Feb 4, 2018
HEKIMA ZA MAISHA NA MAFANIKIO; Maelezo Marefu, Mwisho Huleta Uongo.
Habari
rafiki na karibu katika wakati mwingine wa kuweza kujifunza hekima za maisha na
mafanikio kama ilivyo kawaida ya siku yetu ya leo. Kupitia hekima hizi zinatupa
nafasi ya sisi kujifunza mambo ya kale kwa upya kabisa na tofauti.
Huwezi
kutoka vile vile ikiwa utakuwa unajifunza hekima hizi, kwani zitakusaidia wewe kuyaangalia
maisha yako kwa jicho la kitofauti. Sasa nikukaribishe uchukue kalamu na karatasi
na ukaribie jamvini ili tuweze kujifunza kwa pamoja.
1. Mtu anayehamisha mlima, anaanza na
jiwe moja.
Hakuna
kinachoshindikana kwenye maisha ikiwa wewe utaamua sasa kwamba ni nini unakitaka.
Yawe ni matatizo ukitaka yaondoke yataondoka au uwe ni mradi fulani, ukitaka
kuufanya utaufanya na utakupa matokeo.
Hekima
hii inatuonyesha na inatutaka tuwe wavumilivu na kujua kwamba kila kitu
kinaweza kubadilika kikipewa muda. Ndio maana hekima inasema hata mtu ayetaka
kuhamisha mlima huwa anaanza na jiwe moja.
Kwa hiyo
hata wewe usizuiliwe na kitu chochote, anza kuhamisha jiwe moja moja kwa
chochote kile unachokifanya na itafika utafanikiwa. Usitishike na ukubwa wa
mlima ulionao, anza kuhamisha wewe jiwe moja moja na mafanikio utayaona.
2. Watu ndio muhimu, vitu vingine
tunavipata tu.
Katika
hekima hii ya maisha na mafanikio inatuonesha unaweza ukapoteza pesa ukaipata,
unaweza ukapoteza kitu chochote kile na ukakipata, lakini si kupoteza mahusiano
au watu wako wa karibu na wenye msaada.
Msisistizo
wa hekima hii unaonyesha, ni muhimu kutunza mahusiano bora ya watu na si kuyapoteza
hovyo hovyo, kwani kupoteza kabisa mahusiano hayo linakuwa ni jambo la hatari
ambalo linatufanya tuishi kama kisiwa.
Mahusiano
bora ndio msingi mkubwa wa mafanikio yetu pia. Inapotokea ukawa ni mtu wa
kupotezea watu na kuthamini vitu, hiyo kwako unakuwa unajiweka kwenye hatari. Unapaswa
kukumbuka kwamba watu ni muhimu, vingine
tunavipata tukiweka juhudi.
3. Maelezo marefu, mwisho huleta uongo.
Kila
mmoja anapaswa kujua anatakiwa kuwa mtu wa kutokutoa maelezo marefu sana kwa
kitu ambacho kinaeleweka. Inatakiwa kueleza kitu kwa ufasaha na ikaeleweka pale
kinapotakiwa na watu wakalitambua hilo.
Katika
hekima hii, inatuonyesha kwa uwazi kwamba, maelezo marefu mwisho wa siku huleta
uongo. Ni jukumu lako kujua pale unapaonza kujielezea sana kupitiliza ujue
uongo unaweza ukafata hapo.
Hilo
unaweza ukaliona kwa watu waongo ni kipi wakifanyacho. Watu waongo mara nyingi
wanatumia maelezo marefu sana kama sehemu ya kutetea uongo wao. Hivyo,
tunaambiwa malezo marefu mwisho wa siku huleta uongo, tafakari.
Fanyia
kazi hekima hizi na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.