Jun 1, 2020
Kama Unataka Kufanya Mabadiliko Makubwa Katika Maisha Yako, Hakikisha Unasoma Hapa.
Ili tuweze kufanikiwa,
kuridhika na kuyafurahia maisha ya mafanikio, wakati mwingine hutulazimu
tubadilike. Suala hili la kubadilika lipo kwa ajili yetu, hata kama hatuko tayari
kufanya hivyo. Tunaishi katika dunia ambayo inabadilika kila siku. Sasa, iwapo
dunia hii iko tayari kubadilika , kwa nini binadamu agome kubadilika kama
umuhimu huo upo?
Hata hivyo,
tunapokusudia kufanya mabadiliko kwenye maisha yetu, hilo huwa ni jukumu zito
na gumu. Kwa mfano pale tunapoamua kubadili mambo fulani, huwa tunaamua
kuyaondoa mambo yote ya zamani na kuleta mambo mapya ambayo hatuna uzoefu nayo.
Hali hii inaweza ikasababisha tuyumbe, tuogope na hata tukose mwelekeo.
Hata hivyo, tunaweza tukakabiliana
na hata kupunguza madhara ya hali hii yenye wasiwasi na mtikisiko iwapo tutajua
jinsi ya kukabiliana na mabadiliko haya kwa njia ambazo ni imara kwetu.
Haitakuwa rahisi kwetu tena kuyumba na kuanguka kwani hiyo itakuwa na sawa
tumejishikiza katika nguzo imara, ambayo sio rahisi kuweza kubomoka.
Ni lazima na muhimu
sana kwetu kufanya mabadiliko hata kama wakati mwingine akili na miili yetu
huwa inatugomea. Kumbuka, hauwezi kufanikiwa kama hautafanya mabadiliko katika
maisha yako, utaendelea kubaki vilevile siku zote. Na kama unataka kufanya mabadiliko haya makubwa katika maisha yako,
hakikisha unafanya mambo haya:-
1.Kudhamiria
na kujitoa kikamilifu.
Ni muhimu sana kwetu
kudhamiria na kujitoa kikamilifu katika kufanya mabadiliko tunayoyahitaji
katika maisha yetu. Hata hivyo, kudhamiria na kujitoa huku kunaweza
kutudanganya kama hatutaweza kuwa waangalifu kwa kiasi cha kutosha. Hapa
namaanisha kwamba, sisi wenyewe tunaweza tukajigawa katika sehemu mbili.
Sehemu moja inakuwa iko
tayari kufanya mabadiliko na sehemu inayobaki inakuwa haiko tayari kufanya
mabadiliko. Hivyo, kunakuwepo kudhamiria kunakoshindana. Mara nyingi,
kudhamiria kunakoshindana husababisha upinzani. Na katika juhudi za kupambana
na upinzani huu hatimaye tunajikuta tunakata tamaa na kushindwa kufikia kwenye
malengo yetu.
Hali ya kudhamiria
kushindana inapokuwepo ndani ya mtu humfanya mhusika aanze kuhujumu juhudi zake
binafsi za kukamilisha mabadiliko anayoyataka. Hapa, visingizio na sababu
nyingi hutolewa kwa lengo la kuhalalisha kushindwa. Hapa, lawama nyingi
kutolewa na watu wengine walioko nje na ambao hawahusiki na mabadiliko
tunayotaka kufanya.
Hali hii huhujumu na
kuharibu morali au ari ya kufanya mabadiliko. Mara nyingi , siyo rahisi kwa mtu
kutambua kwamba, upinzani anaopata unatoka ndani mwake mwenyewe. Vilevile
upinzani huu humpeleka mtu kwenye utaratibu mwingine nje ya ule unaohusu
mabadiliko anayotaka . Hivyo basi, ni muhimu kudhamiria na kujitoa ili
kuushinda upinzani.
2.Tunahitaji
kuwa na Muundo.
Hili ni suala la muhimu
na la msingi katika kuharakisha mabadiliko unayoyataka, lakini mara nyingi
suala hili limekuwa halizingatiwi ipasavyo. Muundo ndiyo unaoshikilia na
kudhibiti mchakato mzima wa mabadiliko
tunayoyataka kufanya. Unahusu rasimali zote tunazotaka kutumia na mifumo
itakayotusaidia wakati tunafanya mabadiliko hayo.
Hivyo, muundo
ndiyo utakaotuhakikishia usalama wetu
wakati wa mabadiliko. Unaruhusu tushirikiane na magumu na changamoto zetu na
watu wengine, na hivyo kutupunguzia mizigo. Pia unatuhakikishia mafanikio. Kwa
maneno mengine nguzo hii ndiyo inayotupatia watu wa kutusaidia na kututia moyo,
wa kusherehekea nao tunapofanikiwa, wa kutukumbusha na kutuhamasisha.
Hivyo ni muhimu kwa mtu
kuwa na muundo uliothabiti ambao utatoa msaada kwake kwa kiwango kinachotakiwa wakati
anapitia kwenye mabadiliko. Ingawa suala la mafanikio ni gumu na linalotisha,
lakini linawezekana pia ukiamua. Ikiwa utajiandaa vizuri na kwa ukamilifu,
ndivyo utakavyojikuta unarahisisha na kufanikisha safari yako ya mabadiliko.
3. Jambo
jingine muhimu ni suala la ufanisi.
Kuwa na ufanisi binafsi
utakaokuwezesha kusonga mbele ni kitu muhimu sana kwako. Hapa tukiwa na maana
kuwa wakati mwingine suala zima la ujuzi au uzoefu huwa unahitajika katika
kuleta mabadiliko unayoyataka. Pia kuwa na muda, nishati na uwezo unaohitajika
kwa ajili ya kujifunza na kujipatia maarifa na ujuzi.
Kumbuka kama dunia
inabadilika kwa nini wewe usibadilike? Hivyo ndivyo unavyoweza kufanya
mabadiliko katika maisha yako kwa kufanya mambo hayo.
Nakutakia mafanikio
mema, endelea kutembelea mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO kwa
kujifunza vitu muhimu vitakavyobadili maisha yako.
TUPO PAMOJA MPAKA
MAISHA YAKO YAIMARIKE.
IMANI
NGWANGWALU
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.