Feb 6, 2018
Usikubali Mambo Haya Yakuzuie Kufanikiwa.
Yapo mambo mengi ambayo yanaweza
yakawa chanzo cha kushindwa kwetu. Kwa leo nitakutajia mambo mawili tu, nimeamua kuyataja hapa kwa sababu
ndio mambo ambayo yanawazuia watu wengi sana kushindwa kuweza kufanikiwa.
Ukiwatazama watu wengi ambao
wameshindwa ndani mwao wanayo sana mambo hayo na ambayo wanakuwa wanayashikilia
sana na unakuta inakuwa ndio chanzo cha anguko lao la kushindwa kuweza kufikia
mafanikio.
Jambo
la kwanza ni hofu. Watu wengi wamekuwa wakikwama kwenye maisha
yao kwa sababu ya hofu kubwa. Hofu hii imekuwa ikiwazuia kuchukua hatua na
wakati mwingine hofu hii imekuwa ikiwazuia hata kuthubutu kuchukua hatua ndogo ndogo.
Kwa kawaida unapokuwa na hofu
sana huwezi kufanya kitu kwani kila kitu unakuwa unaogopa hali ambayo
inapelekea wewe inakuwa ni ngumu sana kuweza kufanikiwa kwako mpaka pale
utakapokuwa umeziweka hofu pembeni.
Umeshawahi kujiuliza au
kutambua ni kwa jinsi gani ambavyo hofu zako zinavyochangia katika kukuangusha
wewe. Kama ulikuwa hujui kuanzia sasa unatakiwa ujue hilo kwamba hofu inaweza
ikakuzuia ukashindwa kufanya mambo mengi sana.
Unatakiwa kuachana na kila
aina ya hofu na kisha kuvaa moyo wa kijasiri ambapo utaweza kukabiliana na vitu
vingi na ukashinda. Ikiwa hautafanya hivyo utazidi kuwa mtu wa kushindwa sana
maishani mwako.
Hakuna mshindi katika maisha
ambaye amejawa na hofu za kupitiliza. Ni jukumu lako wewe kuanzia sasa
kuhakikisha kwanza hofu unaziweka pembeni ili kusonga mbele. Ukiweka hofu
pembeni, jiandae kuanza kuwa mshindi wa mafanikio yako.
Jambo
la pili ni kukatataliwa. Inatakiwa uelewe kukatliwa kunakuwa
kunauma sana pale unaporuhusu kukataliwa huko kukuumize. Mtu anapokwambia
hapana, haimaanishi yeye ndiye yupo sahihi, hata yeye anaweza asiwe sahihi kabisa.
Usione vibaya kile unachokifanya
kinapokataliwa kwa namna moja au nyingine. Tafuta njia au majibu kwa nini kitu
hicho kinakataliwa. Unapopata majibu hayo inabidi yakusaidie kuweza kuendelea
mbele zaidi.
Lakini kuchukua hatua ya
kusikitika sana na kuanza kujiona yaani wewe ndio hufai eti kwa sababu kuna mtu
amekukatalia utakuwa unajikosea wewe. Kumbuka kuchukulia kukataliwa huko kama
fundisho kwako na si vinginevyo.
Chunga sana kila wakati mambo
haya mawili yasikuzuie wewe kuweza kuchukua hatua za kuweza kufanikiwa. Usikubali
hofu na wala usikubali kukataliwa kwa namna yoyote ile ndio kukazuia safari
yako ya mafanikio.
Usiwe miongoni mwa watu
ambao wanashindwa kwa sababu ya kuzuiliwa na hofu na kukataliwa. Washindi katika
maisha wanajua vizuri namna ya kukakabiliana na mambo hayo na hadi kuweza kushinda
na kufikia ngazi ya juu kimafanikio.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686
141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.