Jun 29, 2020
Namna Sahihi Ya Kuendana Na Mabadiliko Ya Kidunia Kwenye Jambo Unalofanya.
Wakati
mwingine unapaswa kuelewa kwamba kile ambacho unakijua leo baada ya miaka
mitano ijayo kinaweza kisiwe na faida tena au kinaweza kisilete matokeo yale
ambayo mwenyewe unayapata kwa sasa. Nimesema hayo kwa sababu kwa hivi sasa
mambo yanabadilika sana.
Ile
dunia ya jana si dunia ya leo. Mambo kila kukiacha yanabadilika sana, watalamu
nao hawalali kutwa wanaumizwa vichwa vyao kuweza kugundua mbinu mpya ambazo ni
rahisi kwa mwanadamu kuweza kumrahisishia kazi mbalimbali.
Kama
nilivyosema hapo awali kwamba dunia inakwenda kasi hivyo ili kuendana sawa na mabadiliko hayo ni
kwamba hata wewe unapaswa kubadilika pia. Na njia pekee ambayo itakayokusaidia
kwa namna moja ama nyingine kuwa bora zaidi kwenye kila eneo unalofanyia kazi
ni kwamba unatakiwa kujiimarisha wewe mwenyewe kila siku.
Na
njia pekee itakayokusaidia kuweza kujiimarisha ni kwamba unatakiwa kuhakikisha
kwamba unaenda na mabadiliko yanayotokea kila siku, ni kujifunza mambo mapya kila wakati kwa sababu
usipojifunza mambo mapya ni kwamba utapitwa na vingi.
Ni
muhimu kuelewa kwamba kwenye kila sekta unayoifanyika kazi unapaswa kujifunza
namna ambavyo utakuwa bora kila wakati. Kumbuka kujifunza hakuna mipaka hivyo ni
muhimu sana kwako kuweza kujifunza mambo mbalimbali yatakayokusaidia kwa namna
moja ama nyingine kuwa bora zaidi kwenye kile unachokifanya kila wakati kwani
pindi utakaposhindwa kufanya hivyo ni kwamba hata wewe utapitwa na utashindwa
kuendana na kasi ya mabadiliko ya kidunia yanayotokea.
Kwa
muktadha huo, unapaswa kila wakati uwekeze muda mwingi kwenye kujifunza vitu
vipya kila siku. Kama wewe ni mkulima basi ni jifunze mbinu mpya kila siku zitakazokuwezesha
kufanikiwa zaidi katika kilimo hicho, kama wewe ni mtalamu wa jambo fulani basi
yakupasa kuweza kujipambanua zaidi kwa kujiwekeza kwenye kupata maarifa sahihi
juu ya jambo hilo.
Ni
muhimu kupata maarifa fulani kila wakati
kwa sababu kwa sasa dunia inakwenda kasi
sana hivyo bila kuwa na maarifa mapya ni kwamba utazidi kuwa mtu wazamani kila
siku , kwani kila kitu ambacho kitakuwa kinafanywa na watu wengine kwako
kitakuwa kigeni.
Mwisho
naomba nitamatishe kwa kusema ya kwamba kila wakati ongeza ubobezi kwenye kila
eneo unalofanyia kazi kwa sababu ubobezi humsaidia mtu kuweza kufanya jambo
lililo bora zaidi, pia kila wakati unapaswa kuelewa kwamba ubobezi hupatikana
kwa kuweza katika kujifunza vitu vipya kila siku ili uweze kuendana na
mabadiliko ya kidunia.
Ndimi: Afisa Mipango Benson
Chonya.
0757-909942
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.