Jun 23, 2020
Jifunze Mambo Haya Utafanikiwa.
Msingi wa maisha ya mafanikio upo kwenye kujifunza. Kupitia kujifunza kuna mambo mengi utayajua na yatakusaidia sana ikiwa utayafanyia kazi.
Kupitia makala haya, nimekuandalia mambo mbali mbali ya kujifunza katika maisha ili uweze kufanikiwa. Mambo hayo ni yepi, twende pamoja kujifunza.
1. Unapokuwa mjasiriamali unatakiwa uwe na maono, imani na moyo wa kusonga mbele. Hivi ni vitu vya msingi unatakiwa kuwa navyo. Kama utakosa kitu kimojawapo hapo, itakuwa ni ngumu sana kwako kuweza kufanikiwa.
VISION + FAITH + COURAGE.
Kama ukiwa na vitu hivyo, basi safari yako ya ujasiriamali itakuwa ya mafanikio. Hata Nuhu wakati anajenga safina alikuwa na vitu hivyo vitatu vya msingi sana na ambavyo kwa kila mjasiriamali anatakiwa awe navyo na kuvitumia.
Hebu fikiria, wakati nuhu anamwambia mkewe, na watoto wake kwamba anajenga safina, unafikiri watoto wake walimshangaa vipi, unafikiri mkewe na jamii ilimshangaa vipi? Hapa ni lazima Nuhu alionekana kituko.
Amini wengi walimwambia mzee unaota hii ni nchi ya jangwa, hakuna mvua kubwa ya namna hiyo ambayo inaweza ikanyesha. Inawezekana mzee Nuhu sasa unaelekea kuchanganyikiwa. Hayo ndio maneno alikuwa pengine akipewa.
Lakini, kwa sababu ya maono, imani na nguvu ya kuendelea mbele, Nuhu aliamua kufanya kazi hiyo bila kuchoka ya kujenga safina. Na mwisho wa siku safina ikapona na baada ya muda mvua ikanyesha.
Jiulize ukiwa mjasiriamali, je, una maono/vision? Je, una faith/Imani ya kukuongoza, je una courage/ moyo wa kuendelea mbele hata kama kuna watu wanakukatisha tamaa. Vitu hivi ni lazima na muhimu ili uweze kufanikiwa kwenye ujasiriamali wako.
2. Huwezi ukajifunza biashara kwenye kitabu, ni lazima uwe na biashara halisi na ambayo utakuwa unaifanyia mazoezi kila siku ili ikupe mafanikio. Kama unaishia kujifunza kwenye vitabu na kusema unajifunza biashara unapotea.
3. Marafiki hawana uwezo mkubwa wa kutengeneza biashara ya ushirika/ business partner. Jifunze kutengeneza biashara ambayo haina uwezo wa kuhusisha ushirika wa marafiki yaani hapa namaanisha business partner.
4. Ni muhimu kwako kuwa na kumbukumbu au rekodi za kipesa; kila pesa unayoitumia ni lazima iwe na rekodi zake. Usikubali kutumia pesa hovyo pasipo kuwa na kumbukumbu zake huko kunakuwa ni kujipoteza wewe.
5. Kuna wakati inachukua pesa nyingi, kutengeneza biashara ambayo unayoipenda. Si kitu cha mara moja, biashara sahihi inataka pesa, hivyo ukae hilo ukilijua akilini mwako kwamba pesa inahitajika.
6. Sio ukosefu wa pesa ndio unaua biashara, bali biashara zinakufa kwa sababu ya kukosa uzoefu kwenye biashara na kukosa kusema ukweli. Hayo ndio mambo mawili yanayoua sana biashara nyingi sana kila wakati.
7. Kila unaposhindwa, iwe kwenye biashara au kwenye jambo lolote. Hiyo inakuonyesha ni kwa jinsi gani ambavyo wewe hujui mambo mengi, na ni wapi urekebishe, kwa hiyo kushindwa kwako isiwe inshu, jifunze kwa kushindwa kwako.
8. Ni muhimu sana kuwa na elimu ya msingi wa pesa, mapema kwenye maisha yako. Ikiwezekana elimu hii, itafute kila siku na anza kuwapa watoto wako mapema, kwani itawasaidia kujenga msingi bora sana wa maisha yao ya kifedha.
9. Watu wengi wanafanya kazi hadi uzeeni kwa sababu, ni watu ambao wanakuwa bado hawajajiandaa na maisha ya uzeeni. Hata watu hao ukiwaona wamevaa suti na wamependeza, lakini wanakuwa hawajajiandaa na maisha, baada ya kustaafu.
10. Kama unatafuta pesa au unafanya uwekezaji wowote anza kuufanya kwanza kichwani mwako. Kama pesa utaanza kuiona kwenye akili yako, huku nje nako utaiona tu. Pesa ukiona kwenye akili kwanza, amini na kwa nje pia utaipata.
11. Kwenye maisha yako jifunze kuwa mwekezaji/investors na usiishie kuwa mfanyabiashara tu. Faida kubwa ya kuwa mwekezaji ni kwamba, hata soko likibadilika na kushuka sana bado mwekezaji ataendelea sana kutengeneza pesa ya kutosha na faida juu.
Uzuri wa mwekezaji ni kwamba anatengeneza pesa wakati wote. Kiwe kipindi kigumu pesa inatengenezwa au kipindi cha kawaida pesa inatengenezwa. Hivyo, mwekezaji hawezi kulia lia na mabadiliko yoyote yale ya kiuchumi kama alivyo mfanyabiashara.
12. Kila wakati unatakiwa kujua kwamba, kuna mabadiliko ya kiuchumi, ambayo yanaweza kutokea mbele ya maisha yako. Usifikiri hali ya uchumi ya sasa na ndio itakuwa kesho. Kaa, ukijua, maisha yanabadilika na wewe unatakiwa kubadilika.
13. Kama unaishi maisha yale yale, kama unachukua hatua zilezile, sahau kabisa maisha yako ya kesho kuwa bora kuliko yalivyo leo. Hiyo ni kwa sababu, hatua unazozichukua ni zile zile na hakuna mabadiliko, kwa hiyo hata matokeo ni yale yale.
14. Unaweza ukapoteza kila kitu, na ukajikuta umeingia kwenye ulimwengu halisi huna kitu. Hata hivyo nikwambie, unaweza ukarudi kule ulikotoka, na ukajenga mafanikio upya ikiwa wewe utaamua iwe kwako hivyo na ukachukua hatua madhubuti.
15. Ni vyema na ni vizuri kuwa na mpango sahihi wa kustaafu. Nchi, nyingi duniani zina mpango sahihi wa kustaafu kwa wananchi wake. Hata kampuni, zinaandaa mpango sahihi wa kustaafu kwa wafanya kazi wake. Na wewe unatakiwa uwe na mpango wako sahihi wa kujiandaa na uzeeni.
16. Watu wengi wenye maisha ya kati, wanashindwa kuwa matajiri kwa sababu, ya kukosa elimu ya pesa. Kwa kadri unavyokosa elimu ya pesa ndivyo uwekezaji kwako unakuwa mgumu na unajikuta unapoteza pesa nyingi ukiwekeza.
Dawa ni kuwa na elimu nzuri ya pesa, ili ukiwekeza uweze kufanikiwa. Ukikosa elimu ya pesa, unajiweka kwenye wakati mgumu sana wa wewe kuweza kufanikiwa. Anza kujifua na kuwekeza kwenye elimu ya pesa, itakusaidia sana kufanikiwa kwako.
17. Kuna elimu tatu za muhimu. Hizi ni elimu ambazo kila mmoja anatakiwa kuzijua zote, ingawa kwa bahati mbaya elimu mojawapo kati ya hizo tatu, haifundishwi shuleni.
Kwa kifupi, haya ndio Mambo ya msingi ambayo unaweza utajifunza kqmwenye maisha yako na kufanikiwa. Hebu chukua hatua na hakikisha ndoto zako zinatimia. Kila la kheri.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Shukrani
ReplyDelete