Nov 27, 2018
Kipato Kikubwa Kinatengenezwa Kwa Kufuata Hatua Hizi.
Katika nyakati za sasa, wakati ambapo dunia inakwenda kwa kasi na hali ya uchumi ikibadilika sana, ipo haja ya kila mtu kuweza kujifunza namna ya kuweza kutengeneza kipato kikubwa na cha kudumu.
Hiyo iko hivyo kwa sababu, bila kufanya hivyo,
utaachwa nyuma sana kimafanikio na utajikuta ukiwa ni mtu wa pale pale, miaka
na miaka. Una anzaje kujitengenezea kipato kikubwa wakati pengine mtaji wako ni
mdogo?
1. Anza na kidogo.
Katika harakati za kutengeneza kipato cha
kikubwa na cha kudumu ni vyema ukajifunza kuanza na kidogo. Anzia pale ulipo
ili kutafuta mafanikio yako. Chochote ambacho unaona kinakufaa kifanye, hata
bila kuona haya.
Watu waliofanikiwa si kwamba walianza na mambo
makubwa sana, hapana. Mara nyingi ni watu waliomua kukubali kukaa chini na
kuanza na kidogo kile walichonacho ili kufikia mafanikio yao.
Ni jukumu hilo hilo ambalo unaweza hata wewe
ukalichukua na kuanza na kidogo ulichonacho. Acha kusubiri sana mpaka kila kitu
kikamilike ndio uanze kufanya. Ukifanya hivyo, yaani kuendelea kusubiri utakuwa
unajichelewesha mwenyewe kufanikiwa.
2. Jenga fikra chanya.
Hautaweza kutengeneza kipato kikubwa na
kufanikiwa kama kila wakati fikra zako zipo hasi, hasa linapokuja suala
linalohusiana na mambo ya fedha. Ni lazima fikra zako ziwe chanya na kuamini
kwamba una uwezo wa kutengeneza pesa.
Acha kuendelea kung’ang’ania fikra mgando
ambazo hata hazikusadii kitu, zaidi zinakukwamisha sana kufanikiwa. Watu
waliofanikiwa kipesa na kutengeneza pesa nyingi, kila wakati huamini sana wao
ni watu wa pesa.
Kwa kuamini kila siku na kuendelea kufanyia
kazi yale wanayoyafanya bila kuchoka hujikuta wakiwa na pesa nyingi sana katika
maisha yao. Kama leo hii unataka kutengeneza kipato kikubwa, jenga fikra chanya
juu ya pesa na utafanikiwa.
3. Weka mipango imara.
Silaha pekee ya kuweza kufanikisha kujenga
kipato kikubwa na cha uhakika ni kwa wewe kuhakikisha unakuwa na mipango ya
kutengeneza kipato hicho. Ni muhimu sana kujiwekea mipango imara ili ikusaidie
kutimiza lengo lako.
Kwa mfano, unaweza ukaweka mipango ya kuwekeza
vitega uchumi vya aina tofauti tofauti ambavyo vitakusaidia katika kutengeneza
kipato kikubwa. Ukishaweka mipango hiyo unaiweka kwenye utekelezaji.
Watu wenye mafanikio makubwa ndvyo ambavyo
hujiwekea mipango yao kwa staili hiyo karibu kila siku. Lakini hawaishii kuweka
mipango hiyo bali huchukua jukumu la kuifatilia kial siku. Hicho ndicho kitu
unachotakiwa kukifanya ili ufanikiwe pia.
4. Kuwa mvumilivu.
Kila mafanikio yanahitaji uvumulivu wa aina
fulani ili uweze kuyapata. Hakuna mafaniko ambayo unaweza eti ukayapata bila
kuvumilia. Kipo kipindi ambacho kwa vyovyote vile ni lazima usibiri.
Hivyo wakati umejiwekea mipango na mikakati
yako ya kukuwezesha kufanikiwa, tambua unatakiwa kuwa mpole kwa kukaa chini na
kusubiri mchakato wa mafanikio yako kuwezekana.
Kila mtu aliye na mafanikio leo hii ukimuuliza
ni lazima atakwamba alivumilia kwa namna fulani hivi na hakuyapata mafanikio
hayo mara moja. Ili nawe uweze kujenga kipato kikubwa unahitaji uvumilivu wa kutosha.
Jipe muda wa kuvumilia.
Kitu unachotakiwa ukijue mapema ili uweze
kutengeneza kipato kikubwa ni kwamba, kipato hicho huwa hakitengenezwi kwa
bahati mbaya. Mara nyingi huwa ipo misingi au hatua unazotakiwa uzifuate
kama ambavyo tulivyojadili kujadili.
Kumbuka zaidi ili uweze kutengeneza kipato
kikubwa, unahitaji kuanza na kidogo, kujenga fikra chanya juu ya pesa, kuweka
mipango imara na wewe kuwa mvumilivu. Ukiweza kuzingata mambo hayo. Hilo halina
shaka, tayari utakuwa na uhakika wa kutengeneza kipato kikubwa.
Endelea kutembelea
dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.