Feb 9, 2018
Chanzo Cha Kutoelewana Kwingi Kinasababishwa Na Jambo Hili.
Upo muda
iwe kazini au katika maisha yetu ya kawaida, kunakuwa na kutokuelewana
sana kati yako wewe na wale wanaokuzunguka. Kwa mfano, unakuta maelewano yanakuwa
sio mazuri sana na kunakuwa na kupishana kwingi.
Umeshawahi
kujiuliza nini huwa chanzo cha kutokuelewana vizuri, iwe kwenye familia, kazini
au eneo lingine la maisha yetu hali ambayo husababisha migogoro sana. Kwa jinsi
ilivyo chanzo kingi cha kutoelewana husababishwa na jambo moja tu, ambalo ni
kutokuwaelewa wengine vizuri.
Moja
ya kitu cha muhimu sana ambacho unatakiwa kuwa nacho kwenye maisha yako ni kuwa
na uwezo wa kuwaelewa watu wengine pia ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima. Hiyo yote ni kwa sababu tumeumbwa watu tukiwa wa tofauti, hivyo ni lazima uwaelewe
watu wengine.
Ni
muhimu kujua wewe ni wa tofauti huwezi kufanana na mwingine kwa mambo mengi.
Kwa hiyo swala la kuendana na watu wengine jinsi walivyo hutakiwi kupuuza hata
kidogo ndio maana tunasema ni muhimu sana kuwaelewa wengine vizuri.
Unapowaelewa
watu wengine vizuri kabla hujaanza nao kufanya kazi yoyote, inakusaidia sana
kukuondolewa wewe msongo wa mawazo na inaondoa kwako migongano ambayo
ungekutana nayo bila sababu yoyote.
Jaribu
kujiuliza ni mara ngapi umepatwa na hasira kwasababu ya jambo ambalo umekuja
kugundua kwamba alaa kumbe ilikuwa ni kitu tu cha kutokuelewana. Unapokuja
kugundua hivyo unakuwa tayari umepoteza nguvu na muda wako sana.
Inahitaji
utulivu kidogo ili kuweza kuwaelewa wengine wanataka nini na wewe unataka nini
ili mweze kwenda pamoja. Ikiwa itakuwa kinyume ya hapo utaanzisha mgogoro ambao
hukutakiwa kuanzisha, lakini kisa ni maelewano mabovu.
Unatakiwa
kujua ni rahisi tu kugombana na kila mtu ikiwa huwezi kuwaelewa watu vizuri. Uwe
na uhakika utagombana na familia yako, utagombana na wenzako kazini na marafiki
zako kwa sababu ya kushindwa kuleta maelewanao kati yenu ambayo yalikuwa ni
rahisi kueleweka.
Kila
siku ipo nafasi ya wewe kuweza kujenga uelewa wako kwa wanao kuzunguka. Unakuwa
na nafasi ya kujenga maelewano na watu wanaokuzunguka hiyo ni faida kubwa sana
kwako ya kudumisha mahusiano.
Unapokuwa
unaelewa kujenga mahusiano mazuri, elewa haufaidiki wewe tu, hata wanao
kuzunguka nao wananaanza kufaidika kwa kulewana kwa ufasaha ambako inakuwa
tayari wewe kumekujenga na kukudumisha.
Kuanzia
leo usikubali uwe chanzo cha mgogoro kwa sababu tu ya kutoelewana. Jenga maelewano
mazuri sana karibu katika kila eneo na hiyo itakusadia sana kuweza kuweza
kujenga mahusino mazuri na yatakayokupa pia mafaniko kwenye maisha yako.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686
141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.