwa
kwako na kitu cha kufanya ni kuufanyia kazi udhaifu wako na kuhakikisha unakuwa
bora. Lakini usijaribu kuweka udhaifu wako nje hata kwa rafiki, watoto au mtu
wa karibu unayemwamini kama mkeo. Ni kosa kubwa kama kweli ukiamua kuanika
udhaifu wako.
Amini usiamini ipo siku utaumizwa tu kwa wewe kuuweka udhaifu wako nje kama utafanya hivyo. Kwa hiyo dawa pekee ya kuweza kukwepa kuumizwa huko ni kukaa kimya na udhaifu wako na si kusema kwa kila mtu.
Achana
na tabia ile ya watu utakuta anasema aah, mimi nina hasira ujue. Watu ipo siku
watatumia hasira hizo hizo kukufanyia kitu ambacho wewe hujaamini. Kitu cha
msingi hapa ni kuhakikisha unafunga mdomo wako na kuweka moyoni mwako udhaifu
wako.
Neno la
mwisho kwangu nikukumbushe, usijaribu hata siku moja kuonyesha udhaifu wako kwa
wengine, watu hao watatumia udhaifu huo kama fursa ya kuweza kukuumiza wewe. Tafakari
hili na utagundua ukweli hasa wa hiki nikisemacho.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa
vifaranga wa kuku aina ya KUROILER,
SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao
kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na
wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.