Nov 16, 2018
Sababu Tano (5) Kwa Nini Biashara Yako Inapoteza Sana Wateja.
Utake au usitake, upo uwezekano mkubwa sana wa biashara yako inapoteza sana wateja. Umeshawahi kujiuliza kwa nini au wewe ndio wale wale umebaki na sababu zile zile kwamba ‘usawa huu ni mgumu, na mambo hayaendi kabisa?’
Ikiwa
umekuwa na wewe unatoa sababu kama hizo, nikwambie tu, hapo unajidanganya wewe
mwenyewe. Sababu kubwa ya biashara yako kukosa wateja, chanzo kikubwa ni wewe
na si mtu mwingine au hali yoyote ile nje na wewe.
Naona
unanishangaa kivipi, na mbona mambo yangu yalikuwa mazuri siku za nyuma na kwa
biashara hihii, iweje mimi ndio niwe chanzo leo? Nisikilize vizuri, wewe ni chanzo cha biashara yako kukosa wateja,
kivipi, ngoja nikupe sababu;-
1. Una huduma mbovu kwa wateja wako.
Huwezi
kukwepa kukosa wateja kama una huduma mbovu kwa wateja wako. Unaweza usiwe
wewe, hapa wanaweza wakawa ni wasaidizi au wafanyakazi wako ndio wanaokuharibia pasipo wewe kujua kitu
chochote na ukaona uko sawa.
Wengi
kwa kushindwa kujua kwamba wanahuduma mbovu ndio wanajikuta ni chanzo cha
kuanza kupoteza wateja wengi tena bila kujua. Huduma yako mbovu inaweza ikawa
kwenye bidhaa au mazingira au hata jinsi
ya kuwahudumia wateja na wakaridhika.
Nini kifanyike?
Hapa
kuwa makini sana na mazingira yote yanayoweza kupelekea huduma mbovu ikatolewa,
kama wafanyakzi wako, mazingira na bidhaa unazozitoa. Vitu hivyo unatakiwa
kuvihakiki mara kwa mara ili visiwe chanzo cha huduma ya hovyo kwako na
kupelekea kukosa wateja.
2.
Bidhaa zako zimeshindwa kukidhi matakwa ya wateja.
Inapotokea
bidhaa zako zimeshindwa kukidhi matakwa
ya wateja wako, hapa unakuwa unawakatisha tamaa wateja wako. Wale wateja wako wanakuwa
hawana hamu na wewe na pia hawana hamu hata na biashara yako, hivyo ‘automatic’ unakosa wateja.
Hakuna
mteja ambae atakuwa na furaha ya kununua bidhaa zako ambazo hazijaweza
kumsaidia. Mteja hyu ni lazima ataachana na wewe na kwenda kutafuta huduma
ambayo inamsaidia hata iwe kwa gharama kubwa, ataifata tu popote.
Nini kifanyake?
Unatakiwa
kutengeneza au kutoa bidhaa bora sasa. Ili hili lifanikiwe unatakiwa kufanya
kazi na watu ambao ni wataalamu kwa hilo. Pia si hivyo tu jaribu bidhaa zako
hizo kabla haijawafikia wateja wako na kujiridhisha je, zinafaa au hazifai?
3.
Hauonyeshi thamani kwa wateja kikamilifu.
Kinachowafanya
wateja wanunue huduma au bidhaa zako ni thamani wanayopewa na wewe. Pia kitu
kingine kinawachowafanya wateja wanunue ni kwa sababu unauza kwa bei ndogo bali
ni ile thamani kubwa wanayopewa, hivi ni vitu vya msingi sana.
Kama
utajua jinsi ya kutoa thamani sahihi na inayoendana sawa sawa na mteja wako
utafanikiwa, kama ni suala la bei mbona kila mtu anaweza kupunguza bei, ila si
kila mtu anaweza kutoa thamani sahihi itakayombakisha mteja kwa miaka mingi.
Nini cha kufanya?
Hakikisha
unatoa thamani iliyo kamili kwa wateja wako. Wewe pamoja na ‘timu’ yako unatakiwa kufanya kazi sana
ili kuweza kuwalinda wateja kwa kuwapa thamani sahihi. Ukumbuke thamani kwenye
biashara ndio chanzo cha mafanikio makubwa.
4.
Biashara yako ina mwendelezo mbovu.
Katika
biashara na katika maisha kwa ujumla, kufanya kitu kwa mwendelezo/consistent pasipo
kusimama na kwa muda mrefu, kunaleta kuaminiwa sana. Huwezi kufanikiwa katika
biashara kama leo hii umeifungua na kesho umeifunga au unafanya unavyotaka kisa
ni biashara yako.
Watu
wanaodumu katika biashara na wanaofanikiwa katika maisha, ni watu ambao wanafanya
vitu vyao kwa mwendelezo na kwa muda
mrefu. Utakuta mtu anafanya jambo la aina fulani kwa muda mrefu, lakini
mafanikio anakuja kuyaona baadae.
Nini kifanyike?
Jenga
nidhamu au utaratibu wa kufanya biashara yako kwa mwendelezo sahihi, pasipo
kujali kuna wakati unakutana na changamoto au la. Wewe kazana kuweka juhudi
kila siku kwa kufanya kitu kilekile hata kama hakitakupa matokeo leo makubwa
lakini kifanye.
5.
Mbinu zako za kimauzo zimepitwa na wakati.
Inapotokea
mbinu zako za kimauzo zimepitwa na wakati huwezi kuendelea kuwapata wateja
wengi. Hapa ndipo maana kampuni kubwa zikaja na kitengo cha huduma kwa wateja
ili kila siku kuweza kumudu kuboresha huduma ili kuleta mafanikio.
Kama
kila wakati utaendelea kuwa na mbinu zile zile za kimauzo pasipo kuzibadilisha
na kutegemea muujiza utakaokupa wateja wengi, naomba nikwambie kwenye hilo
jambo lisahau kabisa. Ni muhimu ukabadilika kwanza wewe na wasaidizi wako.
Nini kifanyike?
Kila
mara pata mafunzo ya jinsi ya kuboresha huduma kwa wateja na unaweza kuyapata
kupitia semina au warsha mbalimbali za kibiashara. Pia jenga urafiki na wateja ili wakusaidie
kupata wateja wengine zaidi na zaidi ili kufikia mafanikio.
Kwa kumalizia
niseme hivi, unapoona biashara yako inakosa wateja, ukumbuke huo sio uchawi au
bahati mbaya. Unatakiwa kutambua kwa uwazi kabisa kwamba zipo sababu kama hizo
na wengi wanakuwa hawazijui.
Ninaamini
kwa kuzijua sababu hizo leo, basi utazifanyia kazi na kuamka kwenda
kuisimamisha biashara yako kwa kishindo kikubwa.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa
vifaranga wa kuku aina ya KUROILER,
SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao
kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na
wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.