Jun 13, 2020
Mambo Muhimu Ya Kuzingatia Ili Uwe Kiongozi Mzuri Kazini.
Kuwa
kiongozi bora kazini inatakiwa kujifunza. Kuwa kiongozi kazini huwa haitokei
kama ajali bali mtu husika anatakiwa kujifunza namna ambavyo anatakiwa kuwa
hivyo. Hivi hujawahi ona umeajiriwa sehemu fulani lakini miaka nenda mika rudi
hujawa kuwa kiongozi hapo ofisini hata siku moja? Unafikiri ni wapi ambapo huwa
unakosea?
Kama
hujawahi kufikiri ni wapi ambapo uwa unakosea basi naomba nikupe mbinu hizi
ambazo zitakusaidia kwa namna moja ma nyingine ili uweze kuwa na wewe ni
kiongozi siku moja hapo ofisini kwako kwa kuzingatia mambo yafuatayo:
Unatakiwa
kujifunza kutoa maamuzi.
Miongoni
mwa mambo yatakayokusaidia kuwa kiongozi bora katika kampuni ni pamoja na kuwa
na uwezo wa kutoa maamuzi, na si maamuzi tu bali na maamuzi mazito yaliyojawa
na mtazamano chanya wa kuinuia au kuijenga ofisi yako.
Watu
wengi wamekuwa wakichemka sana katika hili, yaani unakuta mtu fulani kafanya
kosa fulani kazini ila anashindwa kumuwajibisha mtu huyo, jambo hili ndilo
tunaloita kukosa mtazamo na mwongozo wa namna ya kutoa maamusizi sahihi juu ya
mtu huyo.
Uwezo
wa kutafuta majibu ya changamoto.
Ili uwe
kiongozi bora katika kampuni au ofisi yako basi uanatakiwa kuwa ni kinara wa
kutafuta majibu ya kila changamoto inayojitokeza katika kampuni au ofisi
uliyopo, kila changamoto inayojitokeza katika ofisi fulani basi haitakiwa kuwa
kikwazo cha ofisi hiyo kufanya kazi zake kwa ufasaha bali wewe kama mmoja kati
ya wadau wa ofisi hiyo unatakiwa kiongozi na mstari wa mbele katika
kutatua changamoto hiyo kwa kutafuta majibu sahihi.
Uwezo wa
kushirikiana na watu wengine.
Unapokuwa
unafanya kazi fahamu kuwa ushirikiano na nguvu, na utengano ni udhaifu. Hivyo
kila wakati ili uwe kiongozi mwema kazini basi unatakiwa kuelewa namna sahihi
inayoweza kukusaidia kwa namna moja ama nyingine kuweza kusaidia katika
kutekeleza majukumu ya kiofisi ili kampuni au taasisi iweze kusonga mbele
kimafanikio kwa namna moja ma nyingine.
Miongoni
mwa faida utakazozipata pindi utakapoamua kuwa na ushirikianao na watu wengine
ni kwamba utaweza kujifunza mambo mbalimbali ambayo hapo awali wewe ulikuwa
hauyajaui. Pia kufanya kazi kwa ushirikiano husaidia sana kuongeza kasi ya
utendaji wa kazi husika, kwa mfano kazi iliyotakiwa kufanywa kwa muda mrefu
basi kazi itafanyika kwa muda mfupi.
Hivyo
kila wakati unatakiwa kubeba dhana hii “kufanya kazi kwa ushirikiano ni chachu
ya maendeleo” hivyo hakikisha unakuwa ni mtu wa kushirikiana na watu wengine
kadri uwezavyo ili kuweza kuleta maendeleo.
Uwezo
mzuri wa kuwasiliana.
Jambo
jingine litakalokusaidia kwa namna moja ama nyingine ili kuwa kiongozi
mzuri wa kiutendaji katika kazi yako ni vile ambavyo utaamua na kulibeba jukumu
la kuweza kuwasilina vyema na watu wengine.
Namna
ambavyo utaweza kuwasiliana vyema na wafanyakazi wengine, namna ambavyo utakuwa
una uwezo wa kuongea na wateja ndivyo ambavyo watu watakavyozidi kukuamini au
kuiamini ofisi ambayo unaifanyia kazi.
Ukiweka
kinyongo na maslai mengine binafsi nyuma husasani suala la mawasiliano ndivyo
ambavyo utavyokuwa unaiua kampuni pasipo wewe mwenyewe kujua.
Mtu mmoja
aliwahi kusema “watu mara nyingi huwa hanunui bidhaa yako tu, bali hununua
mahusiano yaliyopo kati yake na yako”. Mahusiano haya mara nyingi hujengwa na
mawasiliano yaliyo kati yako na yake. Hivyo kila wakati ili uweze kuwa ni mmoja
kati ya watu wenye chachu na shauku kubwa ya kufanya vizuri katika jambo
unalolifanya basi unatakiwa kuwa ni mtu ambaye unadumisha mawasilaino yenu
yaliyopo kati yako na wateja wako.
Ndimi
Afisa Mipango: Benson Chonya
0757-909942
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.