Feb 21, 2018
Huu Ndio Ukweli Kuhusu Maisha Ya Mafanikio Unaotakiwa Kuufahamu Vizuri.
IIi
kufikia mafanikio, kuna wakati inatakiwa uujue ukweli wa aina fulani hivi na
kwa kuujua ukweli huo utakusaidia kufanikiwa. Lakini kuendelea kuishi kwa
kujidanganya na huku ukiwa hujui mbele wala nyuma juu mafaniko utajidangaya tu,
hutafanikiwa.
Najua
utaweka juhudi hii au ile kufikia mafanikio, lakini hutaweza kufikia kwa sababu
utakuwa bado unaishi kwenye dunia ya giza ambayo inakuwa imekufunika na
ushindwe kutafuta mafanikio yako kama inavyotakiwa iwe kwako.
Kupitia
makala hii ya leo, tunakuangazia kweli tano ambazo unatakiwa uzijue na ili zikusaidie
kufanikiwa. Ni matumaini yangu, utafaidika vya kutosha na kuweza kubadilisha
maisha yako kwa kufanyia kazi kweli hizi. Kweli hizi ni zipi, karibu ujifunze.
1. Ni kazi ngumu kufikia mafanikio.
Asije
akakudanganya mtu kwamba kufikia mafanikio ni kazi rahisi, huyo atakuwa ni mtu
mwongo kabisa. kufikia mafanikio inahitaji uweke juhudi na maarifa ya kutosha
ili kufikia mafanikio hayo. Kama huweki juhudi huwezi kufanikiwa.
Kwa
lugha nyepesi tu bila kukuficha kitu naomba nikwambie kufikia mafanikio ni kazi
ngumu na sio nyepesi kama wengine wanavyowezza wakawa labda wanakudanganya
kwamba ni kitu rahisi tu na cha mara moja.
Lakini
hata hivyo haimaanishi kwa kuwa ni kazi ngumu kufika mafanikio, basi
haiwezekeni kuyafikia. Kufikia mafanikio ni kweli ni kazi ngumu, lakini
inawezekana kuyafikia kwa asilimia zote na hilo halina ubishi. Huu ni ukweli
unaotakiwa uumeze kama ulivyo bila kutema.
2. Unahitaji msaada kufikia mafanikio.
Hakuna
mafanikio ambayo unaweza ukayapata ukiwa wewe kama wewe. Unahitai msaada ili kuweza
kufikia mafanikio yako. Pasipo kuweza kupata msaada huwezi kupata mafanikio
yoyote, kwani mafanikio yapo kwa watu.
Kwa
hiyo utaona unahitaji msaada kutoka kwa rafiki zako, utahitaji msaada kutoka
kwa ndugu zako wa karibu na hata pia utahitaji msaada kutoka kwa wale watu wanaokusaidia
kazi zako na ambao wanakuwa wana mchango fulani kwako.
Huhitaji
hapa kutunisha kifua kusema mimi ndio mimi, mafanikio ni muunganiko wa misaada
tofauti tofauti kutoka kwa watu wengine pia. Ukweli huu unatakiwa kuujua kwamba
mafaniko yanahitaji msaada wa wengine pia, hivyo heshimu watu.
3. Makosa ni ngazi ya kufikia mafanikio.
Imezoeleka
kati ya kitu kinachowaangusha wengi katika safari ya mafanikio ni yale makosa
ambayo wanakuwa wanayafanya wakati wanatafuta mafanikio yao. Watu hao wamekuwa
wakisahau kwamba makosa ni kama shule.
Unapokuwa
unatafuta mafanikio ya aina fulani, kukosea ni kitu cha kawaida sana. Kwa hiyo
hutakiwi kujilaumu kwa chochote kwamba kwa nini umekosea katika eneo la aina
fulani, badala yake unatakiwa ujifunze kusonga mbele.
Utakwama
sana kwenye maisha yako, kama makosa utakuwa unayachukulia kwa umakini sana na inakupelekea mpaka kushindwa
kufanya vitu vingine. Yafanye makosa yawe shule yako ya kukuwezesha wewe kuweza
kusonga mbele zaidi na si kukurudisha nyuma.
4. Kuwa king’ang’anizi.
Sifa
mojawapo kubwa ya watu ambao wamefanikiwa ni wabishi. Ni watu ambao hawakubali
kushindwa kirahisi, ni watu ambao wanaamua liwalo na liwe, lakini wanapigana
mpaka kuhakikisha ndoto zao zinaweza kutimia.
Hata
wewe ili uweze kufanikiwa unatakiwa uwe king’ang’anizi sana. Kwa kifupi
unatakiwa uwe na roho ngumu, roho ambayo haikubali kushindwa kirahisi, inayotaka
lazima mabadiliko yaweze kutokea kwenye maisha yako.
Ukiujua
vyema ukweli huu kwamba unatakiwa kuwa mbishi hilo litakusaidia sana kuweza
kuweza kung’ang’ana kufanya kila linalowezekana na kuongeza juhudi zote kwa
kufanya kila kilicho cha msingi, ilimradi tu ufanikiwe.
5. Jipe hamasa ya mafanikio kila siku.
Usifanye
kosa la kusubiri hali au kitu chochote kikupe hamasa ya kufanya kile unachotaka
kufanya. Jipe hamasa hiyo wewe mwenyewe kila siku. Kama huoni hamasa ikitokea
usitulie, wewe endelea kufanya, hamasa itakuja mbele ya safari wakati
unaendelea.
Washindi
katika mafanikio hawasubiri hamasa ili kuweza kusonga mbele. Ni watu wa kufanya
na mwisho wa siku hamasa inayofuata. Kwa hiyo hata wewe unaweza ukaanza kujihamasisha
wewe mwenyewe.
Hakikisha
unafanyia kazi kweli hizi muhimu kwako na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako
zinatumia.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
MUHIMU ZAIDI; kama
unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana,
ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097
na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.