Feb 20, 2018
Usitegemee Kufanikiwa Kama Hautafanya Jambo Hili Mapema.
Kufanya
maandalizi ya kitu chochote kile ni jambo la muhimu sana kwako na pia ni moja
ya dalili nzuri kwamba unajiandaa kuwa mshindi kwa kitu hicho unachokifanya. Kama
haufanyi maandalizi ni rahisi tu kushindwa na hilo halina ubishi.
Ndio
maana unaona mwanafunzi ni lazima ajiandae mapema ili aweze kufaulu mtihani
wake, ndio maana unaona mkulima anaandaa shamba lake mapema pia ili wakati wa
kilimo ukifika ili aweze kufanikisha kilimo chake.
Hiyo
haitoshi unaona pia, mwana riadha anaanza kufanya mazoezi mapema ya kukimbia ili wakati ukifika aweze kushinda
mbio hizo, hiyo yote inaonyesha maandalizi ni kitu cha muhimu sana kwa ushindi
wowote ule.
Hakuna
mshindi anayetokea au kuibuka tu kiholela pasipo kuwa na maandalizi yale ya mwanzo
ya kuweza kujifua haswaa ili kutengeneza ushindi huo. Kila ushindi unaouona
umetokezea kwa nje, ujue kabisa ushindi huo umeandaliwa na haujaja kwa bahati.
Unapaswa
ukumbuke pia hata wakati ule wa Nuhu. haikuwa kipindi cha mvua au gharika
wakati Nuhu anajenga safina, bali Nuhu alifanya maandalizi ya mapema na gharika
inayokuja mbele yake na hilo kweli lilikuja kutokea.
Halikadhalika
na wewe unatakiwa kujenga maisha yako kwa ubora sana kipindi ambacho mambo yako
hayajaanza kuharibika au mambo hayajaanza kubanana na mpaka ukasombwa na
gharika ya changamoto.
Unatakiwa
kujua kwamba wakati wa kutengeneza maisha yako ni sasa wakati bado una nguvu za
kutosha ni si baadae. Huu ndio wakati wa kutengeneza safina ya maisha wakati
hali, nguvu na muda wako bado vinakuruhusu.
Kitafika
kipindi ambacho hautakuwa na uwezo huo yaani muda utakuwa huna, na wala nguvu
utakuwa huna. Angalia sana usije ukaanza kulia kama wale watu waliokuwa
wakimlilia Nuhu wafungulie kwenye safina, lakini akawaambia hakufunga yeye
mlango.
Hata
wewe angalia usije ukafika muda ambao utaanza kuwalilia watoto wako, ukaanza kuwalilia
wajukuu wako wakati utakapoanza kusombwa na maji na ukiangalia ulishindwa
kujenga safina yako mapema. Wakati wa kufanya na kukazana ni sasa na si kesho.
Kwa nini
usubiri mabaya ya kukute ili upambane nayo wakati una uwezo wa kujindaa sasa
mapema na kuyaepuka. Huhitaji kusubiri kitu, unahitaji kufanya kitu kwa ajili
ya maisha yako ya kesho bila kujali hli uliyonao kwa sasa ni ipi.
Hebu
nikuulize kitu, kama utashindwa kutengeneza maisha yako sasa na yakaonekana yana
maana, je, utaweza kweli ukishazeeka. Hapo ulipo ni kijana umeshindwa je,
ikifika uzeeni utaweza? najua hutaweza hata ufanyaje.
Ndio
maana unatakiwa kuweka juhudi sana za kuhakikisha unafanya kila kinachowezekana
wakati bado damu yako ina chemka, wakati bado una nguvu ili ufanikiwe. Nikwambie
tu ukisubiri, jiandae kusombwa na gharika ya changamoto za maisha.
Na ubaya
wa gharika inakuwa haina msamaha au hakuna kupona, ikikukuta ujue ndio tayari
umeshaenda. Kwa hiyo usikubali kupoteza maisha yako ya mafanikio kwa sababu ya
kushindwa kufanya maandalizi mapema.
Kuanzia
sasa fanya maandalizi mapema kwa kila kitu ambacho unachokifanya. Usipofanya maandalizi
mapema utaanguka na utajiangusha wewe mwenyewe na kutakuwa hakuna mtu ambaye
ataweza kukuamsha tena.
Ndiyo
maana, unatakiwa uweke akiba mapema kipindi ambacho kabla hujaishiwa. Unatakiwa
uzime moto mapema, kabla moto haujawaka vya kutosha. Ni muhimu kufanya
maandalizi mapema ya chochote kile ukifanyacho ili ikusaidie kuwa mashindi.
Kama
hautafanya maandalizi ya mapema kwa chochote unachokifanya kushindwa hautaweza
kukwepa hata kidogo. Kumbuka hata Nuhu alijenga safina mapema, kabla hata
gharika haijafika. Tafakari na chukua hatua.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686
141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Blog; dirayamafanikio.blogspot.com,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.