Feb 16, 2018
Ijue Misingi Hii Ya Fedha, Maisha Na Mafanikio Inavyofanya Kazi.
Hakuna unachoweza kusema unakipata
kwenye maisha yako kwa kubahatisha. Kila kitu unachopata kwenye maisha yako ni
matokeo ya msingi ambao unakuwa umejiwekea. kama umejiwekea misingi mibovu, ujue utapata matokeo mabovu pia.
Ni matumaini yangu wewe uweze kujifunza misingi sahihi ya mafanikio yako ili uweze kufanikiwa. Ni misingi hii sahihi ya fedha, maisha na mafanikio, ndiyo ambayo mimi
na wewe nataka tuifatilie kwenye somo hili na kujifunza jinsi ya kuifanyia kazi
kila siku.
1. Kipato
unachokipata si sawa na utajiri. Sio kile unachokipata ndio kinakufanya uweTAJIRI bali kile unachowekeza ndicho
kinachokufanya uwe tajiri. Kosa kubwa wanalofanya wengi ni kuweka akiba na
kuitumia kwenye mambo ambayo hayana uwezo wa kuwasaidia KUFANIKIWA.
2. Utafiti
unaonyesha ni asilimia mbili tu ya wazee wanaofikisha miaka 65 ni hao ndio
wanakuwa wako huru kifedha. Asilimia kubwa inayobaki wanabaki wakiwa na maisha
magumu sana na ya kuteseka. Hutakiwi kuwa miongoni mwa kundi la watakaoteseka, badilika sana na kuanza kuwekeza.
3.
Utajiri haujengwi kwa siku, utajiri unajengwa kwa idadi ya miaka. Unatakiwa
kuwa mtulivu sana hasa pale unapoamua kujenga utajiri wako na hutakiwi kuwa na
papara, tulia, weka mipango na utafanikiwa. Ila kama utautaka utajiri wa siku moja tu, ni ngumu sana kufanikiwa, unatakiwa kuwa na mipango ya muda mrefu.
4.
Uchaguzi unao wewe kwenye maisha, kupanda na kusubiri mavuno au kuwa omba omba
katika kile kipindi cha mavuno ambapo tayari kuna watu walipanda wakati wa
nyuma.
5.
Unachotakiwa kujiuliza, je, ukipewa nafasi ya kuishi miaka 90, utakuwa na pesa
za kukuwezesha kuishi miaka hiyo au utategemea msaada kwa watoto wako na watu
wengine, tafakari hilo kama utaona hutajiweza, kisha weka utani pembeni na
ongeza juhudi sana za kutafuta pesa.
6.
Moja kati ya kitu cha kushitua sana katika maisha ya siku hizi, kila mtu
ukimuuliza kwamba ana mkopo sehemu, idadi kubwa sana watasema ndiyo. Utafikiri
swali hilo umeuliza nani ni binadamu. Usijenge tabia sana ya kuazima pesa,
jenga tabia ya kuazima watu pesa na si kuazima.
7.
Haina haja ya kulalamika sana, unatakiwa ujifunze kwa bidii na hadi ukaelewa
namna ya kuongeza pesa ulizonazo zikawa hata mara tano. Huhitaji wewe mshahara
mkubwa. unachohitaji ni juu ya kujua jinsi unavyoweza kuongeza pesa ulizonazo
na ukafanikiwa kwa asilimia kubwa.
8.
Ikiwa leo maisha yako ya uzeeni yataishia kwenye umaskini, sio swala la
kumlaumu Mungu. Unatakiwa kujilaumu wewe kwa kushindwa kwako kufanya uchaguzi
sahihi wa kupanda katika kipindi cha kupanda na kuvuna katika kipindi cha
mavuno na si kuwa ombaomba.
9.
Mkakati wa kuwekeza kwa muda mrefu unatakiwa uwe na mambo haya yafuatayo:-
Moja, wekeza kila mwezi, kwa muda usiopungua
miaka 20 kutokana na kipato unachokipata bila kujali kipato hicho ni kidogo
kiasi gani.
Mbili,
wekeza kila mwezi bila kujali, huo mwezi ni una Tsunami, una maafa au mwezi una
mafuriko ya kiasi gani. Ila unachotakiwa kufanya ni kuwekeza angalau kila mwezi
kwa kile unachokipata, hakuna haja ya kutoa sababu au kisingizio chochote.
10.
Ukitaka kujenga utajiri wako na ukafika mbali kweli, amua kuujenga utajiri wako
kama kobe. Chukulia kama hizo ni mbio za muda mrefu, usikurupuke kujenga
utajiri wako utakwama sana.
Fanyia
kazi misingi hii na chukua hatua
kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686
141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.