Feb 8, 2018
Mbinu Itakayokusaidia Kuwa Karibu Na Wateja Wako Ni Hii.
Miongoni
mwa changamoto ambazo huwakabili wafanyabiashara wengi ni kuwapoteza wateja
wengi bila wao kujua. Na tatizo hilo huanza kutokana na wafanyabiashara hao
kutokuwa na mawasiliano thabiti kati yao na wateja.
Kwa kutambua
hilo Siku ya leo nitakupa mbinu itayaokusaidia kuwa karibu na wateja wako. Na
mbinu hii endapo utaamua kuitumia itakusaidia sana katika biashara unayoifanya.
Nasema
hivi nikiwa nina ushahidi wa kutosha kwani mimi binafsi mbinu hiyo imenisaidia
kuweza kuwa karibu na wateja wangu na hatimaye naona matunda yake. Ni mbinu ambayo inafanya kazi vizuri sana
ukiitumia.
Na
mbinu hiyo siyo nyingine bali ni kuwa na mawasiliano thabiti baina yako na wetaja
wako au kwa lugha ya kitaalamu huitwa ‘customer database’. Customer database ndiyo ambayo hutumiwa
na makampuni mbalimbali.
Kwa
mfano makampuni ya simu hutumia mbinu
hii ili kumjuza mteja ujio wa bidhaa, punguzo la bei, au kumjuza mteja taarifa
muhimu kuhusu huduma husika. Kwa hiyo taarifa zote za mteja zinakuwa hapo.
Na
kwa kufanya hivi kumewafanya wateja kupata taarifa sahihi na kwa muda sahihi kuhusu huduma ambayo hutolewa na kampuni
husika. Mteja anakuwa hakosi taarifa sahihi kwa sababu anakuwa anatumiwa mara
kwa mara.
Kwa
kuliona hili nimeona ni vyema nawe ukatumia mfumo wa aina hii ili uwe karibu na
wateja wako, mawasiliano thabiti huweka ukaribu baina na
wateja wako, hii haijalishi ni biashara gani ambayo unaifanya.
Bali
kitu cha muhimu cha kuzingatia ni kuhakikisha unafanya hivyo ili uwe unawajuza
wateja wako kuhusu biashara unayoifanya. Kama kuna mabadiliko yeyote
yanayayohusu biashara yeyote unayoifanya basi usisite kuwajuza wateja wako.
Jinsi ya kuandaa mfumo wa mawasilino wa
wateja wako (customer database)
Mfano;
JINA LA MTEJA
|
NAMBARI ZAKE ZA SIMU
|
BARUA PEPE YA MTEJA
|
MAHALI ANAPOISHI
|
|
1.
|
BENSON
CHONYA
|
0757-909942
|
bensonchonya23@gmail.com
|
KIMARA-DSM
|
2
|
IMAN
NGWANGWALU
|
0713-048035
|
dirayamafanikio@gmail.com
|
LUSHOTO-TANGA
|
3
|
XXXXX
|
06XX-XXXX
|
XXXXX@gmail.com
|
MIYOMBONI-IRINGA
|
Hivyo ndivyo muundo wa 'customer database' ambavyo unatakiwa kuwa.
ANGALIZO:
KUMBUKA MAWASILIANAO HAYO YAWE KWA AJILI
YA BIASHARA TU, ENDAPO UTAIFANYA VINGINEVYO KUMBUKA LOLOTE LINAWEZA KUKUTOKEA.
Fanyia
kazi mfumo huo wa ‘customer data base’ ili uwe na msaada kubwa kwako na kumbuka pia kuchukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686
141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako afisa mipango wa mafanikio yako,
Benson Chonya,
Mawasiliano; +255 757-909942,
Email; bensonchonya23@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.