Feb 2, 2018
Hakikisha Kitu Hiki Kisikuzuie Kabisa Kufikia Mafanikio Yako.
Haijalishi
kwenye safari yako ya mafanikio unakutana na ugumu wa aina gani, lakini
unachopaswa kuelewa ugumu huo unaokutana nao ni ugumu wa muda mfupi sana kwako
na wala hauhitaji wewe kukata tamaa.
Uelewe
hivi, pamoja na kwamba unakutana na ugumu ili hali unaweka juhudi za kutosha,
unapaswa kuvumulia na kuendelea kuweka juhudi tena kwani matunda ya mafanikio
utakayoyapata yatakuwa ni ya muda mrefu kwako.
Ni
rahisi kufikiri au kuamua kuachana na ndoto zako na kutoa sababu mbalimbali kwa
sababu ya ugumu ambao unakutatana nao kimaisha. Hayo yote hayawezi kukusaidia
unachotakiwa kujua ugumu huo ni wa muda na wewe unatakiwa kupambana.
Kesho
yako unatakiwa kuitengeneza wewe kwa kufanya kila linalowezekana hadi kuweza
kufanikiwa. Kutoa sababu kwa sababu mambo ni magumu hilo sio suluhisho hata
kidogo, unatakiwa kukazana tu bila kujali nini kinakutokea.
Labda
nikulize kitu? Ni kipi unachokipenda upate mateso ya muda halafu baadaye uje
ufurahie maisha yako kwa muda mrefu au upate starehe za muda na baadaye uje
uteseke. Naamini utachagua bora ya mateso ya muda mfupi.
Kama
iko hivyo na kwako, hutakiwi sasa kukatishwa tamaa na hali unayokutana nayo.
Ugumu wa maisha usikuchanganye hata kidogo. Kila mtu aliyeko duniani amekutana
na ugumu wa maisha kwa wakati wake yeye, hakuna ambaye hajakutana na ugumu.
Wafatilie
watu wote wenye mafanikio, utajua ni watu ambao wamekutana sana na ugumu wa
maisha. Kile unachokiona kwa nje ni picha tu za mafanikio unayoyaona kwa nje,
lakini ndani mwao wamekutana na magumu mengi sana.
Najua
hawawezi kukwambia jinsi ilivyo, lakini ukweli uko hivyo. Ndio maana tunasema, unatakiwa ukabiliane sana na ugumu wa kila aina yoyote ile hadi uweze
kufanikiwa, kwani hali hiyo ni ya muda tu, nayo itapita.
Uwe
unalala chini, uwe unakula mlo mmoja kwa siku, uwe huna pesa kabisa, yote hayo
ipo siku yataisha ikiwa utakuwa ni mtu wa kuishi kwa malengo na kuchukua hatua
za kubadilisha maisha yako hatua kwa hatua.
Inawezekana
pia njia unayopita sasa hivi inakuchanganya kwa sababu ya taabu zake nyingi na
imekuwa kama njia ya miiba na kuona mbele tumaini limekufa. Unatakiwa kujiambia
mafanikio ni lazima hata kitokee kitu gani.
Maisha
ya mafanikio hayaji mara moja, ni matokeo ya mabadiliko ya hatua kwa hatua hadi
kufikia mafanikio. Kipi kinakushinda na kwa nini una wasiwasi, kwa nini uumie
na ugumu wa maisha ulionao, kila kitu kinabadilika ukiamua.
Unachopaswa
kufanya ni kuchukua hatua za haraka kila wakati. Hutakiwi kusita sita, chochote
unachotaka kukifanya, kifanye. Acha kudharau kitu, chukua hatua za kufanya na
hapo ndio utakuwa unabadilisha maisha yako.
Kabla
siku hii ya leo haijakwisha unatakiwa kuelewa kukubali kukabiliana na
changamoto, weka juhudi, pambana na ugumu wa maisha na itafika wakati ugumu huo
utakwisha na utakuwa na maisha bora kwako.
Kwa
jinsi utakavyokuwa ukiweka juhudi kukabiliana na hali uliyonayo, ndivyo
utakavyokuwa ukibadilisha maisha yako na kuyafanya kuwa bora. Usikate tamaa,
ugumu wa maisha usikuzuie kabisa kufikia mafanikio yako.
Hakuna
kitu au hali yoyote ambayo inakuzuia kufanikiwa hata kama hali hiyo kwako ni
ngumu kwako. Kila changamoto kwenye maisha ni ya muda tu. Ni wakati wa kuamua
kusonga mbele na siku zote usiruhusu
ugumu wa maisha ukakuzuia kufanikiwa.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686
141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.