Feb 14, 2018
Ukishindwa Kuzingatia Mambo Haya Mawili Tu, Utakwama.
Kila
mtu anapanda kwenye ngazi ya mafanikio yake. Kila mtu anakimbilia ngazi ya mafanikio
yake, pasipo kujali ni kitu gani ambacho anakifanya, lakini kila mtu yupo kwenye
ngazi ya kuelekea kwenye mafanikio yake kwa namna fulani hivi.
Tatizo
la watu wengi wanapokuwa wanapanda ngazi ya mafanikio yao, badala ya kwenda juu
wanakua ni watu ambao wanapanda ngazi hiyo kwa kushuka chini. Unaweza usinielewe
kiurahisi, lakini ndivyo watu wanavyofanya hivyo.
Yapo
mambo ambayo kwa kawaida huwa yanachangia katika watu hao badala ya kupanda
ngazi ya mafanikio kwa kwenda juu na wao wanakwenda chini. Mambo haya naweza
yakawa yanafahamika kwa wengi au yasifahamike kwa namna yoyote ile.
Lakini
jambo mojawapo ambalo linaweza likafanya mtu badala ya kupanda ngazi yake ya
mafanikio na hadi kuweza kufanikiwa, anajikuta anarudi nyuma hio yote ni kutokana na matumizi ya muda wake.
Muda unaoutumia unautumia vipi.
Ni
watu wengi sana ambao matumizi ya muda wao hayajakaa sawa. Mara nyingi sana
watu hawa hawafanyi vitu vya kuwasaidia kulingana na muda wao walionao. Ni watu
wa kufanya sana vitu vinavyowakwamisha na kuwarudisha nyuma kimafanikio.
Ni
hatari sana na ni ngumu kuweza kupanda ngazi ya mafanikio na kuweza kufanikiwa
kama matumizi yako ya muda unayatumia kwa vitu ambavyo si sahihi yaani vitu
vinavyoukwamisha na kukurudisha nyuma.
Kuutumia
muda wako hivyo hiyo ni sawa na kuamua kurudisha mafanikio yako kwa kurudi
nyuma. Unaweza ukawa unaona unapanda ngazi ya mafanikio yako vizuri, kumbe
unaigiza yaani unarudi nyuma kimafanikio.
Unatakiwa
ujue namna ya kutumia muda wako vizuri sana ili uweze kupanda ngazi yako ya
mafanikio kwa ufasaha na kuweza kufanikiwa.
Kama utakuwa unatumia muda wako hivyo tu kila wakati ujue kabisa
unajiangusha wewe kwa kurudi nyuma.
Jambo
la pili, ambalo linaweza likafanya upande ngazi yako ya mafanikio kwa kushuka chini
badala ya kwenda juu ni nguvu zako. Inatakiwa ifike mahali utambue nguvu zako
unazitumia kwenye mambo gani.
Haiwezekani
kufanikiwwa kama nguvu zako unazielekeza sana kwenye mambo ambayo hayawezekani
yaani mambo ya hovyo. Ni vyema kutumia nguvu zako kwenye mambo ambayo yanakupa
mafanikio na sio kinyume cha hapo.
Kama
unaona kuna jambo linakupotezea nguvu zako, bila kujali nguvu zako ni za
kufikiri au kusema, lakini kama linakupotozea nguvu zako na wewe hufaidi na
kitu chochote, nakushauri sana achana na jambo hilo mara moja kwani halikufai.
Watu
wenye mafanikio hawapotezi nguvu zao hovyo, ni watu wa kuhakikisha wanatumia
nguvu zao kwa ufasaha mkubwa sana. Na wewe unaweza ukawa ni miongoni mwao ukatumia
nguvu zako vizuri na zikakusadia kufanikiwa.
Kwa
namna yoyote hutakiwi kupote nguvu zako kwa kitu kinachokuridisha nyuma. Unatakiwa
sana kuchunga nguvu zako na zikatumika vizuri kwa manufaa ya mafanikio yako
makubwa ya leo na ya kesho pia.
Kitu
cha kuzingatia hapa ni kwamba, ukishindwa kuzingatia mambo haya mawili yaani
matumizi yako ya muda na matumizi yako ya nguvu zako, ujue utashindwa tu. Ni lazima
kujua umuhimu wa kutumia nguvu zako na muda wako vizuri sana.
Haya
mambo mawili ndiyo yanayowapa watu
mafanikio sana, nimesema muda na matumizi ya nguvu zako. Ukiwachunguza watu
waliofanikiwa wanatumia muda na nguvu zao vizuri, watu hawa hawapotezi muda wao
au nguvu zao kwa namna yoyote ile.
Kuanzia
sasa, anza kutumia muda wako vizuri na anza pia kutumia nguvu zako vizuri.
Usifanye vitu ambavyo vitakupotezea muda na nguvu zako. Haya ni mambo ya muhimu
sana na kwenye mafanikio yako na vitakusaidia kufikia kwenye kilele cha
mafanikio.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686
141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.