Nov 29, 2018
Kanuni Za Kujua Kusudio La Kuumbwa Kwako.
Kila
mwanadamu ameumbwa na kusudio lake hapa dunia. Pia itakuwa ni dhambi kubwa kama
upo hapa dunia pasipo kutambua hilo
kusudio lako. Watu wengi wanashindwa kufanya vizuri katika yale wayafanyayo hii
ni kwa sababu watu hao wanafanya vitu ambavyo sio vyao bali ni vya watu wengine.
Watu
wengi tunaishi kwa kuigaiga mambo ya watu wengine, yaani utakuta mtu fulani
anafanya jambo fulani kisha mtu mwingine naye anaanza kufanya jambo hilo ,
kitendo hiki ni kujipoteza wewe mwenyewe pasipo wewe kujua.
Hivyo zifuatazo ndizo kanuni za kujua
kusudio la kuumbwa kwako;-
1. Muombe mwenyezi Mungu.
Kwa
imani uliyonayo basi unashauriwa kutumia imani hiyo hiyo kuomba Mungu akujalie
ili uweze kufahamu kusudio lako uwepo wako katika sayari hii. Kwani ukweli ni
kwamba Mungu wetu ni mwema na ni muaminifu pia, hivyo tunaamini anatambua kila
mmoja wetu lengo lake ni nini hapa duniani.
2. Hakikisha unafanya kitu ambacho
unakipenda.
Miongoni
mwa mambo ambayo humsaidia mtu ili aweze kujua lengo lake na kuwepo hapa
duniani ni pamoja na kufanya mambo ambayo anayapenda.
Wengi
wetu tunashindwa kufanikiwa katika maisha hii ni kwa sababu tunafanya vitu
tusivyovipenda. Hivyo kila wakati unatakiwa kuhahakisha kila unachokifanya
unakipenda kutoka moyoni mwako.
Kama
unafanya jambo ambao hulipendi unashauri uachane na jambo hilo mara moja kwani
ni sawa na kupoteza muda tu, kwani unatakuwa unafanya ilimradi siku iendee tu.
3. Jitafute/wewe ni nani?
Unashauriwa
pia ili uweze kutambua uwezo ulionao ni pamoja na kuwekeza muda mwingi wa
kujitafuta wewe ni nani. Ninapozungumzia wewe ni nani hapa ni maana ya kwamba
ni lazima uwaze kuwa wewe upo vizuri katika kufanya jambo gani?
Mara
baada ya kupata majibu ya kwamba wewe upo vizuri katika jambo gani ndipo
unapotakiwa kuwekeza nguvu, muda, akili na pesa katika kulikeleza jambo hilo.
Kama
wewe ni mwanamitindo, mfanyabiashara, fundi au jambo lolote lile basi ni vyema
ukaweka mkazo wa kiutendaji katika mambo hayo na si vinginevyo.
Pia
ni ili uweze kujitambua wewe ni nani zinahitajika akili za ziada za kuweza
kujitambua madhaifu na uwezo ulionao katika utendaji wa jambo fulani.
Katika
madhaifu uliyonayo basi yafanyie kazi madhaifu hiyo ili weze kuondokana nayo
kabisa, ila katika uwezo ulionao basi unatakiwa kuongeza juhudi ili uweze
kufanya bora zaidi ya uwezo wako.
Hayo
ni baadhi ya ya mambo ya msingi unayopaswa kuzingatia katika kutambua kusudio
lako hapa dunia ili uweze kuishi maisha yenye furaha hatimaye kupata mafanikio
unayoyataraji.
Ndimi Afisa mipango: Benson Chonya.
bensonchonya23.gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.