Feb 23, 2018
Huu Ndio ‘Ugonjwa’ Mpya Hatari Usipothibitiwa Mapema, Utaangamiza Familia Nyingi.
Inafahamika yapo magonjwa mengi sana, ambayo yamekuwa tishio kwa familia na jamii inayotuzunguka kwa muda mrefu. Magonjwa hayo yapo ambayo yamekuwa yana dawa na yapo ambayo hayana dawa, lakini yapo.
Kwa
kuwa mimi si daktari hapa katika makala haya sitataja sehemu ya magonjwa hayo
ambayo yamekuwa ni hatari kwa familia, pengine na taifa kwa ujumla, bali hapa
mimi nitazungumzia ugonjwa mmoja tu ambao naufahamu ila ni hatari sana.
Ugonjwa
huu ambao nauzungumzia hapa na ambao ikiwa hauathibitiwa mapema, basi tujiandae
kupoteza familia nyingi na kuzipeleka kubaya zaidi, ni ugonjwa wa mmonyoko wa maadili,
ndio nimesema ni mmonyoko wa maadili.
Kwa
miaka ya hivi karibuni ukifatilia kwa makini, utagundua swala la kuporomoka kwa
maadili kadri siku zinavyokwenda mbele nalo limekuwa likiongezeka kwa kasi.
Watoto wa sasa, wamekuwa si watoto wa
miaka ile, mambo yamekuwa yametofautina sana.
Malezi bora kwa watoto yanatakiwa kusimamiwa vizuri. |
Hilo
unaweza ukaliona vizuri kwa watoto wa sasa, kama si wa kwako basi wa jirani na
kama si wajirani basi ni wa ndugu. Lakini kitu ambacho kipo na kinaendelea
kutokea katika jamii zetu tunamoishi kila siku.
Najua
walezi wa watoto kama wazazi, walimu pia ambao kwa sehemu wanajukumu la kukaa
na watoto kwa muda mrefu, hapa wanaweza wakawa wananielewa kwa uzuri sana kwamba
mmomonyoko wa maadili tayari limekuwa ni tatizo au ugonjwa ambao unakuja kimya
kimya.
Kwa
bahati mbaya sana kila mtu anakazana na kinga ya nyumbani kwake na wengine hata
hiyo kinga hawaijui, matokeo yake watoto wanakuwa wanalelewa tu kama kibahati, na
mwisho wa siku ni hatari kubwa ambayo inapelekea mmonyoko wa ukweli.
Kiuhalisia
ukiangalia yapo mengi yanayosababisha ‘ugongwa’ huu wa mmonyoko wa maadili kwa
sasa kutokea kwa kasi kuliko wakati mwingine. Moja ya msingi mbovu inaweza
ikawa ni malezi mabovu ya wazazi na walezi kwa watoto na hata pia mitandao ya
kijamii.
Hivi
ni vitu ambavyo vinaweza vikawa na mchango mkubwa sana kupelekea mmonyoko wa
maadili kwa watoto wetu. Na pasipo vitu hivi au swala hili la mmomonyoko wa
maadili kudhibitiwa basi taifa la kesho tutakalokuwa nalo litakuwa ni bovu sana.
Unaona
mpaka hapo ni jukumu la kila mmoja wetu kusimamia kwa umakini swala la mmonyoko
wa maadili kutokuendelea, vinginevyo tutakuwa na taifa ambalo litakuwa halina maadili
kwa siku za huko baadae.
Ni
imani na mategemeo yangu wazazi na walezi watajitahidi kuziba mianya yote inayopekeleka
mmonyoko wa maadili. Hayo yote hayawezi kufanikiwa pasipo kutoa ushirikiano kwa
wazazi wote.
Pia
walimu wetu inatakiwa washirikishwe na watiwe moyo na wazazi katika kuhakikisha
watoto wanalelewa katika maadili mazuri na bora. Kila mtu akisimama katika
nafasi yake mabadiliko yatawezea kutokea.
Lakini
ikiwa tukishindwa kuthibiti kwa sasa mmomonyoko wa maadili, basi tujiandae kuwa
na kizazi ambacho kitakuwa kipo kipo tu.
Mpaka hapo ieleweke hatujachalewa, uwezo wa kuthibiti ‘ugonjwa’ huu wa mmonyoko wa maadili inawezekana.
Inawezekana
unajiuliza tunaanzia wapi, anzia hapo ulipo, ‘mtoto wa mazazi mwezio ni mtoto wako pia.’ Kama unaona mtoto
amekosea kitu hata kama sio wako, chukua jukumu la kumuonya.
Pale
mtoto atakapogundua alaa kumbe anaweza kuonywa na mzazi ambaye si wake, najua
atajirekebisha na vivyo hivyo tutajikuta tuna kizazi chema, kizazi ambacho
tutakifurahia siku za usoni kwenye maisha yetu.
Watengenezaji
wa maisha ya watoto wetu ni sisi wenyewe, jukumu ni letu sote. Tuchuke hatua za
kuweza kubadili sisi kwa kuwa wazazi au wazazi wawajibikaji na kwa kufanya hivyo
tutaweza kuthibi ‘ugonjwa’ huu wa
mmonyoko wa maadili.
Fanyia
kazi ujumbe huu, linda kizazi cha kesho kwa kukipa maadili bora na ya manufaa
leo na si kesho.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
MUHIMU ZAIDI; kama
unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana,
ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686
141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.