Feb 1, 2018
Kama Unataka Kuwa Mfanyabiashara Mwenye Mafanikio Hakikisha Una Kuwa Hivi.
Katika sayari
hii idadi kubwa ya shughuli ambazo hufanywa na mwanadamu ni
biashara, kama ndivyo hivyo basi naomba niweze kujikita zaidi katika
kulizungumzia jambo hilo siku ya leo. Na siku ya leo nataka kusema jambo moja
ambalo kila mfanyabishara anapaswa kulifahamu ili kujikuza katika biashara
yake.
Na jambo
hilo wafanyabiashara walio wengi wamekuwa wakilitumia kinyume chake
hata kupelekea wao wenyewe kutokufanya vizuri katika tasnia ya biashara. Wengi
wa wafanyabiashara wanafikiria kufanya hivyo ni kukua kibiashara kumbe si
kweli.
Japo hilo si lingine
bali kusema uongo juu ya biashara ambazo wanazifanya. Jambo hili
limekuwa likiwafanya wateja wengi kuhama na kwenda sehemu zingine, na kitendo
hicho hufanya mfanyabiashara kupoteza wateja bila ya yeye mwenyewe
kujijua.
Na kutoka na uongo
ambao wanautumia wafanyabiashara wengi wamekuwa , vinara wa kulalama ya kwamba
vyuma vimekaza, huku wao wenyewe ndio chanzo cha kukuza kwa vyuma hivyo kwani
wamekuwa wakiwafukuza wateja hao njia ya udanganyifu.
Inawezekana ukawa bado
hujanielewa ipo hivi, hivi hujawahi kununua kitu fulani huku
mfanyabiashara aliyekuuzia kitu hicho akikukwambia kitu hicho ni original, ila
baada ya kukitumia kitu hicho ukakikuta ni feki? Hivi hujawahi kula chipsi za
jana huku mfanyabiashara wa chipsi akakwambia hizi ni za leo leo. Bila shaka
umewahi kukutana na uongo wa aina hii.
Kwa athari ambazo
ulikutana nazo mara baada ya kununua vitu hivyo ukiwa kama mteja , swali
linakuja je unadhani je? unadhani utakwenda kununua kitu kilekile kwa yule
ambaye alikuuzia hapo awali? Bila shaka hakuna ambaye atadiliki kufanya hivyo.
Swali linakuja ni nini
Kifanyike?
Binafsi nadhani lipo
jambo la muhimu ambalo kila mfanyabiashara anapaswa kulifahamu hasa pale
anapofanya biashara yale na jambo hilo sio jingine bali ni kuwa muwazi wa
wateja wake. Kuwa muwazi kwa wateja wako hukufanya ukue kibiashara na kufanya
kuongezeka kwa wateja.
Unapoingia katika
fungu la kuwa mfanyabiashara muongo fahamu fika unapoteza wateja wako.
Kumueleza mteja ukweli kuhusu bidhaa au huduma unayoitoa kunakufanya uweze
kudumu katika biashara yako na kumiliki wateja kwa muda mrefu.
Hivyo ndugu yangu kama
kweli unataka kuwa mfanyabiashara mwenye mafanikio ni vyema ukachagua fungu
lililo jema kwako kwa kuamua kuwa ni mtu wa kusema ukweli katika biashara
ambayo unaifanya. Kama kitu ni origino basi uwe unamaanisha.
Mpaka kufikia hapo
sina la ziada nikutakie siku njema na mafanikio mema.
Ndimi; Afisa mipango
Benson chonya
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.